Rupia ya Mjerumani

Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Messages
347
Likes
10
Points
35
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined May 24, 2011
347 10 35
Wadau,nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa, hapa nchini kuna sehemu wajerumani walichimbia rupia zao. Je sababu ya wao kuzichimbia na wasiende nazo kwao ni nini? Na kumekuwa na uvumi kuwa watu wanazitafuta sana, ni kwa ajili ya nini?

Na pia zimekuwa zikihusishwa na mambo ya ushirikina, kwamba huwezi kuzichimbua mpaka uwe na dawa kwa sababu zina mlinzi ambaye ni mzimu, je ni kweli? Kwa anayejua naomba anifafanulie tafadhani, nimeona kuna kamvuto ka kujua hii habari.
 
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
29,404
Likes
7,469
Points
280
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
29,404 7,469 280
nitarudi hapa ni kitu kinavutia sana hiki.
 
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
9,937
Likes
1,749
Points
280
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
9,937 1,749 280
Ulongo mtupu.
 
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
20,002
Likes
1,627
Points
280
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
20,002 1,627 280
Huwa inasemwa sana,nafikiri ni uvumi tu.
 
tz1

tz1

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2011
Messages
2,128
Likes
45
Points
145
tz1

tz1

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2011
2,128 45 145
Waganga wakienyeji wana tabia ya kukuagiza kitu ambacho nikigumu kukipata,kwa mfano ukitaka cheo
peleka nywele za kisogoni za boss wako.
 
M

Mantaleka

Senior Member
Joined
Dec 14, 2008
Messages
104
Likes
0
Points
0
M

Mantaleka

Senior Member
Joined Dec 14, 2008
104 0 0
Hakuna atakaye kupa jibu sahihi juu ya hilo utakalo kulijua, wengine watakuambia ni uongo na wengine watakushangaa, amini vile wewe nafsi yako inavyo kuongoza kujua.
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,577
Likes
38,988
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,577 38,988 280
Wadau,nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa, hapa nchini kuna sehemu wajerumani walichimbia rupia zao. Je sababu ya wao kuzichimbia na wasiende nazo kwao ni nini? Na kumekuwa na uvumi kuwa watu wanazitafuta sana, ni kwa ajili ya nini?

Na pia zimekuwa zikihusishwa na mambo ya ushirikina, kwamba huwezi kuzichimbua mpaka uwe na dawa kwa sababu zina mlinzi ambaye ni mzimu, je ni kweli? Kwa anayejua naomba anifafanulie tafadhani, nimeona kuna kamvuto ka kujua hii habari.
vua hirizi yako kiunoni. Maana habari za rupia hazikai kabisa kichwani ukiwa umevaa hirizi.
 
Nding'oli

Nding'oli

Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
45
Likes
1
Points
0
Nding'oli

Nding'oli

Member
Joined Oct 6, 2010
45 1 0
Ukweli ni kwamba, hakuna cha maana kuhusiana na RUPIA za Kijerumani. Kwa sababu ya umasikini wetu tulio wengi, badala ya kufanya kazi tunategemea tupate nafuu ya maisha kwa miujiza. Kwa sababu hizo, wengi wamekuwa wepesi mno kujiingiza katika mtego wa wanaoitwa 'wataalamu'. Kama watu wangeamini kuwa kufanya kazi kwa bidii, kwa kutumia maarifa pekee ndiyo njia pekee ya kuondoa umasikini, kila mmoja angejitosheleza katika mahitaji yake ya lazima na NDOTO za utajiri bila kufanya kazi zisingekuwepo. Hata hao 'wataalamu' (waganga wa kufikirika) wangekosa pa kudanganya kwa kuwa wote wamejitosheleza.
Rupia za kijerumani hapo zamani sana wakati zilipoanza kutumika fedha kwa ajili kulipia mambo mbalimbali, coin zote zilitengenezwa kwa DHAHABU. Mpaka matumizi yalivyoongezeka ikakubalika kuwa badala ya DHAHABU vitumike vyuma vingine badala ya DHAHABU. Zilianza kutengenezwa kwa kutumia FEDHA na SHABA ambazo thamani yake ni ndogo. Baada ya kugundua kuwa DHAHABU ni mali, zile RUPIA za zamani zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia DHAHABU zikaanza kutafutwa kwa udi na uvumba. 'Wataalamu' wakaanza kuwadanganya watu waliowaendea kuuliza 'ni wapi watapata RUPIA za mwaka fulani zenye chapa ya simba n.k.' kuwa kila alipozikwa Mjerumani hapa Tanganyika kuna RUPIA alizikwa nazo. Makaburi yamechimbwa mengi mno, lakini hakuna aliyefaulu kupata. Mjerumani ni mjinga azike mali hivihivi tu? Maeneo ya Tanga Wajerumani walipenda sana kuishi wakiwa hapa Tanganyika wakati likiwa koloni lao. Hivyo pia walikufa na kuzikwa, ndio sababu uchimbaji ni mwingi sana huko kuliko sehemu nyingine za nchi, kwa kuwa yapo makaburi mengi ya Wajerumani. Asikudanganye mtu ukweli ndio huo. Ukiiokota Rupia ya wakati huo umeokota dhahabu na utaiuza kwa gramu zilizotengeneza RUPIA hiyo na si vinginevyo. Habari ndiyo hiyo ndugu yangu mtoa HOJA.
 
feis buku

feis buku

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
2,370
Likes
8
Points
0
Age
29
feis buku

feis buku

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
2,370 8 0
Waganga wakienyeji wana tabia ya kukuagiza kitu ambacho nikigumu kukipata,kwa mfano ukitaka cheopeleka nywele za kisogoni za boss wako.
tehethethet!! hii imekaa njema!!
 
B'REAL

B'REAL

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Messages
3,262
Likes
354
Points
180
B'REAL

B'REAL

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2010
3,262 354 180
jamanii mimii nina ushahidi na nnacho ongea,kama kunaa mtu ameshawai kufikaa Mwanga[usangi]sehemu inaitwaa shingatini,kuna sekondari pale ilaitwa shingatini na kanisaa la kwanzaa la KKT na ukumbuke katika historia kuna histori ya ugweno {usangi},mjerumani aliye kuwa missionary mkuu alikuwa ana itwa HANS FOCUS na amezikwa kwenye makaburi kando ya shule hiyo.

Sehemu hiyo kunaa mlimaa maarufu inaitwa KAMWALA.nishawai kupanda nikifatilia hizi tafiti kama ni kweli au laa.wazee wahapo walituambia zamani sanaa,walikujaa wajerumani wengi sanaa,wakiwa na baskeli zilizo na bendera za ujerumani,walikuwa na ramani.walipo fika hapo kanisani waliacha zile baskeli wakapanda huo mlima wakiwa na chifu na watu kama tano au kumi wenyeji.

Walikaa huko mlimani kwa masaa mengi tu na walipo rudi walirudi na sanduku.baadae walipo wauliza wezao na chifu walisema wale wajerumani waliondoka na sanduku lenye adhina kubwaa ya vitu vya dhahabu kama vikombe,fimbo,vijiko nk.nilivutiwa na story na nikataka kusibitishaa.

Tukiwa group ya watu kama kumi tulipanda ule mlima tukiwa na mwenyeji,ambae alitupeleka katika sehemu sanduku lilipo tolewa,amini usiamini nnacho kwambia ni kweli kuna kilaa dalili.kwanza nijiwee kubwa limeandikwa sign ambazo sio rahisi kufutika kama atua moja ndo kuna kama pango,tukadumbukiaa ndani ya hilo pango mmoja mmoja tukakuta ndani lina uwezo wa kukaa watu tano adi sita wakiwa wamesimamaa.

huko ndani kuna jiwee jingine ambalo nahisi hilo sanduku lilipo tolewaa,jiwe kubwaa katikati linaonyesha kulikuwa na kitu ndani yake,ukubwaa wa hiyo nafasi ambalo sanduku lilikuwa siwezi kusema kwani siku pimaaa.nazani ni histori nzuri ya kujifunzaa watu wengi wamesahau that history of pare.but its there and still living.

Wazee wanasemaa walishapoteza watu wengi wakitafutaa hiyo hazinaa mlima kamwalaa na hawakuwai kuipata kwani kulikuwa na jokaa kubwa katika eneo hilo.

AMINI USI AMINII
 
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Messages
347
Likes
10
Points
35
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined May 24, 2011
347 10 35
Nimewahi kusikia pia, tena wanasema zimechimbiwa zaidi maeneo ya Tanga..
Hata mimi nilisikia kwamba yapo Tanga, sababu ya kuleta mada hii hapa ni kwamba, nilisikia kuna watu walikuwa wanataka hizo rupia, wakaamua kwenda kwa mganga. Mganga akawaambia watoe pesa ili dawa ya kupata mahali zilipofukiwa inunuliwe, walipopata hiyo dawa wakaenda eneo la tukio, wakichukua na dhana zingine za kiganga ukiwemo mkuki.

Sababu ya kuchukua huo mkuki ni kwamba, hizo rupia zinalindwa na eagle (kwenye rupia kuna picha ya eagle ambae anasemekana ndie mlinzi) sasa huo mkuki utatumika kumuua ili rupia ipatikane. Basi wakafika eneo la tukio, mganga akafanya dawa, kisha akachoma ule mkuki ardhini kwa nguvu sana, akasema sasa eagle amekufa, wakafukua na kweli wakapata sanduku la rupia.

Wakachukua mzigo wakaweka kwenye buti ya gari tayari kwa safari ya kurudi eneo walilotoka, wakiwa njiani mara wakasikia kishindo kikubwa nyuma ya gari mpaka kioo cha nyuma kilivunjika, kutahamaki buti na yenyewe ipo wazi, kwenda kuangalia wakakuta sanduku halipo limetoweka.

Nikamuuliza huyo aliyekuwa ananisimulia, kwa nini ilitokea hivyo, akasema hizo mali zilizikwa na watu, ilikuwa wafanyakazi wa kwa mjerumani wanaulizwa, nani anataka kuwa mlinzi wa hii mali tumuachie maana tunarudi kwetu, atakaejitokeza kusema ni mimi, basi alikuwa anauwawa na mwili wake unazikwa na rupia, ndio maana mlinzi wake unakuwa ni mzimu ukiongozwa na eagle.

Nimevutiwa sana kujua zaidi habari hii ndio nikaona niilete hapa kwa great thinkers nikiamini nitapata ufafanuzi zaidi.
 
The last don

The last don

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2011
Messages
652
Likes
290
Points
80
The last don

The last don

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2011
652 290 80
hata mimi nilisikia kwamba yapo Tanga, sababu ya kuleta mada hii hapa ni kwamba, nilisikia kuna watu walikuwa wanataka hizo rupia, wakaamua kwenda kwa mganga. Mganga akawaambia watoe pesa ili dawa ya kupata mahali zilipofukiwa inunuliwe, walipopata hiyo dawa wakaenda eneo la tukio, wakichukua na dhana zingine za kiganga ukiwemo mkuki.

Sababu ya kuchukua huo mkuki ni kwamba, hizo rupia zinalindwa na eagle (kwenye rupia kuna picha ya eagle ambae anasemekana ndie mlinzi) sasa huo mkuki utatumika kumuua ili rupia ipatikane. Basi wakafika eneo la tukio, mganga akafanya dawa, kisha akachoma ule mkuki ardhini kwa nguvu sana, akasema sasa eagle amekufa, wakafukua na kweli wakapata sanduku la rupia.

Wakachukua mzigo wakaweka kwenye buti ya gari tayari kwa safari ya kurudi eneo walilotoka, wakiwa njiani mara wakasikia kishindo kikubwa nyuma ya gari mpaka kioo cha nyuma kilivunjika, kutahamaki buti na yenyewe ipo wazi, kwenda kuangalia wakakuta sanduku halipo limetoweka.

Nikamuuliza huyo aliyekuwa ananisimulia, kwa nini ilitokea hivyo, akasema hizo mali zilizikwa na watu, ilikuwa wafanyakazi wa kwa mjerumani wanaulizwa, nani anataka kuwa mlinzi wa hii mali tumuachie maana tunarudi kwetu, atakaejitokeza kusema ni mimi, basi alikuwa anauwawa na mwili wake unazikwa na rupia, ndio maana mlinzi wake unakuwa ni mzimu ukiongozwa na eagle.

Nimevutiwa sana kujua zaidi habari hii ndio nikaona niilete hapa kwa great thinkers nikiamini nitapata ufafanuzi zaidi
Mhh kahadithi kakuvutia hako,sijasikiliza hizi simulizi muda mrefu sana,ebu endelea kutusimulia zaidi kitty nahakika unamengi zaidi ya haya uliyotupatia,karibu!
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,577
Likes
38,988
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,577 38,988 280
yaani kama mama na mwana enzi za deborah mwenda redio tanzania
 
Nyamgluu

Nyamgluu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
3,144
Likes
98
Points
145
Nyamgluu

Nyamgluu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
3,144 98 145
Hahaha nimekumbuka mbali sana. Wakati nina miaka kumi na tatu (13) niliamua kutafuta rupia. Ilikua ni kutokana na curiosity na kuangalia movies kibao na cartoons za treasure hunting. Sasa every Saturday mama akienda kanisani mimi naingia chumbani na chukua shilingi mia 2 naenda pakia gari kutoka Iringa mjini hadi Kalenga. (alikozikwa mkwawa!!)

Hahaha dah the guts I had, sijui moyo wa adventure nime uzika wapi.

Anyway kwenye visit ya tatu nika pelekwa kwa babu mmoja ambae inasemekana angeweza nisaidia kupata. Kufika pale tukamkosa, nikaambiwa nirudi Juma5.

Sasa haikuwezekana kutoroka shule, so I solicited the help of a close friend!! Huyo jamaa angu mpaka ninavyoandika sasa ni ana usongo na rupia na madini na hivi sasa anatafuta almasi wapi kusini huko!! Hahaha kila nikimwona ananilaumu eti nimemponza na kuacha kutafuta hela za madini hawezi.

Anyways to cut the long story short, mshkaji alivyoenda alipewa masharti magumu saaaana na hatukuweza kutekeleza kutokana na kutokua na hela umri huo. Wakati naendelea kujipanga nikapelekwa shule boarding fasta. And that was the end of my quest for rupia!!
 
Beso

Beso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2011
Messages
216
Likes
6
Points
35
Beso

Beso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2011
216 6 35
[QUOTE=kijijini kwetu maeneo ya korogwe kuna mganga wa kienyeji jirani na kwetu inasemekana anayo,toka nikiwa mdogo wahindi na wafanyabiashara wengine kiguu na njia ikisemekana wanakuja kumshawishi awauzie hadi leo dili haijafanyika!!miaka zaidi ya 15!
 
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Messages
347
Likes
10
Points
35
Kitty Galore

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined May 24, 2011
347 10 35
Mhh kahadithi kakuvutia hako,sijasikiliza hizi simulizi muda mrefu sana,ebu endelea kutusimulia zaidi kitty nahakika unamengi zaidi ya haya uliyotupatia,karibu!
hata mimi nilivutiwa sana na simulizi za rupia, sina zaidi ndio maana nikaleta hapa lakini naona kama vile sio watu wengi wanafahamu hii habari ya rupia
 
IHOLOMELA

IHOLOMELA

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
1,743
Likes
1,426
Points
280
IHOLOMELA

IHOLOMELA

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
1,743 1,426 280
Wadau,nimekuwa nikisikia mara kwa mara kuwa, hapa nchini kuna sehemu wajerumani walichimbia rupia zao. Je sababu ya wao kuzichimbia na wasiende nazo kwao ni nini? Na kumekuwa na uvumi kuwa watu wanazitafuta sana, ni kwa ajili ya nini?

Na pia zimekuwa zikihusishwa na mambo ya ushirikina, kwamba huwezi kuzichimbua mpaka uwe na dawa kwa sababu zina mlinzi ambaye ni mzimu, je ni kweli? Kwa anayejua naomba anifafanulie tafadhani, nimeona kuna kamvuto ka kujua hii habari.
Kwa ufupi ni aina ya utapeli ambapo anakuja mtu mmoja kwako kama wewe ni mwenye pesa anatangaza kuitafuta rupia tena anasema dau kubwa, akiondoka baada ya siku kadhaa, anakuja mwenzake ambaye anatangaza kuuza rupia kwa bei ya chini kidogo tofauti na ile aliyotangaza yule wa kwanza. Let's say, jamaa alisema atainunua kwa 10milion, huyu mwenye nayo atasema anauza 7ml. Hivyo kwa kuwa wewe unataka faida, na jamaa kakuachia mawasiliano, unampigia kumwambia umepata rupia, hapo tapeli mnunuzi atakusisitiza uinunue yeye akija atakupa hiyo 10m..kwa tamaa zako unanunua ili upate faida nono ndani ya kipindi kifupi. Ukinunua tu, jamaa wanaenda kugawana hizo hela na huo ndio unakuwa mwisho. Pia kuna ujanja mwingine wa kitapeli wa kumtajirisha mtu kwa rupia..itategemea wamekuingia kwa gia ipi. But all in all, rupia ni utapeli. Be warned
 
B

Bryson Mbeula

Member
Joined
Sep 25, 2011
Messages
45
Likes
0
Points
13
B

Bryson Mbeula

Member
Joined Sep 25, 2011
45 0 13
Kwa ufupi ni aina ya utapeli ambapo anakuja mtu mmoja kwako kama wewe ni mwenye pesa anatangaza kuitafuta rupia tena anasema dau kubwa, akiondoka baada ya siku kadhaa, anakuja mwenzake ambaye anatangaza kuuza rupia kwa bei ya chini kidogo tofauti na ile aliyotangaza yule wa kwanza. Let's say, jamaa alisema atainunua kwa 10milion, huyu mwenye nayo atasema anauza 7ml. Hivyo kwa kuwa wewe unataka faida, na jamaa kakuachia mawasiliano, unampigia kumwambia umepata rupia, hapo tapeli mnunuzi atakusisitiza uinunue yeye akija atakupa hiyo 10m..kwa tamaa zako unanunua ili upate faida nono ndani ya kipindi kifupi. Ukinunua tu, jamaa wanaenda kugawana hizo hela na huo ndio unakuwa mwisho. Pia kuna ujanja mwingine wa kitapeli wa kumtajirisha mtu kwa rupia..itategemea wamekuingia kwa gia ipi. But all in all, rupia ni utapeli. Be warned
daah!ebwana eee,haya maisha yana mambo mengi kweli,nilishuhudia jirani yetu anafirisika hivi hivi kwa kutafuta rupia!
 
Forum statistics

Threads 1,250,505
Members 481,371
Posts 29,736,016