RUKWA: RC aagiza walimu kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina

Miogozo mengine unasikiliza wakiondoka na wewe unachana page uliyoandika maisha yanaenda.

Sasa wewe kamvue hirizi ndio utajua bibi yake anafananaje wakati wa usiku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rc anatuchafulia mkoa wetu. Watu tunaotokea Rukwa tunaonekana wa ajabu Sana pale tunapokua mikoa mingine.

Anyway ngoja niongee na Bibi ampe show akili imkae sawa kidogo.
 
Ninao uzoefu mkubwa sana na mambo ya HIRIZI.

USIINGILIE KABISA HAYA MAMBO KICHWA KICHWA, UTAUMIA!!

nakumbuka miaka 20 iliyopita nikiwa nasoma shule ya msingi KWATA iliyoko KOROGWE VIJIJINI mkoani Tanga, tuliwahi kwenda kwa mtaalamu mmoja (aliitwa maji marefu kama sijakosea, alikuwa karibu na shule ya sekondari MAGOMA)

Kipindi hicho nilikuwa darasa la kwanza tu ila nakumbuka kila kitu

Kijijini pale kulivuma sana ishu za kupigana zongo, vibwengo kuja mpaka kwenye makazi ya watu usiku, kurushiana majini mashuleni, tukienda sokoni kule MAKANGARA basi sharti kila unachonunua ukifiche sana kwenye kapu mixer kufunika na nguo.

Yani ilikuwa vurugu tupu.

Basi Bwana, siku hio tukaenda kwa mtaalam, usiku usiku tukakuta foleni kubwa sana, watu wametoka mbali kuja kupata huduma.

Sisi tukakaa mpaka usiku wa manane ndipo zamu yetu ikafika. Kwangu ilikuwa ni jambo la kushangaza kwanza kuona watu wengi, magari (ushamba wangu mana ndo kwanza nimetoka mara kuja mkoa kusoma).

Tukaingia mmoja mmoja, nadhani maelekezo yalishatolewa kabla, tukachanjwa na kisha kila mmoja kupewa hirizi.

KWA MSIOIJUA HIRIZI
Hirizi ni kwa umbo iko kama tonge mviringo la ugali, rangi mara nyingi ni nyeusi. Inatengenezwa kwa vitu vingi vyenye nia ya kukinga dhidi ya jambo flani.

Okay, sisi pale tulipewa hirizi, mimi yangu nikawa nayo sharp.
Asubuhi tukaambiwa ukiona sindano moja haipo ujue adui yako kashambuliwa huko.

Nikaanza kupata shauku ya kuichunguza daily. Nikawa kila nikienda shule ni sharti niivae..

Jaman nimesoma Tanga, kule ukiwa smart kichwani lazima wakuchezee. Ukila vizuri lazima wakuchezee. Kila jambo la kimaendeleo lazima lifanyiwe figisu.

Nitaendelea baadae...
 
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewaagiza walimu wakuu na wakuu wa shule kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi wawapo shuleni, ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina.

Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

Taarifa: Nipashetz

Kuna Mtu aliwahi kuniambia All - Rounder kuwa kama kuna Mkoa ambao hata Baba wa Taifa aliuogopa na kuna RC alilazwa Darini ni wa Rukwa.
Huyo RC aache kuingilia mambo ya watu,

Anaweza kujitafutia matatizo bure

Washirikina na wachawi Sio watu , wanaweza mfanya mbaya
 
Ningekuwa na MTOTO huko ningemshirikisha mshana Jr amuandalie begi kabisaa!( joking)
 
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewaagiza walimu wakuu na wakuu wa shule kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi wawapo shuleni, ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina.

Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

Taarifa: Nipashetz

Kuna Mtu aliwahi kuniambia All - Rounder kuwa kama kuna Mkoa ambao hata Baba wa Taifa aliuogopa na kuna RC alilazwa Darini ni wa Rukwa.
Ushirikina ni imani kama ilivyo Ukristo na Uislamu. Kujaribu kuuingilia kwa njia rasmi hivyo ni kuvunja katiba.
 
Yaani huu ujinga wa kuvaa hirizi na Imani za kijinga huwezi kuzisikia KILIMANJARO wala ARUSHA ambayo imeongoza kufaulisha CSEE mwaka huu

Hii mikoa na ya pwani yenye ndoa za mitara, kucheza watoto ngoma na kucheza bao ni balaa tupu

Wabillah Tawfiq

Sent by Azarel
Kwani kuvaa hirizi ni ujinga?
 
Naona anaevaa hirizi na anaevaa rozari ni sawa. Rozari ni imani ya mtu na hirizi ni imani ya mtu.
Nashukuru kuisoma hii comment yako kabla sijacomment. Uko sahihi kabisa na ubarikiwe sana. Ni muhimu kila mtu kuheshimu imani ya mwenzake
 
Yaani huu ujinga wa kuvaa hirizi na Imani za kijinga huwezi kuzisikia KILIMANJARO wala ARUSHA ambayo imeongoza kufaulisha CSEE mwaka huu

Hii mikoa na ya pwani yenye ndoa za mitara, kucheza watoto ngoma na kucheza bao ni balaa tupu

Wabillah Tawfiq

Sent by Azarel
Hoja iko rukwa kuhusu hirizi,wewe unawananga wa pwani na ndoa zao za matala sio mitala Kama ulivyoandika.
Kuongoza matokeo kidato Cha nne sio hoja,hoja ni kua na maarifa yakusaidie maishani,unaweza kuwa uliiba mitihani ukaongoza Ila huna maarifa.
 
Back
Top Bottom