RUKWA: RC aagiza walimu kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina

Screenshot_20210122_164207.jpg
 
Ukisikia ulimbukeni ndio huu, hajapiga marufuku imani zilizoletwa na meli na kuja kutoka magharibi ya mbali, bali anapiga marufuku / kudharau imani za mababu zake ? Ama kweli emancipation from mental slavery inatakiwa...

Imani ni Imani tu iwe imeandikwa kwenye kitabu fulani au imetoka / tolewa katika kinywa cha watu fulani kupinga hii na kutokupinga ile (iwapo hakuna madhara) ni kuingilia uhuru wa kuabudu
 
Utaenda kumvua mtoto wa mtu hirizi chamoto utakiona vinginevyo uwe fiti na wewe kwenye ulozi au mcha Mungu kweli, lakini ukiwa mweupe unaweza kujuta maisha yako na familia yako ukaiponza...Wengine haya ni madhabahu yao wamehifadhi vitu vizito sana.
 
Utaenda kumvua mtoto wa mtu hirizi chamoto utakiona vinginevyo uwe fiti na wewe kwenye ulozi au mcha Mungu kweli, lakini ukiwa mweupe unaweza kujuta maisha yako na familia yako ukaiponza...Wengine haya ni madhabahu yao wamehifadhi vitu vizito sana.
Usitutisheee!!
 
Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

"Walimu wakuu na wakuu wa shule, wakagueni wanafunzi wenu ili muone kama wamevaa hirizi, kwani hayo ndiyo yanayowasumbua wanafunzi wengine, utakuta kwenye shule wanafunzi wanaugua ugonjwa wa kuanguka ovyo, hirizi ndiyo inasababisha hali hiyo," aliagiza.
Hirizi kwani ni kitu gani. Ni imani tu ya kujikinga. Mapete ya ajabu ajabu vidoleni mwenu , bangili za shaba mikononi mwenu, na hata baadhi ya chain mnazovaa mashingoni vyote hivyo ni hirizi pia. Inapishana tu matumizi yake.
 
Acha uongo. Kilimanjaro na Arusha wapo wengi tu wanavaa hirizi. Kwani unafaidika na nini kuongea uongo? Mimi nashindwa enda hata kwa bibi upareni sababu ya mambo hayo.
Labda kwa huko upareni na hiyo ni kama 4% labda na Tanga kiasi

Hatujawafikia wala hatufanani na washirikina na wacheza ngoma wa pwani na huko ufipa sijui Lindi

Kazi ujinga tu
 
Back
Top Bottom