Rungwe amuomba kikwete ampe hata viti maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rungwe amuomba kikwete ampe hata viti maalum

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by silver25, Nov 8, 2010.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jmaa alipo ona kuwa kakosa alicho kitaka, sasa aenda ikulu na kumuomba kikwe ampe hata vitimaalum bungeni akapige kelele huko,

  Kwakuwa kikwe alikuwa adui yake kipindi cha uchaguzi akaamuru walinzi wamtoe nje na wampe chai hukohuko nje anywe kisha atoweke kabisa...
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siasa haipaswi kuwa uadui. Source please.
   
 3. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hahahahahaahahhahah Alhakial wajinga ndio waliwaaaoooooo,,, aaammeeeeeee
   
 4. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I think JK got to think allowed. Haoni tafu lote alilopigiwa na hawa jamaa na wenzake waliokubali matokeo na ikawa ndo upenyo wa kuingia ikulu? Wameonesha moyo tangu mwanzo kwa kuharakisha kujitangaza kugombea jambo ambalo limechelewesha kuundwa kwa katiba mpya. hili nailiona kama pande kwa JK.
   
 5. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujue Rungwe bonge la mtu ukimuweka bungeni pale unatengeneza picha nzuuuriiiii, lakini JK halijui hilo
   
 6. Wateule

  Wateule JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 263
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  Naungana na mdau aliyeomba chanzo cha habari hii, kwani sidhani kama ina ukweli wowote. Ninavyomfahamu Rungwe, si mtu wa kujipendekeza kiasi hicho. Uchaguzi umekwisha na mshindi kwa njia ya uchakachuaji ameshapatikana, kwahiyo wanaoipenda nchi yao na kuitakia mema wamekubali matokeo. Rungwe kama alivyokuwa anasema kwenye kampeni zake, alikuwa "haombi kwenda Ikulu kutafuta Benz"......Yeye ni mtu ambaye ana biashara zake, ikiwemo kampuni ya sheria (RUNGWE & COMPANY ADVOCATE), ambayo kila leo ana saidia watanzania wanyonge kupata haki zao. Ataendelea kufanya hayo kwa kupitia Ikulu au nje ya Ikulu. Maisha yake yote amekuwa ni mjasiliamali na mtu ambaye ameendesha maisha yake na familia yake kwa mafanikio makubwa mpaka hapo alipofikia. Tatizo la wanasiasa wengi nchi kwetu, ni kwamba siasa ndio kazi,kwahiyo wakikosa nafasi kwenye serikali basi wamefilisika kimaisha. Hali hii ndio inapelekea wanasiasa wengi wa kiafrika wapiganie vyeo kwa kufa na kupona......hawajali hata kama tamaa yao hiyo itahatarisha amani ya nchi.
   
 7. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe wasema
   
 8. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #8
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hata Hivyo si katengeneza jina? kabla ya hapo nani alikuwa anamjua ukiacha ndugu na jamaa zake, wala hajatumia nguvu zake kukampaign zaidi ya ku pring picha zake chache
   
 9. Wateule

  Wateule JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 263
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 60
  Ndugu yangu Ghumpi , nafikiri ningekubaliana na wewe kama ungesema kuwa Rungwe amefahamika zaidi baada ya Uchaguzi. Kama wewe ulikuwa haumfahamu, haina maana kuwa alikuwa anafahamika kwa ndugu na jamaa zake tu. Kama nilivyosema awali, Rungwe amekuwa kwenye shughuli za ujasiliamali na za jamii kwa muda mrefu na mimi nimemfahamu kwa shughuli zake hizo.
  Nafikiri vyama vya upinzani, ambavyo vilikuwa havina wabunge (ikiwemo NCCR) vilijitahidi kufanya kampeni kadri ya uwezo wao. Wengi wa wagombea wa vyama hivi waliingia gharama binafsi, ili kuwafikia wananchi. Sasa katika mazingira kama hayo huwezi kuwafananisha na CCM ambao wanashikilia dola na tumeshuhudia jinsi mali za serikali zilivyokuwa zina changanywa na chama. Je Ghumpi, ulitegemea Rungwe afanye kampeni kama walizofanya CCM?? Unaposema Rungwe hakutumia nguvu na alichapisha picha chache ili kutengeneza jina una maanisha nini?, mbona CCM na mgombea wao "maarufu" walikuwa na mabango ya picha kama za COCA COLA nchi nzima? Na wao walikuwa wana mtengenezea jina mgombea wao?
  Asanteni.
   
Loading...