Rukwa: Rais Magufuli amtaka IGP kumshusha cheo na kumsimamisha kazi Kaimu RPC kwa kudharau amri halali ya Waziri Kangi Lugola

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
7,875
2,000
56907188-950B-4D06-9CC8-1050632FE886.jpeg

Kwa kushindwa kwake kutii amri ya Waziri Kangi Lugola ya kuwahamisha askari polisi waliokuwa wanatuhumiwa kwa rushwa.

Sasa ripoti zimefika kwa Rais Magufuli na RPC kaitwa mbele ya hadhara kaishia kujiuma uma tu.

Nafikiri baada ya mkutano huu, Rais atakutana na wasaidizi wake juu ya RPC huyu wa Rukwa.

Tumuombee hekima na busara Rais Magufuli, asimtumbue RPC japo polisi ni waonevu ila kama binadamu tumuombee tu asitumbuliwe.

Nawasilisha

----- Update-----
Rais Magufuli amemtaka IGP Sirro kumshusha cheo aliyekuwa kaimu RPC Rukwa na mara moja amsimamishe kazi hadi pale atakapotoa maelekezo mengine.

-
Akihutubia mamia na makumi ya wananchi wa Mji mdogo wa Laela Mkoani Rukwa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli amehoji ni kwasababu gani amri halali ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya kuwataka Askari baadhi waliotuhumiwa na wananchi wa eneo hilo kwa matumizi mabaya ya ofisi na ulaji rushwa hawajachukuliwa hatua hadi leo hii.

Ndipo sasa RPC wa Rukwa alipotakiwa na JPM kueleza ni kwanini asichukuliwe hatua kwa puuzo lile la kutekeleza amri ya Waziri. Akijitetea mbele ya Mheshimiwa Rais RPC wa Rukwa amedai wakati wa takwa lile la Waziri lugola hakuwepo.

Akiwa na hofu na kutokujiamini RPC wa Rukwa amewaangushia jumba bovu OCD wa Laela na Afisa mmoja aliyemkaimisha madaraka baada ya yeye kuwa safari.

Rais Magufuli amemtaka IGP Sirro kumshusha cheo aliyekuwa kaimu RPC Rukwa na mara moja amsimamishe kazi hadi pale atakapotoa maelekezo mengine.
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,968
2,000
Jeshi la polisi linaenda kisiasa sana,kila mwanasiasa anataka kujichukilia pointi kwa hao Askari,wanafanya linaonekana kama jeshi dhaifu sana.Walipe heshima,ndiyo linafanya wanapohutubia au kufanya mambo yao ndani ya nchi,kuwe na usalama wa mali zao na watu wao.
 
ki2c

JF-Expert Member
Jan 17, 2016
2,968
2,000
Hivi mfanyakazi akituhumiwa kwa Rushwa anahamishwa kituo?

AU

Anasimamishwa kazi na mamlaka husika ili kupisha uchunguzi?
Kwa Tanzania inategemeana na kipi ambacho mkuu wa kazi ataona kitampendeza mwanasiasa.
 
maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
9,361
2,000
Basi naye ni fal.a kama alipewa maagizo akakaa nayo...tena usawa huu... bora niombee wagonjwa kuliko kumuombea mzembemzembe
 
pureView Zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
5,311
2,000
Ingawa ni waonevu Sana hawa polisi tunamuomba jiwe ampasue kabisa vipande vipande..
Hawa malofa wanajidai Sana ukiwakuta Kwenye anga zao
 
kandawe

JF-Expert Member
Jun 24, 2013
1,139
2,000
Kwa kushindwa kwake kutii amri ya Waziri Kangi Lugola ya kuwahamisha askari polisi waliokuwa wanatuhumiwa kwa rushwa.

Sasa ripoti zimefika kwa Rais Magufuli na RPC kaitwa mbele ya hadhara kaishia kujiuma uma tu.

Nafikiri baada ya mkutano huu, Rais atakutana na wasaidizi wake juu ya RPC huyu wa Rukwa.

Tumuombee hekima na busara Rais Magufuli, asimtumbue RPC japo polisi ni waonevu ila kama binadamu tumuombee tu asitumbuliwe.

Nawasilisha
Keshapewa muda wa kutekeleza agizo na definitely keshafanya maana alirudi na karatasi nafikiri ina majibu ya utekelezaji wa agizo.
Labda tena lizuke lile la waliowekwa ndani kuwekewa dhamana.
Lakini inavyoonekana Mh JPM ameshamhurumia ni kazi yake sasa RPC kubadirika na aende na kasi ya Mh Rais.
 
ZENJIBARIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
616
1,000
Kama wanaukula rushwa adhabu yao ni kupewa uhamisho basi Mahakama ya rushwa ivunjwe,manake itakuwa haina kazi ya kuamua chochote juu ya wala rushwa.
Kutokomeza rushwa ni LAZIMA watuhumiwa na wahukumiwa utumikie kifungo na kufutwa kazi kabisa,ili iwe funzo kwa wengine. Bila ya hivyo tutaendelea kuishi na utamaduni wa rushwa
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,738
2,000
Waziri ana mamlaka kwanini hakuwaondoa yeye, kwanini amuagize rpc badala ya kumalizana nao alipokuwa huko.
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,963
2,000
Amekwishaliwa kichwa live,Rais kampigia IGP kamwambia amsimamishe kazi muda huo.huo
Ni kwa vile ni ACP angekua koplo naona angevuliwa vimbavu hadharani
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
25,963
2,000
Kama wanaukula rushwa adhabu yao ni kupewa uhamisho basi Mahakama ya rushwa ivunjwe,manake itakuwa haina kazi ya kuamua chochote juu ya wala rushwa.
Kutokomeza rushwa ni LAZIMA watuhumiwa na wahukumiwa utumikie kifungo na kufutwa kazi kabisa,ili iwe funzo kwa wengine. Bila ya hivyo tutaendelea kuishi na utamaduni wa rushwa
Ushahidi ni wa kimazingira,uhamisho ni sehemu ya adhabu jeshini
Anaweza kupelekwa kua askari wa farasi wakati yeye ni mpelelezi
Au kama ni trafiki unapelekwa pemba akuchukue hela za majini ufilie mbali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom