RUKWA: RC aagiza walimu kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,527
2,000
MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo, amewaagiza walimu wakuu na wakuu wa shule kuwakagua wanafunzi ili kubaini iwapo wanavaa hirizi wawapo shuleni, ili kukabiliana na vitendo vya kishirikina.

Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

Taarifa: Nipashetz

Kuna Mtu aliwahi kuniambia All - Rounder kuwa kama kuna Mkoa ambao hata Baba wa Taifa aliuogopa na kuna RC alilazwa Darini ni wa Rukwa.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
19,703
2,000
Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

"Walimu wakuu na wakuu wa shule, wakagueni wanafunzi wenu ili muone kama wamevaa hirizi, kwani hayo ndiyo yanayowasumbua wanafunzi wengine, utakuta kwenye shule wanafunzi wanaugua ugonjwa wa kuanguka ovyo, hirizi ndiyo inasababisha hali hiyo," aliagiza.
 
The Technologist

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
641
1,000

Ye amejuaje kuwa hirizi ndo inasababisha hiyo Hali?

Hivi dawa ya malaria inaweza kusababisha mtu apate malaria?
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,304
2,000
Ilani labda inasisitiza kufyekelea mbali ulozi majumbani na mashuleni!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
18,915
2,000
Yaani huu ujinga wa kuvaa hirizi na Imani za kijinga huwezi kuzisikia KILIMANJARO wala ARUSHA ambayo imeongoza kufaulisha CSEE mwaka huu

Hii mikoa na ya pwani yenye ndoa za mitara, kucheza watoto ngoma na kucheza bao ni balaa tupu

Wabillah Tawfiq

Sent by Azarel
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,273
2,000
Yaani huu ujinga wa kuvaa hirizi na Imani za kijinga huwezi kuzisikia KILIMANJARO wala ARUSHA ambayo imeongoza kufaulisha CSEE mwaka huu

Hii mikoa na ya pwani yenye ndoa za mitara, kucheza watoto ngoma na kucheza bao ni balaa tupu

Wabillah Tawfiq

Sent by Azarel
Siwatetei. Ila hii mikoa ya pwani wanatamaduni hizo. Na hiziri.. sijui na madudu gani ni mambo ya imani zao.

Hatuwez lingana sababu jamii zinatofautiana kitamaduni. Huyo mkuu wa mkoa atafanya msako mpaka achoke. Lakin ataishia hapo hapo.. wanarithishana hao..
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
11,648
2,000
Agizo hilo alilitoa jana kwenye mkutano alioufanya Kijiji cha Malonje wilayani Sumbawanga kutokana na baadhi ya wananchi kudaiwa kuwa na tabia ya kuwaita waganga wa jadi, maarufu lambalamba, na kuwalipa fedha ili wawasafishie nyumba na mali zao.

"Kutokana na baadhi ya wazazi wa wanafunzi kuamini ushirikina kupita kiasi, huenda wakawapa hata watoto wao hirizi na matunguli ili waende nayo shuleni wakiamini kuwa vitu hivyo vitawalinda watoto wao hali ambayo itasababisha usumbufu kwa wanafunzi wengine.

"Walimu wakuu na wakuu wa shule, wakagueni wanafunzi wenu ili muone kama wamevaa hirizi, kwani hayo ndiyo yanayowasumbua wanafunzi wengine, utakuta kwenye shule wanafunzi wanaugua ugonjwa wa kuanguka ovyo, hirizi ndiyo inasababisha hali hiyo," aliagiza.
Mambo ni 🔥🔥🔥🔥🔥🔥 ukisikia 5 tena ndiyo hii sasa. Mingine feki
 
Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,487
2,000
Yaani huu ujinga wa kuvaa hirizi na Imani za kijinga huwezi kuzisikia KILIMANJARO wala ARUSHA ambayo imeongoza kufaulisha CSEE mwaka huu

Hii mikoa na ya pwani yenye ndoa za mitara, kucheza watoto ngoma na kucheza bao ni balaa tupu

Wabillah Tawfiq

Sent by Azarel
Acha uongo. Kilimanjaro na Arusha wapo wengi tu wanavaa hirizi. Kwani unafaidika na nini kuongea uongo? Mimi nashindwa enda hata kwa bibi upareni sababu ya mambo hayo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom