Rungu kwa Wakurugenzi au Madiwani....?

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,420
2,271
"Halmashauri nyingi nchini kupitia kwa wakurugenzi wake zimekuwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa kipindi kirefu, sasa utaratibu unaandaliwa wa kuwabana viongozi hawa," alisema Pinda.
Halmashauri zote zinaundwa na Waheshimiwa Madiwani na Watendaji. Mkuu wa Madiwani katika halmashauri hizo huwa ni Meya au Mwenyekiti, wakati watendaji wanawajibika kwa Mkurugenzi. Katika vikao vya Madiwani Mkurugenzi huwa ni katibu.

Linapokuja suala la matumizi ya fedha za Halmashauri, Mkurugenzi anawajibika kutumia fedha hizo kwa mujibu wa maelekezo na matakwa ya madiwani.

Kauli ya Waziri Mkuu mpya kuwa anaandaa RUNGU kwa wakurugenzi wa halmashauri kutokana na matumizi mabaya ya fedha linanitia shaka kama rungu hilo litakuwa limempata mrengwa halisi.

Source:Tanzania Daima
 
Kibunango,

Nakubaliana na wewe juu ya hili. Inatakiwa sheria zinazoongoza serikali za mitaa zifanyiwe marekebisho makubwa sana. Tatizo namba moja ni capacity ndogo madiwani hasa kwa wilaya za vijijini. Pili, wakururugenzi, mkuu wa wilaya na mbunge wana mamlaka kidogo sana kwenye utendahi wa hizo halmashauri.

Matokeo yake ni utendaji mbovu na upotefu wa mabilioni ya pesa. Tunawapa mabilioni ya pesa watu ambao hawawezi hata kusimamia project ya milioni moja.

Kunahitajika mafunzo makubwa sana kwenye utendaji wa serikali za mitaa, vinginevyo huko nako tutaendelea kupoteza mabilioni ya pesa.

Pia hakuna ubunifu kabisa wa miradi endelevu, wanakuja na projects za ajabu ajabu ambazo haziongezi value yoyote kwenye jamii.

Japo lengo la kuwa na serikali za mitaa ni zuri sana lakini bila kuwa na watendaji wa maana, hakuna mafanikio yatakayopatikana.
 
Hoja ni nzuri lakini kimawazo yangu nakumbuka kuna thread tulishaliongelea hili jambo. Mimi kwa hili kikubwa kinachonisumbua ni hiki:
1. Majukumu ya Mkuu wa Wilaya (DC) kufananisha na yale ya Mkurugenzi wa Meandeleo wa Wilaya (DED). Hili usiache kuangalia pia majukumu ya Mbunge (MP)??

2. Majukumu ya Watendaji Kata, Viongozi wa Serikali za Mitaa/Vijiji, Wajumbe wa Nyumba Kumikumi (wapo hawa bado ee??) na kufananisha na yale ya maDiwani.

My take ni kwamba pamoja na kwamba tupo kwenye multiparty system bado kuna hivi vyeo ambavyo vingi ni vyenye "Political orientation" at the cost ya wananchi!! Hawa wote wakikaa kwenye vikao ni pesa (kupanga/allowances/usafiri nk). Sasa ka nchi kenyewe ni kama haka ka kwetu halafu kila kona ukikatiza kama sio STJ la DED au DC (na kamkopo T 000 XYS 000 la Mbunge) then unakutana na DIwani na wengine. Haya yote ni magharama makubwa kwa serikali. Kwanini tusipunguze hawa waheshimiwa jamani. Itasaidia kupunguza operating cost za serikali (nani kasema chama ndo kinacho kidhi gharama za viongozi - hata yule mpiga debe ni pesa ya kodi kijijini au mtaani, usiniulize wanapataje lakini am sure wanakula). Wapunguzwe hawa watu ni limzigo tu kwetu!!!

Sasa hivi kila mtu anasema tupunguze ukubwa wa Baraza la Mawaziri lakini kule kwenye grassroot tunaacha majitu yanakaa hayana cha kufanya zaidi ya kuishia kugombana kutokana na "Overlap of responsibilities"

Mungu Ibairiki Tanzania na watu wake.......
 
Lakini, huyu Bwana Pinda ndiye alikuwa waziri wa local governments. Sasa alikuwa wapi kuwapiga hilo Rungu au anataka kusema waziri wa local governments hana uwezo huo ila ni waziri mkuu??? Mungu tuepushe asije akawa msanii mwingine!!!!
 
Mimim sielewi ni kwanini Bwana Pinda hakuweza kufanya haya anayosema sasa. Kwani Mkaguzi wa mahesabu ya serikali mwaka jana litoa taarifa amabayo ilionyesha ubadhirifu mkubwa sana katika Halmashauri za wilaya. Halmshauri nyingi zilipata wanavyoita vyeti vichafu, hatukusikia hatua. Na mimi naamini kama nagefanya kazi yake ipasavyao na kama anavysemwa na wengi basi wizara aliyopkuwa aniongiza ingeweza kuleta mabadiliko makubwa mabyo kila mtanzania angeyahisi.
 
Kibunango,

Nakubaliana na wewe juu ya hili. Inatakiwa sheria zinazoongoza serikali za mitaa zifanyiwe marekebisho makubwa sana. Tatizo namba moja ni capacity ndogo madiwani hasa kwa wilaya za vijijini. Pili, wakururugenzi, mkuu wa wilaya na mbunge wana mamlaka kidogo sana kwenye utendahi wa hizo halmashauri.

Matokeo yake ni utendaji mbovu na upotefu wa mabilioni ya pesa. Tunawapa mabilioni ya pesa watu ambao hawawezi hata kusimamia project ya milioni moja.

Kunahitajika mafunzo makubwa sana kwenye utendaji wa serikali za mitaa, vinginevyo huko nako tutaendelea kupoteza mabilioni ya pesa.

Pia hakuna ubunifu kabisa wa miradi endelevu, wanakuja na projects za ajabu ajabu ambazo haziongezi value yoyote kwenye jamii.

Japo lengo la kuwa na serikali za mitaa ni zuri sana lakini bila kuwa na watendaji wa maana, hakuna mafanikio yatakayopatikana.

Mtanzania:
Nakubaliana na wewe kuhusu uwezo mdogo wa madiwani, hasa kielimu kiasi kwamba hushindwa kupang ni nini kinahatajika katika kuendeleza wadi zao.

Aidha napenda ujue vita vikubwa kati ya madiwani na wabunge. Diwani katika wadi hujiona ndie kiongozi mkubwa na ndie mwenye mamlaka yote ya maendeleo katika wadi yake. Hivyo mara nyingi huwa tofauti na Mbunge wake ambae huwa anasimamia zaidi ya wadi moja. Diwani anawajibika moja kwa moja katika halmashauri yake, wakati Mbunge anawajibika katika serikali kuu. Hii usababisha migongano ya utendaji kila siku. Na mbaya zaidi iwapo Diwani ana ndoto ya kuja kuwa mbunge siku moja.

Mkuu wa wilaya kwa upande mwingine ndie kinara katika wilaya yake, hivyo hupenda kuona Mkurugenzi wa halmashauri akifuata maelekezo yake. Mkurugenzi huyohuyo anawajibika kwa madiwani, na huku akipata misukosuko toka kwa mbunge. Hapa kuna conflict kubwa ya utendaji.

Viwango vya elimu ndogo, uchumi na rushwa vimetalawa sana katika halmashauri za wilaya. Ukija mikoani, Manispaa au Jiji au halmashauri za mikoa, nazo zina tatizo lile lile, Ubabe wa mkuu wa mkoa na wabunge na zaidi hao madiwani.

Kuna wakati sheria za uchaguzi zilitaka wadiwani wawe na kazi ambazo zinawapatia vipato vya kila siku, ili kupunguza kutegemea posho ya vikao. Hata hivyo hii haikuweza kufanikiwa. Zaidi Madiwani walitaka posho za vikao vyao zilipwe kama misharaha. Yaani sio kila baada ya kwisha kwa vikao, bali zikusanywe na kulipwa mwisho wa mwezi. Hii imesababisha madiwani wengi kama sio wote kushinda kutwa nzima katika ofisi za halmashauri, ambapo utafikili kuwa ni watendaji, badala ya kuwepo kwenye wadi zao.

Halmashauri nyingi zina watendaji wazuri, ila wamebwana na madiwani, ambao hawajui mipaka yao ya kazi. Madiwani kwa ufupi ndio watengenezaji wakubwa wa majungu katika halmashauri zao, ndio mafisadi wa ngazi ya mwanzo kabisa katika mfumo mzima wa tawala za mikoa.

Waziri Mkuu anajua hilo, kwa kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika serikali za mitaa. Ananishangaza na kauli yake hiyo ilhali anajua uwezo wa mkurugenzi na watendaji wa halmashauri unafikiwa wapi. Ni wizara yenyewe ya tawala za mikoa chini ya waziri wa tawala za mikoa ambao wameshindwa kuja na mbinu, sera au kanuni bora za kuwezesha kutokuwepo na matumizi mabovu katika halmashauri.
 
Zitangazwe zabuni za kazi huko vijijini ili wasomi wasing'ang'anie mijini tu ,CV zinazohusiana au wagombea wa udiwani wawe na elimu ya kiwango fulani na iwachwe ile tabia ya kukurupuka kila mtu anagombea udiwani,maana hizi nafasi zingekuwa zinagombewa na watu wenye CV nzuri basi hata utendaji wa halmashauri na sehemu nyengine zingekuwa na watendaji wazuri na fisadi ingelikuwa rahisi kumkamata.Lakini leo ukijuwa kusifu chama kijijini baaasi hakuna mwengine unaefaa ila wewe ,yaani itafikia wakati Nchi itaongozwa na wapiga debe akina Tambwe Hiza na tumeshafikia maana viggogo wote ni wafanyi biashara mpaka wauza unga nao ni viongozi.
 
Kibunango,

Nakubaliana na wewe juu ya hili. Inatakiwa sheria zinazoongoza serikali za mitaa zifanyiwe marekebisho makubwa sana. Tatizo namba moja ni capacity ndogo madiwani hasa kwa wilaya za vijijini. Pili, wakururugenzi, mkuu wa wilaya na mbunge wana mamlaka kidogo sana kwenye utendahi wa hizo halmashauri.

Matokeo yake ni utendaji mbovu na upotefu wa mabilioni ya pesa. Tunawapa mabilioni ya pesa watu ambao hawawezi hata kusimamia project ya milioni moja.

Kunahitajika mafunzo makubwa sana kwenye utendaji wa serikali za mitaa, vinginevyo huko nako tutaendelea kupoteza mabilioni ya pesa.

Pia hakuna ubunifu kabisa wa miradi endelevu, wanakuja na projects za ajabu ajabu ambazo haziongezi value yoyote kwenye jamii.

Japo lengo la kuwa na serikali za mitaa ni zuri sana lakini bila kuwa na watendaji wa maana, hakuna mafanikio yatakayopatikana.

Ndugu Waziri Mkuu Pinda labda anataka sasa kupeleka ama upelekwe muswada na iwe sheria ya kubadili mambo na ikawa ndiyo tafsiri yake ya kuandaa rungu .
 
ccm ndio kila kitu hapa
Ile Halmashauri ya Jiji la MZA, AR na zile zingine kuleTarime na Kigoma ni vipi? Naona Meya wa Jiji la Mwanza ameanza kulia lia... Huku madiwani wa Halmashauri ya mji wa Arusha wakiwapa kisogo viongozi wao!
 
Back
Top Bottom