Rukwa: Radi yabomoa ukuta wa nyumba na kuua mtu mmoja

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,444
3,354
Mtu mmoja mkazi wa kijiji na kata ya Mkoe wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Girubat Lungwa (34) amefariki dunia baada ya radi kubomoa ukuta wa nyumba yake kisha kuingia ndani na kusabisha kifo chake hapo hapo.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea kufuatia mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na upepo mkali kunyesha maeneo hayo kisha kusababisha kifo cha mtu huyo moja na mmoja kujeruhiwa wote ndugu wa familia moja.

Awali akisimulia mkasa huo mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Machipa amesema radi hiyo iliingia ndani ya nyumba ya mwananchi wake kupitia kona ya nyumba yake ambapo kabla ya kuingia ilichoma mifugo yake wakiwemo mbuzi watatu ,kuku na mbwa mmoja.

Revocatus Lungwa ambaye ni mmoja wa wathirika wa tukio hilo, amesema radi hiyo ilimpiga mara baada ya kusabisha maafa kwa kaka yake.

Kaimu mtendaji wa kata hiyo Noel Kaduma amekiri kutokea kwa tukio hilo nakusema tukio ni la pili kutokea katika maeneo hayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Radi za digital hizo, zinakufuata hadi uvunguni mwa kitanda

thanks to god the almighty
 
Eti RADI imebomoa ukuta, kuingia ndani na kuua mtu.
Kwa maoni yangu: Huu ni uandishi habari wa hovyo kabisa kuwahi kutokea mwaka huu wa 2019.
Yaani radi inavyoelezewa utafikiri ni kiumbe mwenye miguu anayetembea na kufanya matendo mithili ya mwanadamu. Ndiyo haya haya ya kuamini kuwa kuna "samaki mtu" mwenye umbile kama mwanadamu na ana sura nzuri mithili ya malaika; au kuamini kuwa kuna kiumbe anayeitwa 'dragon' anayetoa moto mdomoni.
 
Tuliotokea maeneo yenye radi nyingi hili haiwezi kushangaza kama ulivyotaka iwe na kukosoa mleta habari.

Radi inavunja hadi miti inapokuwa imepita hapo.
Radi kupiga ukuta na kubomoa si la kushangaza kabisa. Na yawezakana mtu huyo kilichomuua ni ukuta uliomwangukia au alikaa kwenye njia ya radi ilipopitia.

Radi ni umeme wenye nguvu sana japo kisayansi sijui wanaelezeaje ile nguvu ya usukumaji wa vitu na kuvunja.
Ila hilo la kubomoa na kuua ni la kawaida sana
 
Eti RADI imebomoa ukuta, kuingia ndani na kuua mtu.
Kwa maoni yangu: Huu ni uandishi habari wa hovyo kabisa kuwahi kutokea mwaka huu wa 2019.
Yaani radi inavyoelezewa utafikiri ni kiumbe mwenye miguu anayetembea na kufanya matendo mithili ya mwanadamu. Ndiyo haya haya ya kuamini kuwa kuna "samaki mtu" mwenye umbile kama mwanadamu na ana sura nzuri mithili ya malaika; au kuamini kuwa kuna kiumbe anayeitwa 'dragon' anayetoa moto mdomoni.
TULIA WEWE MWANAUME WA DSM MBONA UPOFASTA KUKOSOA UTAZANI WOTE HUMU NIWAANDISHI WA HABARI
 
Eti RADI imebomoa ukuta, kuingia ndani na kuua mtu.
Kwa maoni yangu: Huu ni uandishi habari wa hovyo kabisa kuwahi kutokea mwaka huu wa 2019.
Yaani radi inavyoelezewa utafikiri ni kiumbe mwenye miguu anayetembea na kufanya matendo mithili ya mwanadamu. Ndiyo haya haya ya kuamini kuwa kuna "samaki mtu" mwenye umbile kama mwanadamu na ana sura nzuri mithili ya malaika; au kuamini kuwa kuna kiumbe anayeitwa 'dragon' anayetoa moto mdomoni.
Wewe nadhani ndo ujawai shuhudia nguvu ya huu umeme, yaan radi ikipiga wastani wa umeme unaosafiri kutoka juu ya mawingu kuja ardhini ni voltage billion 1 na joto lake ni mara tano ya joto liloko juu ya uso wa Jua na ndo inasababisha hewa kutanuka na kuvibrate ndo sababu ya minguromo, hii kitu ikipiga mti, maji yote ya mti yanakua mvuke na mti unakauka na kupasuka kama bomu. Sasa wewe linaweza hata lisikuguse lakini ukaungua mpaka kufa, kama limepiga karibu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko ndiko kwa Wafipa

Jamaa hawana mchezo kanda hiyo wanajua jinsi ya kumaliza kesi zao wao hawahitaji polisi wala mahakama. Makombora yao huyatuma na kwa kawaida hayawezi kwenda off target.

Poleni wafiwa ila nawasihi wandugu haya maisha sote ni wapitaji, tusifanyiane ubaya wala tusilipe visasi!

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Eti RADI imebomoa ukuta, kuingia ndani na kuua mtu.
Kwa maoni yangu: Huu ni uandishi habari wa hovyo kabisa kuwahi kutokea mwaka huu wa 2019.
Yaani radi inavyoelezewa utafikiri ni kiumbe mwenye miguu anayetembea na kufanya matendo mithili ya mwanadamu. Ndiyo haya haya ya kuamini kuwa kuna "samaki mtu" mwenye umbile kama mwanadamu na ana sura nzuri mithili ya malaika; au kuamini kuwa kuna kiumbe anayeitwa 'dragon' anayetoa moto mdomoni.
Inasemekana imekamatwa wakaiti inatoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom