Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,475
Kiranga, let us agree to disagree.
Only if you are agreeing that you cannot answer my questions.
Kiranga, let us agree to disagree.
nitarudi hapa ni kitu kinavutia sana hiki.
Wadau,nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa, hapa nchini kuna sehemu wajerumani walichimbia rupia zao. Je sababu ya wao kuzichimbia na wasiende nazo kwao ni nini? Na kumekuwa na uvumi kuwa watu wanazitafuta sana, ni kwa ajili ya nini?
Na pia zimekuwa zikihusishwa na mambo ya ushirikina, kwamba huwezi kuzichimbua mpaka uwe na dawa kwa sababu zina mlinzi ambaye ni mzimu, je ni kweli? Kwa anayejua naomba anifafanulie tafadhani, nimeona kuna kamvuto ka kujua hii habari.
Tehethethet!! hii imekaa njema!!Waganga wakienyeji wana tabia ya kukuagiza kitu ambacho nikigumu kukipata,kwa mfano ukitaka cheopeleka nywele za kisogoni za boss wako.
Nimewahi kusikia pia, tena wanasema zimechimbiwa zaidi maeneo ya Tanga..
hata mimi nilisikia kwamba yapo Tanga, sababu ya kuleta mada hii hapa ni kwamba, nilisikia kuna watu walikuwa wanataka hizo rupia, wakaamua kwenda kwa mganga. Mganga akawaambia watoe pesa ili dawa ya kupata mahali zilipofukiwa inunuliwe, walipopata hiyo dawa wakaenda eneo la tukio, wakichukua na dhana zingine za kiganga ukiwemo mkuki.
Sababu ya kuchukua huo mkuki ni kwamba, hizo rupia zinalindwa na eagle (kwenye rupia kuna picha ya eagle ambae anasemekana ndie mlinzi) sasa huo mkuki utatumika kumuua ili rupia ipatikane. Basi wakafika eneo la tukio, mganga akafanya dawa, kisha akachoma ule mkuki ardhini kwa nguvu sana, akasema sasa eagle amekufa, wakafukua na kweli wakapata sanduku la rupia.
Wakachukua mzigo wakaweka kwenye buti ya gari tayari kwa safari ya kurudi eneo walilotoka, wakiwa njiani mara wakasikia kishindo kikubwa nyuma ya gari mpaka kioo cha nyuma kilivunjika, kutahamaki buti na yenyewe ipo wazi, kwenda kuangalia wakakuta sanduku halipo limetoweka.
Nikamuuliza huyo aliyekuwa ananisimulia, kwa nini ilitokea hivyo, akasema hizo mali zilizikwa na watu, ilikuwa wafanyakazi wa kwa mjerumani wanaulizwa, nani anataka kuwa mlinzi wa hii mali tumuachie maana tunarudi kwetu, atakaejitokeza kusema ni mimi, basi alikuwa anauwawa na mwili wake unazikwa na rupia, ndio maana mlinzi wake unakuwa ni mzimu ukiongozwa na eagle.
Nimevutiwa sana kujua zaidi habari hii ndio nikaona niilete hapa kwa great thinkers nikiamini nitapata ufafanuzi zaidi
Mhh kahadithi kakuvutia hako,sijasikiliza hizi simulizi muda mrefu sana,ebu endelea kutusimulia zaidi kitty nahakika unamengi zaidi ya haya uliyotupatia,karibu!