Number ni 26
JF-Expert Member
- Apr 3, 2019
- 1,478
- 2,834
Mkuu yan sio bure lazma kuna ndele inahusika kupumbaza watuHahahaha umenifanya nicheke nimemkumbuka jamaa yangu mmoja mkoani huko pita pita zangu nikamuona kakaa sehemu kama wana kikao vile chini ya mti yupo na wazee kibao kama kikao cha mwenyekiti wa mtaa vile...
Namuuliza hapo vipi kuna kitu gani eti ana niambia kuna rupia wamezipata eti wana jadili jinsi ya kuziuza..nilichoka kwa majibu yake halafu ni mtu wa heshima tu nilicho fanya ni kumuambia biashara njema huyo nikapotea maana hata ninge muelimisha kuhusu hayo mambo ningekuwa napoteza muda tu Maana asinge nielewa.
Sijui wale wajomba huwa wanatumia NGUVU za giza kuwatapeli watu au ni ujinga tu wa watu maana hata umuelimishe vipi mtu akuelewi mpaka akisha pigwa kwanza ndiyo akili ina mkaa sawa.
Sent using Jamii Forums mobile app