Kibunango
JF-Expert Member
- Aug 29, 2006
- 8,364
- 2,167
Halmashauri zote zinaundwa na Waheshimiwa Madiwani na Watendaji. Mkuu wa Madiwani katika halmashauri hizo huwa ni Meya au Mwenyekiti, wakati watendaji wanawajibika kwa Mkurugenzi. Katika vikao vya Madiwani Mkurugenzi huwa ni katibu."Halmashauri nyingi nchini kupitia kwa wakurugenzi wake zimekuwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali kwa kipindi kirefu, sasa utaratibu unaandaliwa wa kuwabana viongozi hawa," alisema Pinda.
Linapokuja suala la matumizi ya fedha za Halmashauri, Mkurugenzi anawajibika kutumia fedha hizo kwa mujibu wa maelekezo na matakwa ya madiwani.
Kauli ya Waziri Mkuu mpya kuwa anaandaa RUNGU kwa wakurugenzi wa halmashauri kutokana na matumizi mabaya ya fedha linanitia shaka kama rungu hilo litakuwa limempata mrengwa halisi.
Source:Tanzania Daima