Rukwa: Rais Magufuli amtaka IGP kumshusha cheo na kumsimamisha kazi Kaimu RPC kwa kudharau amri halali ya Waziri Kangi Lugola

Makosa mengine sio ya kufukuzana kazi kabisa ila ndio hivyo tena maana kuna watu wanajisikia faraja kuu mioyoni mwao kila wanapoinflict maumivu kwa watu wengine. Huu ni ugonjwa na ukipea sana mtu anaweza kugeuka kuwa serial killer
Sadist in power.
 
Jeshi la polisi linaenda kisiasa sana,kila mwanasiasa anataka kujichukilia pointi kwa hao Askari,wanafanya linaonekana kama jeshi dhaifu sana.Walipe heshima,ndiyo linafanya wanapohutubia au kufanya mambo yao ndani ya nchi,kuwe na usalama wa mali zao na watu wao.
Tatizo limeanzishwa na polisi wenyewe, wanakubali kutumika na hasa katika kupambana na vyama vya upinzani.
Kwanza wanasahau kuwa watetezi wakubwa wa maisha yao wamekuwa hao hao wapinzani, wamepigania makazi yao kutoka mabanda ya kuku hadi nyumba za binadamu, mavazi na maslahi lakini wao hawalioni hilo.
SHAURI YAO mazafanta!
 
Kumbuka JWTZ nao walifanya usafi kipindi cha wale upinzani walipotaka kufanya kitu kinaitwa UKUTA lakini lawama zilienda kwa polisi,hawa watu tunawalaumu kwasababu mteuzi wa mkubwa wao,i.e IGP ni mkuu wa nchi ambaye ni kada na mwenyekiti wa chama tawala,wasipotii mamlaka yake au ya waliochini yao,huenda wakapata matatizo.
JWTZ pia wangekua wanashughulika na mambo ya ndani kabisakabisa,hakika nao tungewalaumu tu,tena yawezekana so,sababu kubwa ni wanasiasa wanaokua na nguvu kuliko wanaoongoza vyombo hivi.
 
Kwa kushindwa kwake kutii amri ya Waziri Kangi Lugola ya kuwahamisha askari polisi waliokuwa wanatuhumiwa kwa rushwa.

Sasa ripoti zimefika kwa Rais Magufuli na RPC kaitwa mbele ya hadhara kaishia kujiuma uma tu.

Nafikiri baada ya mkutano huu, Rais atakutana na wasaidizi wake juu ya RPC huyu wa Rukwa.

Tumuombee hekima na busara Rais Magufuli, asimtumbue RPC japo polisi ni waonevu ila kama binadamu tumuombee tu asitumbuliwe.

Nawasilisha
Akimaliza kwetu anakuja kwenu Lisu ali tabiri mapema
 
Kwa kushindwa kwake kutii amri ya Waziri Kangi Lugola ya kuwahamisha askari polisi waliokuwa wanatuhumiwa kwa rushwa.

Sasa ripoti zimefika kwa Rais Magufuli na RPC kaitwa mbele ya hadhara kaishia kujiuma uma tu.

Nafikiri baada ya mkutano huu, Rais atakutana na wasaidizi wake juu ya RPC huyu wa Rukwa.

Tumuombee hekima na busara Rais Magufuli, asimtumbue RPC japo polisi ni waonevu ila kama binadamu tumuombee tu asitumbuliwe.

Nawasilisha
Kapewa maelekezo kayadharau. Wananchi wanabbikiwa kesi kwa ajili ya tamaa ya askari wachache.

Swali:

Asipotumbuliwa wewe unafaidika na nini?
 
Akihutubia mamia na makumi ya wananchi wa Mji mdogo wa Laela Mkoani Rukwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amehoji ni kwasababu gani amri halali ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya kuwataka Askari baadhi waliotuhumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa matumizi mabaya ya ofisi na ulaji rushwa hawajachukuliwa hatua hadi leo hii.

Ndipo sasa RPC wa Rukwa alipotakiwa na JPM kueleza ni kwanini asichukuliwe hatua kwa puuzo lile la kutekeleza amri ya Waziri. Akijitetea mbele ya Mheshimiwa Rais RPC wa Rukwa amedai wakati wa takwa lile la Waziri lugola hakuwepo.

Akiwa na hofu na kutokujiamini RPC wa Rukwa amewaangushia jumba bovu OCD wa Laela na Afisa mmoja aliyemkaimisha madaraka baada ya yeye kuwa safari.

Rais Magufuli amemtaka IGP Sirro kumshusha cheo aliyekuwa kaimu RPC Rukwa na mara moja amsimamishe kazi hadi pale atakapotoa maelekezo mengine.
 
Hapo mtu kajitetea tu inawezekana kabisa alipewa hiyo amri ya lugola na huyo aliyemuachia ofc akampuuza leo kamgeuzia kibao mwenzie daaah
 
Back
Top Bottom