Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 20,713
- 45,096
Kwa kushindwa kwake kutii amri ya Waziri Kangi Lugola ya kuwahamisha askari polisi waliokuwa wanatuhumiwa kwa rushwa.
Sasa ripoti zimefika kwa Rais Magufuli na RPC kaitwa mbele ya hadhara kaishia kujiuma uma tu.
Nafikiri baada ya mkutano huu, Rais atakutana na wasaidizi wake juu ya RPC huyu wa Rukwa.
Tumuombee hekima na busara Rais Magufuli, asimtumbue RPC japo polisi ni waonevu ila kama binadamu tumuombee tu asitumbuliwe.
Nawasilisha
----- Update-----
Rais Magufuli amemtaka IGP Sirro kumshusha cheo aliyekuwa kaimu RPC Rukwa na mara moja amsimamishe kazi hadi pale atakapotoa maelekezo mengine.
-
Akihutubia mamia na makumi ya wananchi wa Mji mdogo wa Laela Mkoani Rukwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amehoji ni kwasababu gani amri halali ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya kuwataka Askari baadhi waliotuhumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa matumizi mabaya ya ofisi na ulaji rushwa hawajachukuliwa hatua hadi leo hii.
Ndipo sasa RPC wa Rukwa alipotakiwa na JPM kueleza ni kwanini asichukuliwe hatua kwa puuzo lile la kutekeleza amri ya Waziri. Akijitetea mbele ya Mheshimiwa Rais RPC wa Rukwa amedai wakati wa takwa lile la Waziri lugola hakuwepo.
Akiwa na hofu na kutokujiamini RPC wa Rukwa amewaangushia jumba bovu OCD wa Laela na Afisa mmoja aliyemkaimisha madaraka baada ya yeye kuwa safari.
Rais Magufuli amemtaka IGP Sirro kumshusha cheo aliyekuwa kaimu RPC Rukwa na mara moja amsimamishe kazi hadi pale atakapotoa maelekezo mengine.