Rukwa waazimia kuanzisha mkoa mpya wa Mpanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rukwa waazimia kuanzisha mkoa mpya wa Mpanda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Mar 13, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  WAJUMBE wa baraza la ushauri la mkoa wa Rukwa (RCC) wamepitisha rasmu ya pendekezo la kuugawa mkoa huo katika mikoa miwili na kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Mpanda kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.


  Katibu Tawala wa mkoa huo, Innocent Mwenda aliwaeleza wajumbe hao kuwa kazi hiyo ya ugawaji wa mkoa wa Rukwa itazingatia vigezo muhimu vikiwemo vya ukubwa wa eneo, idadi ya watu pamoja na shughuli za kiuchumi.


  Pendekezo hilo limekuja wakati tayari kuna pendekezo la kuigawa wilaya ya Mpanda na kuanzisha wilaya mpya ya Katavi na kuigawa wilaya ya Sumbawanga na kuanzishwa kwa wilaya ya Kalambo iliyopitishwa na kikao cha RCC mwaka 2006.
  Source:Mwananchi.


  Wanajamvi naomba msaada huu mtindo wa kuanzisha mkoa kwa kisingizio cha kusogeza huduma karibu na wananchi mbona umekaa kifisadi !.Hivi kweli Tanzania inahitaji kuongeza idadi ya mikoa ili kufikisha huduma karibu na wananchi.  Kwa upande wao, wajumbe wa mkutano huo walitahadharisha kuwa, mgawanyo wa mkoa huo uwashirikishe wananchi na uzingatie zaidi maslahi ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi na siyo ya kisiasa.


  Hata hivyo makao makuu ya mkoa huo mpya wa Mpanda yanatarajia kuwa mjini Mpanda huku ukiwa na ukubwa wa eneo la kilometa za mraba zaidi ya 47,000 na watu zaidi ya 500,000.


  Utaratibu wa kuomba kuanzisha mikoa au wilaya huanzia kwenye wilaya inayohusika na kupitia kwenye mkoa unaohusika na kisha e mapendekezo kuwasilishwa serikalini.


  Mkoa wa Rukwa haukuwepo wakati wa Uhuru, eneo hilo la mkoa wa Rukwa lote lilikuwa chini ya mkoa wa Mbeya na Tabora.


  Wakati huo wilaya ya Mpanda ilikuwa chini ya mkoa wa Tabora na wilaya ya Sumbawanga na Nkasi zilikuwa chini ya mkoa wa Mbeya.


  Hali hii ilisababisha wananchi wa maeneo ya Mpanda, Nkasi na Sumbawanga kuwa mbali sana na serikali yao ya mkoa na Taifa.


  Hivyo ili serikali iweze kuwa karibu na wananchi, Januari 29, 1974 Mkoa wa Rukwa ulianzishwa ukiwa na Wilaya 2 Mpanda na Sumbawanga. Mnamo mwaka 1975 wilaya ya Nkasi iliundwa na kufanya Mkoa kuwa na wilaya tatu, na Halmahauri ya Mji.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kabla sijachangia hoja hii naomba niseme kuwa mipango mingi ya bongo inakwenda kisiasa zaidi kuliko utalaam.Mifano hai ni hii hapa,moja wakati wa Sumaye tulitaka kujenga International airport Arusha wakati KIA ipo km 60.Kutoka makao makuu ya wilaya ya Makete mpaka Iringa ni km 310 lakini ni km 96 mpaka mbeya mjini. Angalia wilaya ya Simanjiro ilivyo,kuna watu wanapotaka huduma (vibali,mahakama,hospitali) ktk ngazi ya wilaya/mkoa inakuwa ni safari ya gharama na ya muda mwingi bila sababu,mfano Mkisi wa Ludewa ziwa nyasa,wapi karibu,Iringa au Songea.Mkisi huyu anatoka ziwani anakuja na kulala Songea mjini akiwa safarini kwenda Iringa kuomba kibali(mhuri) ili afanye kazi zake wakati wakuu walewale anaowafuata Iringa anawaacha pale Songea.

  Mimi ninawaunga mkono kama mkoa huo utamsaidia mkulima wa kule Kasanga kupunguza muda wa kufuata huduma Sumbawanga na badala yake akatumia mda huo kuzalisha. Vigezo vingine tuwaachie watalaam.

  Nimetumia mfano wa Iringa kwa sababu kwa sehemu ninaufahamu mkoa huo.
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Sababu za kuanzisha mkoa wa Manyara zilikuwa za kisiasa zaidi kuliko kumsaidia mwananchi wa kawaida.Wakaazi wa Mererani iliyoka mkoa wa Manyara wakitaka kwenda makao makuu ya mkoa wanalazimika kupitia kwanza mkoa wa Arusha.

  Waziri mkuu mstaafu F Sumaye alitumia wadhifa wake kufanikisha mpango wa kuugawanya mkoa wa Arusha na Manyara.Waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda naye kaamua kufuata mkumbo huo huo.
   
 4. K

  Kwaminchi Senior Member

  #4
  Mar 13, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Tanganyika ilikuwa na majimbo/mikoa minane tu kabla hatujapata uhuru. Provincial Commissioners ambao hii leo tunawajua kama Regional Commissioners walikuwa wanane tu. Gharama zao, mishahara, majumba na allowances zilikuwa ni kidogo sana ukilinganisha na ilivyo hivi sasa.

  Hiki kisingizio cha kumletea mwananchi huduma na maendeleo naona hakishiki maji. Kwa nini hizo huduma na hayo maendeleleo hayasogezwi wilayani na kwenye kata? Kwa nini huduma na maendeleo yawe kwenye mikoa pekee?

  Nakubaliana na wote wanaosema kuwa hii ni janja ya kisiasa, kuwaongezea wananchi gharama za vigogo vya mikoa na wilaya. Ma-RC na Ma-DC wanazidi kuongezeka.
   
 5. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Siasa na ulaji binafsi tu ndio vinaangaliwa zaidi kwa kisingizio cha kusogeza huduma kwa wananchi! Huu ni ufisadi.
   
Loading...