Rungu la Dk. Mwakyembe latua kwa meneja TAZARA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rungu la Dk. Mwakyembe latua kwa meneja TAZARA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 12, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sunday, 12 August 2012 | Mwananchi | Mwandishi: Fidelis Butahe

  WAZIRI wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema atamtimua kazi Meneja Mkuu wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (Tazara), Abdallah Shekimweri, iwapo atashindwa kusimamia majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuwapa vitendea kazi na posho wafanyakazi wa shirika hilo.


  Rungu la waziri huyo lilianza Juni 5, mwaka huu baada ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo.

  Mbali na uteuzi huo pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo ambapo baada ya siku chache alianika ufisadi unaodaiwa kufanywa na kigogo huyo.

  Lakini jana wakati akiwa katika ziara yake ya kushtukiza katika karakana za Tazara, Dk Mwakyembe alisema kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa Shekimweri.

  Mbali na kutembelea Tazara, pia alifanya ziara bandarini na katika ofisi za Kampuni ya Reli Tanzania (TRL).

  Akiwa katika ziara hiyo aliahidi kukutana na uongozi mzima wa Tazara ili kujadili matatizo yaliyopo katika shirika hilo ikiwa ni pamoja na ubovu wa reli, lengo likiwa ni kuyapatia ufumbuzi.

  Mmoja wa wasaidizi wake ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini licha ya kuwa alikuwa amembatana na waziri huyo katika ziara hiyo alisema kuwa suala la kumtimua kazi Shekimweri siyo jambo la utani.

  "Dk Mwakyembe ameshatuma barua kwa uongozi wa Tazara nchini Zambia, amewaeleza wazi kuwa haridhishwi na utendaji kazi wa (Shekimweri) na yupo tayari kutoa uamuzi, itakuwa kabla ya Oktoba mwaka huu," alisema msaidizi huyo na kuongeza;

  "Si unajua hili shirika linaendeshwa kwa ubia wa Tanzania na Zambia, hivyo kama unataka kuchukua uamuzi ni lazima upande mwingine uwe na taarifa."

  Dk Mwakyembe alisema haridhishwi na ufanyaji kazi unavyoendelea katika Karakana ya Tazara na kumtaka Shekimweri kuwapa vifaa wafanyakazi hao na iwapo atashindwa kufanya hivyo atalazimika kumfukuza kazi.  "Tutafukuzana hapa, watu wapo tayari kufanya kazi ila wanakwamishwa, mwambieni Shekimweri kuwa nitamfukuza kazi na nitarudi tena Jumatatu (kesho)," alisema Dk Mwakyembe.

  

Alisema kuwa ni jambo la ajabu kwa menejimenti ya Tazara kushindwa kutoa fedha kwa watumishi wake wakati Serikali imeshatoa fedha za ukarabati wa mabehewa ya treni yanayotakiwa kuanza kutoa huduma ya usafiri kuanzia Oktoba mwaka huu.
  


  Dk Mwakyembe alihoji sababu ya menejimenti hiyo kukalia fedha hizo wakati zinapaswa kulipwa kwa wafanyakazi hao wanaoendelea kukimbizana na muda ili kumaliza ukarabati huo.  "Fedha mnaziweka makao makuu kwani ni maua hayo? Walipeni watu fedha zao na mnunue vifaa, tutafukuzana hapa na hakuna wa kunilaumu," alisema Dk Mwakyembe.

  Aliitaka menejimenti ya Tazara kukamilisha ukarabati wa mabehewa 14 ambayo aliagiza yafanyiwe ukarabati kwa kuwa mpaka sasa ni mabehewa manne tu ndiyo yanayoonekana kukarabatiwa.

  Baadhi ya wafanyakazi waliokuwapo katika maeneo yao ya kazi walimweleza, Dk Mwakyembe kwamba shirika hilo haliwawekei fedha zao za mifuko ya hifadhi ya jamii, suala ambalo waziri huyo aliahidi kulifuatilia kwa ukaribu.

  Akiwa katika Karakana ya TRL, Dk Mwakyembe aliridhishwa na utendaji kazi na kusema kuwa mpaka Oktoba mwaka huu treni ya Reli ya Kati itaanza kutoa huduma zake kama ilivyotangazwa.

  Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe alisema mashine ya kushusha na kupakia mizigo katika meli karibu itafungwa kwa kuwa ujenzi wa reli kwa ajili ya kusimamisha mashine hiyo unaendelea vizuri


  MWAKYEMBE FANYA KAZI KWA MOYO WOTE TUNAKUTEGEMEA NA MUNGU ATAKULIPA KW KAZI NJEMA,, STAY BLESSED
   
 2. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru kwa taarifa hiyo mkuu, kinacho shangaza ni kwa nini fedha zinazo tolewa na G.O.T kwa ajili ya kufanya ukarabati wa mabehewa ambayo yatatumika kwenye Region ya TANZANIA fedha hizo zinapelekwa makao makuu kwa madhumuni GANI?

  Mbona Region office kuna wahasibu na Revenue office, si hilo hata utehuzi wa Regional Manager unatokana na pendekezo la Wizara, sasa RGM anapashwa kuheshimu nani zaidi Serikali ya TAIFA lake au MD/DMD wa Head office? Kwa nini kama RGM aliona kuna utata kutoka kwa mtu aliye pewa dhamana ya kutoa kibali cha matumizi ya fedha zilizo tolewa na G.O.T kunawekewa mikwara, yeye kama meja wa mkoa alipashwa kulivalia njuga suala ili na kiripoti mara moja wizarani; yeye kam Engineer alikuwa anaelewa fika timeline ya kukamilisha zoezi zima la kukarabati mabehewa -sasa tatizo liko wapi!!

  Kusema ukweli fedha za kukarabati mabehewa alipashwa kukabidhiwa Regional Manager na siyo watu wa Head Office, kama walifanya kosa hilo siajabu ukakuta fedha hizo zimetumika kufanya mambo mengine kabisa ambayo hayana uhusiano wowote na ukarabati wa mabehewa, nashauri achukuliwa external Auditor akaguwe pesa hizo zinatumika namna gani unaweza kukuta zimekwenda kununulia Diesel na Lubricants na mambo mengine ya kijinga, hawaogopi lolote, CHUNGA SANA.

  Be blessed Dr. Mwakyembe.
   
 3. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Jambo la muhimu kuhusu mustakbari wa Tazara ni kupitiwa upya mkataba wa uanzishwaji wa mamlaka hiyo baina ya nchi mbili husika.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Sehemu kubwa ya Reli iko Tanzania nashangaa maamuzi mengi lazima yatoke Zambia hata MD lazima atoke Zambia kwa miaka mingi pia pesa zoote account kubwa iko Zambia!sijui mkataba ukoje na kwa nini
   
 5. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa Tazara hususani wa Head Office ni mchwa kwenye shirika.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hivi wachina walijenga kwa ajili ya wabongo nashangaa hawa wa zambia wametekaje nyara reli yetu
   
 7. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kazi ipo
   
 8. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii reli sanasana ilijengwa kwa ajili ya wa Zambia kutokana na Makaburu kuzuia mizigo yao kupita bandari ya Durban...:hat:
   
 9. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu yaani sijuhi kwa nini Serikali yetu huwa aijuhi kwamba Wazambia hawako commited na reli hii zaidi ya ulaji tu wakishilikiana na baadhi ya Watanzania ambao ni wasaliti wa Taifa lao. Wazambia wana mikakati ya kushirikiana na Msumbiji ili watumie port ya Nakala vile vile kutumia port ya Durban South Africa, hili alina siri tena wenzetu awalipi umuhimu wowote suala la uhendeshaji reli ya TAZARA kiufanisi.

  Serikali yetu inapashwa kuimarisha reli upande wa Tanzania ili watumie TAZARA corridor kikamilifu kwa ajili ya Mechanised Agriculture, usafirishaji wa mkaa wa mawe kutoka Mchuchuma kwenda nchi za nje, Iron ore, Mbao, Cement, Uranium, vile vile tunaweza ku-extend reli kwenda Malawi kupitia Mbeya, reli hii ina potential sana upande wa TANZANIA actually as time goesby tutafikia wakati Tanzania itakuwa inajitosheleza kimapato bila ya kutegemea revenue zinazo kuwa generated kutokana kwa kusafirisha shaba kutoka ZAMBIA.
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkataba ndio tatizo kwa kifupi waangalie jinsi ya kurekebisha mkataba kwanza
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, hili ni kingine kati ya madudu yaliyoacha na yule fulani. Kikwete na timu yake lazima wayaweke sawa.
   
 12. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu Wazambia wasingeweza kuteka nyara uendeshaji wa TAZARA bila ya ridhaa ya Watanzania - sisi kukosa umoja na kupikiana majungu/fitina ndio kumewafanya Wazambia wa-exploit weakness zetu to maximum. Yaani ukuitisha mkutano wa ghafla pale TAZARA utakuta Wazambia wanazungumza kauri moja i.e wako highly organised, wanafanikiwa kivipi kuwapiku Watanzanai? mafanikio yao yanatokana na kukutana kila wakati (wiki) na kupanga mikakati- lakini ukija kwa Watanzania utakuta kila mmoja anakurupuka kutoka ofisini/nyumbani kuja mkutanoni bila ya kupanga mkakati wowote wa pamoja, kila mtu anazungumza la kwake hakuna umoja hata kidogo.

  Sad story hii haiko-confined kwa wafanyakazi na viongozi upande wa Tanzania hata Board Members upande wa Tanzanai nao wana weakness hiyo; ndio maana ilikuwa raisi ku-reverse mahamuzi yaliyo tolewa na Mh.Nundu kuhusu kusimamisha kazi baadhi ya viongozi TAZARA, Board ilipokaa baada ya Mh Mwakyembe kuteuliwa katika wadhifa wake mpya Board members wa kutoka Zambia walisha jipanga kupinga uhamuzi wa Mh. Nundu bila ya kujali ushahidi unaonyesha kwamba watuhumiwa wanahusika na tuhumu zilizo tolewa na wafanya kazi dhidi yao, sina hakika kama Board Members upande wa Tanzania walitegemea suprise hiyo! Jamaa hawa walisha tusoma na kujuwa jinsi ya kutupiku.

  Ni kweli Wachina walijenga reli hii kwa ajili ya faida ya nchi zetu mbili, lakini madhumuni makubwa yalikuwa kusaidia Zambia ipate an alternative route ya kusafirisha shaba na madini kwenda nje, chakula na mbolea kwenda nchini mwao kutoka nje.
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu, JK alisema wazi wazi alipo tembelea Wizara ya Uchukuzi kwamba tatizo kubwa linalo ikabili reli ya TAZARA ni UONGOZI mbovu, sasa kama JK aliwahi kusema hivyo kwa nini watu wanataka kumfunga mikono Mh.Mwakyembe ili ashindwe ku-address tatizo hili once and forall!!!
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kuna wengi hawapendi kuona mafanikio ya Serikali ya Kikwete, kwa chuki binafsi tu si zaidi.
   
 15. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280

  Kweli mkuu, suala hili huwa linanisikitisha kweli kweli, niliwahi kuweka humu in chronological order (tangu tupate uhuru) vipindi vya awamu zote, tofauti za Viongozi walio mtangulia JK, mambo waliyo wahi kufanya/maendeleo, mapungufu yao nk. Nilipo uliza kwa nini watu wanataka JK akabiliane na madudu yaliyo kuwa accumulated over the period of (40+) years na Viongozi walio mtangulia, hivi tutakuwa tunamtendea haki JK kutegemea kwamba somehow angafanye miujiza ya kusafisha vices zote nchini ndani ya miaka mitano ya uongozi wake!!! Katika suala hilo hakuna aliye nipa jibu la kuridhisha - mema aliyo fanyia TAIFA letu yanakuwa consumed in a conflagration of hatred, mtu unajiuliza hivi hii blanket condemnation inasababishwa na kitu gani hasa?

  Ukihoji sababu za misingi za kumlahumu JK takribani kwa kila kitu, majibu utakayo jibiwa unapata majibu ya kejeri tu! Mara wewe mtu wa usalama wa taifa, mara umetumwa humu tumekwisha kushtukia, mara unataka kujipendekeza, mara mambo unayo zumgumzia tulikuwa hatujazaliwa! Ukisema kwa nini hamsomi vitabu vya historia au kuhoji watu walio wazidi umri ili wapate picha kamili kuhusu mambo yaliyo jiri katika awamu zilizo mtangulia JK, ukitoa hoja kama hiyo hakuna anaye toa jibu la kuridhisha!

  Hivi tukiwa wakweli bila ya kusukumwa na itikadi za vyama au bifu binafsi, tukianza kuorodhesha miradi, misaada, mikopo yenye riba nafuu ambayo JK amefanikiwa kuileta katika Taifa letu ndani ya miaka mitano, tuki-badilisha yote hayo in monetary TERMS total sum ni colossal; thanks to his negotiating skills and unassuming persona.

  Mimi huwa nafatilia kwa karibu sana kauri zake anapokuwa nchi za nje, ni mara chache kumsikia anazungumzia mambo ya politics anafanya hivyo inapokuwa absolutely necessary lakini lion's share ya muda wake unamkuta anazungumza na wataalamu wa nyanja za IT, Uganga(medicine), Viwanda, Telecommunication, Agriculture (commercial), Utafiti wa vinasaba vya mbegu, Uhanzishwaji vya vyo vya HiTech nchini, Hospitali zenye hadhi ya dunia ya kwanza na kuwasomesha Madkitari bingwa kwa gharama kubwa nk. In general anapenda sana mambo ya sayansi na tekinolojia na yuko well informed katika nyanja hizo, si hilo tu vile vile yuko mstari wa mbele katika azma yake ya kutaka Taifa letu lipige hatua katika Nyanja hii ya sayansi na tekinolojia, sijuhi kwa nini alisomea uchumi badala ya sayansi? usije ukajidanga mambo ya ufundi hayampigi chenga hata kidogo, mifano tunayo - msikilize anapo uliza maswali yanayo husu nyanja hizo.

  Juzi juzi niliomuona kwenye TV mwanae (Ridhiwani) akizungumzia kwa weledi mkubwa mambo ya LTE, WiMax, GSM, CDMA mambo ya IT(hacking)na jinsi ya kukabiliana nayo! Maelezo yake yalinifanya nishikwe butwaa! Walipo niambia ni mwana sheria nilishangaa sana.
   
Loading...