Rupia ya Mjerumani: Ni kweli sarafu hii ina thamani kubwa au ni story tu?

Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
128
Nimekuwa nikisikia muda mrefu kama simulizi hivi, kwamba rupia ya kijerumani ukiipata unatajirika!! Binafsi sielewi ni kwa namna gani hadi juzi hapa nimekutana na mtu mmoja ambaye tunafahamiana naye na ni mfanyabiashara akadai yeye ana taarifa kuhusu rupia ambayo iko sehemu, ila kwa maelezo yake ni kwamba rupia hiyo wajerumani ndio huwa wanatafuta na kwamba ukiwapatia wanatengeneza pesa za kutosha kutokana na rupia hiyo.

Na sababu iliyopelekea mtu huyo kunifuata ilikuwa kuniuliza kama nina fahamiana na mjerumani yeyote, kwani inasemekana kila mjerumani ni mjuzi wa utaalamu huu wa kutengeneza utajiri kwa njia ya rupia.

Kwa imani inaelezwa kwamba: Kama zoezi likienda vizuri huwa zinapatikana pesa za kutosha na hivyo watu wote ambao walihusika kwa namna moja au nyingine na upatikanaji wa rupia hiyo hupata mgao na kuwa matajiri. Kwa hivyo ninachopenda kufahamu kutoka kwa wana JF ambao wamewahi kusikia story kama hii wanijuze kuhusu mbivu na mbichi kuhusiana na nadharia hii.

========
Michango ya wadau
Ukweli ni kwamba, hakuna cha maana kuhusiana na RUPIA za Kijerumani. Kwa sababu ya umasikini wetu tulio wengi, badala ya kufanya kazi tunategemea tupate nafuu ya maisha kwa miujiza. Kwa sababu hizo, wengi wamekuwa wepesi mno kujiingiza katika mtego wa wanaoitwa 'wataalamu'.

Kama watu wangeamini kuwa kufanya kazi kwa bidii, kwa kutumia maarifa pekee ndiyo njia pekee ya kuondoa umasikini, kila mmoja angejitosheleza katika mahitaji yake ya lazima na NDOTO za utajiri bila kufanya kazi zisingekuwepo. Hata hao 'wataalamu' (waganga wa kufikirika) wangekosa pa kudanganya kwa kuwa wote wamejitosheleza.

Rupia za kijerumani hapo zamani sana wakati zilipoanza kutumika fedha kwa ajili kulipia mambo mbalimbali, coin zote zilitengenezwa kwa DHAHABU. Mpaka matumizi yalivyoongezeka ikakubalika kuwa badala ya DHAHABU vitumike vyuma vingine badala ya DHAHABU.

Zilianza kutengenezwa kwa kutumia FEDHA na SHABA ambazo thamani yake ni ndogo. Baada ya kugundua kuwa DHAHABU ni mali, zile RUPIA za zamani zilizokuwa zikitengenezwa kwa kutumia DHAHABU zikaanza kutafutwa kwa udi na uvumba.

'Wataalamu' wakaanza kuwadanganya watu waliowaendea kuuliza 'ni wapi watapata RUPIA za mwaka fulani zenye chapa ya simba n.k.' kuwa kila alipozikwa Mjerumani hapa Tanganyika kuna RUPIA alizikwa nazo. Makaburi yamechimbwa mengi mno, lakini hakuna aliyefaulu kupata. Mjerumani ni mjinga azike mali hivihivi tu?

Maeneo ya Tanga Wajerumani walipenda sana kuishi wakiwa hapa Tanganyika wakati likiwa koloni lao. Hivyo pia walikufa na kuzikwa, ndio sababu uchimbaji ni mwingi sana huko kuliko sehemu nyingine za nchi, kwa kuwa yapo makaburi mengi ya Wajerumani.

Asikudanganye mtu ukweli ndio huo. Ukiiokota Rupia ya wakati huo umeokota dhahabu na utaiuza kwa gramu zilizotengeneza RUPIA hiyo na si vinginevyo. Habari ndiyo hiyo ndugu yangu mtoa HOJA.
----
Jamanii mimii nina ushahidi na nnacho ongea,kama kunaa mtu ameshawai kufikaa Mwanga[usangi]sehemu inaitwaa shingatini,kuna sekondari pale ilaitwa shingatini na kanisaa la kwanzaa la KKT na ukumbuke katika historia kuna histori ya ugweno {usangi},mjerumani aliye kuwa missionary mkuu alikuwa ana itwa HANS FOCUS na amezikwa kwenye makaburi kando ya shule hiyo.

Sehemu hiyo kunaa mlimaa maarufu inaitwa KAMWALA.nishawai kupanda nikifatilia hizi tafiti kama ni kweli au laa.wazee wahapo walituambia zamani sanaa,walikujaa wajerumani wengi sanaa,wakiwa na baskeli zilizo na bendera za ujerumani,walikuwa na ramani.walipo fika hapo kanisani waliacha zile baskeli wakapanda huo mlima wakiwa na chifu na watu kama tano au kumi wenyeji.

Walikaa huko mlimani kwa masaa mengi tu na walipo rudi walirudi na sanduku.baadae walipo wauliza wezao na chifu walisema wale wajerumani waliondoka na sanduku lenye adhina kubwaa ya vitu vya dhahabu kama vikombe,fimbo,vijiko nk.nilivutiwa na story na nikataka kusibitishaa.

Tukiwa group ya watu kama kumi tulipanda ule mlima tukiwa na mwenyeji,ambae alitupeleka katika sehemu sanduku lilipo tolewa,amini usiamini nnacho kwambia ni kweli kuna kilaa dalili.kwanza nijiwee kubwa limeandikwa sign ambazo sio rahisi kufutika kama atua moja ndo kuna kama pango,tukadumbukiaa ndani ya hilo pango mmoja mmoja tukakuta ndani lina uwezo wa kukaa watu tano adi sita wakiwa wamesimamaa.

huko ndani kuna jiwee jingine ambalo nahisi hilo sanduku lilipo tolewaa,jiwe kubwaa katikati linaonyesha kulikuwa na kitu ndani yake,ukubwaa wa hiyo nafasi ambalo sanduku lilikuwa siwezi kusema kwani siku pimaaa.nazani ni histori nzuri ya kujifunzaa watu wengi wamesahau that history of pare.but its there and still living.

Wazee wanasemaa walishapoteza watu wengi wakitafutaa hiyo hazinaa mlima kamwalaa na hawakuwai kuipata kwani kulikuwa na jokaa kubwa katika eneo hilo.

AMINI USI AMINII
----
Hata mimi nilisikia kwamba yapo Tanga, sababu ya kuleta mada hii hapa ni kwamba, nilisikia kuna watu walikuwa wanataka hizo rupia, wakaamua kwenda kwa mganga. Mganga akawaambia watoe pesa ili dawa ya kupata mahali zilipofukiwa inunuliwe, walipopata hiyo dawa wakaenda eneo la tukio, wakichukua na dhana zingine za kiganga ukiwemo mkuki.

Sababu ya kuchukua huo mkuki ni kwamba, hizo rupia zinalindwa na eagle (kwenye rupia kuna picha ya eagle ambae anasemekana ndie mlinzi) sasa huo mkuki utatumika kumuua ili rupia ipatikane. Basi wakafika eneo la tukio, mganga akafanya dawa, kisha akachoma ule mkuki ardhini kwa nguvu sana, akasema sasa eagle amekufa, wakafukua na kweli wakapata sanduku la rupia.

Wakachukua mzigo wakaweka kwenye buti ya gari tayari kwa safari ya kurudi eneo walilotoka, wakiwa njiani mara wakasikia kishindo kikubwa nyuma ya gari mpaka kioo cha nyuma kilivunjika, kutahamaki buti na yenyewe ipo wazi, kwenda kuangalia wakakuta sanduku halipo limetoweka.

Nikamuuliza huyo aliyekuwa ananisimulia, kwa nini ilitokea hivyo, akasema hizo mali zilizikwa na watu, ilikuwa wafanyakazi wa kwa mjerumani wanaulizwa, nani anataka kuwa mlinzi wa hii mali tumuachie maana tunarudi kwetu, atakaejitokeza kusema ni mimi, basi alikuwa anauwawa na mwili wake unazikwa na rupia, ndio maana mlinzi wake unakuwa ni mzimu ukiongozwa na eagle.

Nimevutiwa sana kujua zaidi habari hii ndio nikaona niilete hapa kwa great thinkers nikiamini nitapata ufafanuzi zaidi.
 
Kwa kadiri ninavyofahamu, sarafu za zamani zinakusanywa na watu fulani wenye hobby hii. Kuna watu wanalipa hela nzuri tu kwa sarafu za zamani zinazoweza kutahiniwa uhalisi.

Na thamani inaongezeka kadiri sarafu zinavyokuwa za zamani, si ajabu ukipata sarafu za enzi ya utawala wa Ming utaweza kupata malaki kama si mamilioni ya dola. Haya hayaishii kwenye sarafu tu, watu wanauza mpaka vinyago vya kale, wanajeshi wa Kimarekani waliiba sana artifacts za Babeli kutoka makumbusho za Iraki.

Hizi habari nyingine zinazoelekea kwenye ushirikina ni tetesi zisizo na msingi.

Kwamba kila mjerumani ni mtaalamu wa kutengeneza utajiri kwa rupia inachekesha.
 
Kiranga,
Heshima mkuu,
Kwa maelezo yako hayo ina maana kwamba issue ni kuwa sarafu ya zamani lakini inasemekana wanunuzi wa rupia huwa wana vifaa maalumu vya kupimia na kama rupia husika ilishawahi kufanyiwa mambo wanakwambia kabisa kwamba hii imeshatumika!!
 
Heshima mkuu,
Kwa maelezo yako hayo ina maana kwamba issue ni kuwa sarafu ya zamani lakini inasemekana wanunuzi wa rupia huwa wana vifaa maalumu vya kupimia na kama rupia husika ilishawahi kufanyiwa mambo wanakwambia kabisa kwamba hii imeshatumika!!

Inawezekana kabisa kwamba vifaa hivyo vinapima authenticity na age ya rupia hizo, kama inaonekana feki au si ya zamani sana unaambiwa hii haina thamani.

Sasa wengine tuliozoea kuambiwa gari la msalaba mwekundu ni la nyonya damu tunaona kitu kinachokuwa lost in translation, kwamba zinatumiwa katika shughuli.

Hamna shughuli yoyote hapo.

Unaweza kuona hata online hizi habari kwenye sites kama hii hapa

http://www.zoomcoin.com/insiders-top-picks/?gclid=CNPgp6eX3J8CFQmdnAod4jZbGw
 
Wajinga ndio waliwao.

Man, one is able to use a computer to access JF but is still bound by baseless myths!!

Rupia ya kiJerumani haina chochote cha ajabu zaidi ya sarafu yeyote ya zamani, kama alivyokueleza Kiranga, ni kwamba tu hizi sarafu za zamani ni "collectors' items" kama zilivyo stempu nk
 
Inawezekana kabisa kwamba vifaa hivyo vinapima authenticity na age ya rupia hizo, kama inaonekana feki au si ya zamani sana unaambiwa hii haina thamani.

Sasa wengine tuliozoea kuambiwa gari la msalaba mwekundu ni la nyonya damu tunaona kitu kinachokuwa lost in translation, kwamba zinatumiwa katika shughuli.

Hamna shughuli yoyote hapo.

Unaweza kuona hata online hizi habari kwenye sites kama hii hapa

http://www.zoomcoin.com/insiders-top-picks/?gclid=CNPgp6eX3J8CFQmdnAod4jZbGw
Karinga,
Asante kwa maelezo mazuri, pia kati ya haya kuna mapokezi ya hadithi simulizi abazo huzuka na kupotea kati ya kizazi na kizazi. (the so called Legend) Hii hadithi ya Rupia ni moja wapo kuna wakati ilizushwa ya Noti ya sh 100 yenye picha ya Mmasai. Naamini ziko nyingi nyuingine.
 
Mie kwa uelewa wangu hadithi juu ya rupia zilikuwa zinahusishwa na utapeli,watu wanakuletea deal kuna rupia inatafutwa kwa thamani yoyote,halafu hao hao WANAKUZUNGUKA unakuletea rupia unainunua kwa hela nyingi,ukisha inunua tu mnunuzi anayeyuka!!!!,inakuwa imekula kwako.upo hapo?
 
Kwakweli ni utapeli mtupu kwani maelezo yake ni hayo hayo ila atawalokuwa nazo akuna aliyepata hizo pesa zaidi ya maneno na ushirikina mtupu.
 
Kwa kadiri ninavyofahamu, sarafu za zamani zinakusanywa na watu fulani wenye hobby hii.Kuna watu wanalipa hela nzuri tu kwa sarafu za zamani zinazoweza kutahiniwa uhalisi.
Na thamani inaongezeka kadiri sarafu zinavyokuwa za zamani, si ajabu ukipata sarafu za enzi ya utawala wa Ming utaweza kupata malaki kama si mamilioni ya dola.Haya hayaishii kwenye sarafu tu, watu wanauza mpaka vinyago vya kale, wanajeshi wa Kimarekani waliiba sana artifacts za Babeli kutoka makumbusho za Iraki.

Hizi habari nyingine zinazoelekea kwenye ushirikina ni tetesi zisizo na msingi.

Kwamba kila mjerumani ni mtaalamu wa kutengeneza utajiri kwa rupia inachekesha.

Kuna cousin yangu mmoja alianza kutafuta hizi hela akiwa kijana sasa hivi ana 65 hakuna cha sarafu wala nini - anasema anatafuta mizimu ya kufukua eti kuna mashimo waliacha wajerumani - na wameweka nguvu za kiza. anadai bila kujua unganga huwezi kuzichukua sarafu, dhahabu na vito vya thamani kwenye haya mashimo.

Waliacha ardhini wakati walivyoambiwa waondoke nchini sasa eti kuna wajukuu na watukuu wanachukua hizo ramani wanakuja africa kufuatilia hizo thamani, sasa yeye na wenzake wanatumia unganga kuzitafuta na kuzichukua.

i never believe this.....crup....
 
Kuna cousin yangu mmoja alianza kutafuta hizi hela akiwa kijana sasa hivi ana 65 hakuna cha sarafu wala nini - anasema anatafuta mizimu ya kufukua eti kuna mashimo waliacha wajerumani - na wameweka nguvu za kiza. anadai bila kujua unganga huwezi kuzichukua sarafu, dhahabu na vito vya thamani kwenye haya mashimo.

Waliacha ardhini wakati walivyoambiwa waondoke nchini sasa eti kuna wajukuu na watukuu wanachukua hizo ramani wanakuja africa kufuatilia hizo thamani

i never believe this.....crup....

Though I am highly doubtful, I will not be surprised at all if all of that is true, except for the mizimu part.
 
Though I am highly doubtful, I will not be surprised at all if all of that is true, except for the mizimu part.
Katika mazingira tulimo tunaamini uchawi upo, labda suala ambalo ni tata ni pale ambapo mtu ana kuambia kwamba ana uwezo wa kukufanya ukawa tajiri wakati yeye mwenyewe hali yake ki uchumi sio nzuri.

Ukiondoa utata huu, uchawi upo kwani tunaukuta hata kwenye maandiko mbali mbali ya zamani.
 
Katika mazingira tulimo tunaamini uchawi upo, labda suala ambalo ni tata ni pale ambapo mtu ana kuambia kwamba ana uwezo wa kukufanya ukawa tajiri wakati yeye mwenyewe hali yake ki uchumi sio nzuri. Ukiondoa utata huu, uchawi upo kwani tunaukuta hata kwenye maandiko mbali mbali ya zamani.

Ushawahi kuushuhudia uchawi wewe mwenyewe?
 
Kama ambavyo sijawahi kuuona umeme lakini naziona kazi zake, hata uchawi ni nguvu sio something touchable hivyo nasisitiza upo na unatenda!!

Sijasema "ushawahi kuuona uchawi" nimesema "ushawahi kuushuhudia uchawi", big difference.

Kwa hiyo swali linarudi pale pale, ushawahi kuona kazi za uchawi firsthand?

By the way, umeme unaonekana ukiwa na vifaa vya kuupima, uchawi unaupima kwa vifaa gani?

Wabongo kwa kuamini uchawi na ushirikina tu!
 
Sijasema "ushawahi kuuona uchawi" nimesema "ushawahi kuushuhudia uchawi", big difference.

Kwa hiyo swali linarudi pale pale, ushawahi kuona kazi za uchawi firsthand?

By the way, umeme unaonekana ukiwa na vifaa vya kuupima, uchawi unaupima kwa vifaa gani?

Wabongo kwa kuamini uchawi na ushirikina tu!
Kwangu mimi ushuhuda kwa mujibu wa ufahamu ni kitendo cha kutumia milango ya fahamu (macho,masikio,pua, kuhisi,kugusa, nk) kufanya utambuzi hivyo unaposema kama nilivyo wekea wino mwekundu hapo juu kwamba kuna tofauti kati ya kuona na kushuhudia kama utakuwa na hoja za msingi za kunishawishi kwamba you are right than me nitalazimika back to school (swhili language). Vinginevyo hizo ni hoja za nguvu na si nguvu za hoja!!

Kuhusu kwamba umeme una meter za kupimia je uchawi tunaupima na nini? Jibu ni kwamba hata huo umeme ni something professional sio kila mtu anauwezo wa kupima umeme pengine hata wewe mwenyewe hujui kupima umeme kama sio fani yako. Hivyo hata uchawi una vipimo vyake ndio maana akina prof. Maji Marefu walikuwa wana kamata wachawi.
 
Kwangu mimi ushuhuda kwa mujibu wa ufahamu ni kitendo cha kutumia milango ya fahamu (macho,masikio,pua, kuhisi,kugusa, nk) kufanya utambuzi hivyo unaposema kama nilivyo wekea wino mwekundu hapo juu kwamba kuna tofauti kati ya kuona na kushuhudia kama utakuwa na hoja za msingi za kunishawishi kwamba you are right than me nitalazimika back to school (swhili language). Vinginevyo hizo ni hoja za nguvu na si nguvu za hoja!!

Kwa kutumia approach yako ya milango ya fahamu, unatumia macho kuona, lakini unaweza kupata ushuhuda kwa mlango wowote wa fahamu. Ni vigumu kuiona sauti, lakini unaweza kutumia masikio yako kupata ushahidi kwamba redio ni nzima na inatangaza habari. Kwa hiyo mwenyewe umerahisisha kuonyesha tofauti ya kuona na kushuhudia.Nimekupa uwanja mpana zaidi ya kuona, labda uliweza kuunusa, kuusikia, kuugusa uchawi, uje utuambie hapa.

Kuhusu kwamba umeme una meter za kupimia je uchawi tunaupima na nini? Jibu ni kwamba hata huo umeme ni something professional sio kila mtu anauwezo wa kupima umeme pengine hata wewe mwenyewe hujui kupima umeme kama sio fani yako. Hivyo hata uchawi una vipimo vyake ndio maana akina prof. Maji Marefu walikuwa wana kamata wachawi.

Basically hapa unachosema kina justify mtu yeyote kusema chochote.Mimi naweza kusema kuna dudu lina miguu milioni mbili linakaa juu ya mlima Kilimanjaro, ila huwezi kuliona mpaka uwe na elimu maalum. Utakubali au kukataa? Kwa principle yako hiyo itabidi ukubali kwa sababu si nishasema ili kuliona inabidi uwe na elimu maalum? Utakubali au utakataa?

Huwezi ku prove kitu kwa kushhindwa kuonyesha kitu. Unaweza ku prove kitu kwa kuonyesha kitu.

Nionyeshe uchawi unaupimaje? Kama hujui uchawi unaupimaje then kubali kwamba unaongelea kitu usichokifahamu.
 
Achana na story za mitaani, ongeza bidii kutafuta fedha za halali na si za masharti usijeua wazazi wako bure!
 
Back
Top Bottom