Rungu laja kufungiwa line zilizosajiliwa kiujanja na mawakala

Dhana ya fingerprint hapa mbona siioni! Mi nimeshasajili line yangu kwa NIN na fingerprint, mwingine anaisajiliaj? Yaan NIN inawez kukubali fingerprint Zaid ya moja?

Kama ni kweli, hili zoezi linaweza lisiwe na uwezo wa kukidhi matarajio ya matamanio yetu!

Au mimi ndo sielewi vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wadau wa JF,

Kuna mdau wa TCRA kanitonya kwamba wametoa order kwa makapuni ya simu kuwawezesha wateja kujua kama NIDA ID yake imetumika kwa zaidi ya namba moja au lah.

Ili kujua unabonyeza *106# kisha usajili wa NIDA (Utaingiza NIDA ID yako), baada ya hapo zitakuja namba zote zilizosajiliwa kwa ID yako ya NIDA. Kama namba haijui siyo yako maana yake wakala (agent) alifanya ujanja kutumia ID yako kusajili line nyingine.

Ukishaona kwenye list namba haijui basi unaenda kwenye shop iliyokaribu nawe unaclaim then Customer care anakuambia uweke finger print kisha hiyo namba inafutwa.

Kutokana na watu wengi kutokuwa na Nida mawakala wengi wanatumia ujanjaujanja wa kusajili line kwa kutumia ID ya mtu mwingine na kuuza hizo line kati ya elfu 5 hadi elfu 20 inategemea watakavyokuona na uhitaji wako.

Mawakala wanafanyaje ujanja? Ukienda kusajili line yako atakwambia uingize kidole baada ya dakika atakwambia network inasumbua hebu ingiza tena basi hapo jua umeumia, ile ya kwanza amesajili line ya mtu mwingine na ya pili anasajili yako, kama haujui hiyo mbinu hauwezi kumstukia maana wapo very smart.

Kwahiyo wote mlionunua line kwa mawakala zilizosajiliwa kwa NIDA mjiandae kisaikolojia.

Kosa lingine ni nida wenyewe, mfano mdogo wangu amejiandikisha since mwezi wa kumi but mpaka leo ajapata namba je nafanya nn? Ameenda nida anaambiwa subiri sasa hapo ndio chanzo cha kutafuta another alternative ili Uwe hewan
 
Kosa lingine ni nida wenyewe, mfano mdogo wangu amejiandikisha since mwezi wa kumi but mpaka leo ajapata namba je nafanya nn? Ameenda nida anaambiwa subiri sasa hapo ndio chanzo cha kutafuta another alternative ili Uwe hewan
Hizo hoja zako utaenda kusema ukipelekwa "UBAONI KWA PONSIO PILATO" aka MAHAKAMANI.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom