Rukwa: RC aagiza Walimu wawili kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kuwatia mimba wanafunzi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,420
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya, Dastan Mlelwa anafikishwa Mahakamani baada ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu.

Pia, RC Wangabo ameagiza Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpui iliyopo Halmashauri ya Sumbawanga anayedaiwa kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa kidato cha pili shule hapo na mwanafunzi huyo kuhamishiwa Shule ya Sekondari ya Mazwi Manispaa ya Sumbawanga, akamatwe na afikishwe Mahakamani.

Hii imekuja baada ya Rais Magufuli kufanya ziara mkoani Rukwa na kushangazwa na wanaume kutochukuliwa hatua baada ya kuwapa mimba wanafunzi 229 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Rais Magufuli alisema mkoa wa Rukwa ndio unaongoza kwa wanafunzi kupata mimba na kuwataka wanafunzi kuacha kiherehere na kujikita kwenye masomo kwani hayo watayakuta tu.

Rais Magufuli alisema
Kuna tatizo moja nimeliona kwenye Mikoa hii ya Rukwa ni mimba zimeongezeka, 2018 watoto 229 walipata mimba, sijasikia wanaume 229 wamefungwa zaidi ya miaka 30, na bado wanawatafuta wengine wawape mimba, wakati sheria zipo, RC yupo.
 
mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,461
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya Dastan Mlelwa anafikishwa mahakamani baada ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu.
Huyo Mwalimu anavuna kwenye shamba la shule ,mwalimu mkuu alikuwa anamlinda
 
Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,420
2,000
Naona RC kaogopa baada ya Rais kukemea vitendo vya wanafunzi kubebeshwa mimba huku viongozi wa mkoa wakishindwa kushughulikia suala hilo.
 
Vicky Cruz97

Member
Oct 21, 2019
65
125
Mm nadhan saa nyingine hata wanafunzi nao huwa wanajirahisisha wanafunzi nao wawe wanawajibishwa n.a. wahojiwe
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,275
2,000
Siku zote alikuwa wapi? Mpaka Rais afanye ziara ndiyo ajifanye anapambana kwa kuwatoa hao walimu kafara! Idadi ya mimba zilizotajwa mbona haziendani na idadi ya hao washukiwa?

Vyeo vingine ni vya kuvifutilia mbali tu. Havina tija yoyote ile zaidi ya kutumika tu kisiasa.
 
Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,187
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Rukwa kuhakikisha Mkuu wa Shule ya Sekondari Mzindakaya, Dastan Mlelwa anafikishwa Mahakamani baada ya kuwabaka na kuwatia mimba wanafunzi wawili wa kidato cha pili na cha tatu.

Pia, RC Wangabo ameagiza Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mpui iliyopo Halmashauri ya Sumbawanga anayedaiwa kumbaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa kidato cha pili shule hapo na mwanafunzi huyo kuhamishiwa Shule ya Sekondari ya Mazwi Manispaa ya Sumbawanga, akamatwe na afikishwe Mahakamani.

Hii imekuja baada ya Rais Magufuli kufanya ziara mkoani Rukwa na kushangazwa na wanaume kutochukuliwa hatua baada ya kuwapa mimba wanafunzi 229 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Rais Magufuli alisema mkoa wa Rukwa ndio unaongoza kwa wanafunzi kupata mimba na kuwataka wanafunzi kuacha kiherehere na kujikita kwenye masomo kwani hayo watayakuta tu.

Rais Magufuli alisema
Kuna tatizo moja nimeliona kwenye Mikoa hii ya Rukwa ni mimba zimeongezeka, 2018 watoto 229 walipata mimba, sijasikia wanaume 229 wamefungwa zaidi ya miaka 30, na bado wanawatafuta wengine wawape mimba, wakati sheria zipo, RC yupo.
Nmefanya Field mwaka jana kwenye hii shule yapata miezi 2! Baada tu ya kuondoka miezi kadhaa baadae nikasikia hii sakata ya mkuu kutia mimba dent wakati sie alkua anatusisitiza tuache kula watoto wake ndio kwanza tulkua hatuna muda nao zaidi ya kufuata kilichotupeleka, tulkua tunakula ma concubines wa Mtamila Bar na kitaani tu pesa tulkua nazo za kuhonga so hakutupa shida na risk ya kuharibu maisha yetu na 90% ya watoto wa hiyo shule wanaishi Magetoni(Wakiume kwa wasichana) sabu ndo shule ya kata kubwa kuliko zote eneo hilo na wengi wanatoka vijiji vya mbali sana...! Hivi vitoto bana ni vya kukaa navyo mbali bora ukomae na kina Mwajuma ndala mbili ukishindwa kutafuta plan B matokeo yake ndo haya sasa! Alafu huyo mkuu ana mke wake mkali kishenzi bado ni mbichi ni mwl wa Kaengesa P/S nashangaa tamaa na vitoto wakati mke wake nae bado mtoto tu... Daah wanaume bana sometimes tunashangaza....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom