Rukwa: Mwanamke apigwa mawe hadi kufa kwa tuhuma za ushirikina

Hatari mkuu,,,matokeo yake ananipiga kimya kimya,,, wachawi watu wabaya sn,,,sio wa kuwachekea,,,pengine mkuu ulipaswa uwe hata mteule wa rais,,,lakini wachawi wamekupeleka shughuli zingine...ha ha ha ha..nuksi tupu hawa..
Achana na kufikiria Uteule, huo ni utumwa na siku akiamka vibaya anakudhalilisha vibaya sana!
 
bora niibiwe mali kuliko mtoto
Mhu! Tunachokiita uchawi/ushirikina ni namna jamii inavyoshughulikia migogoro yake, lakini si kwa namna kwamba baadhi ya watu wanazaliwa na au wana nguvu za kuwadhuru wengine kwa hizo nguvu. Hata maandishi yanayotaja uchawi/ushirikina kwenye Biblia mfano hayaongelei 'inert power' bali 'magic' - yaani kufanya au kuona jambo linalotendeka kwa namna ambayo si ya kawaida. Mfano, tricks. Babu aliogopwa sana wilaya nzima kwamba alikuwa na nguvu za kuwafichua wachawi na hata tulipokuwa tukimtembelea nyumbani kwake kulikuwa na dawa kila sehemu na alikuwa amefanikiwa kuwaaminisha watu kuwa yeye yuko juu ya wachawi. Lakini alipokaribia kufa alimwambia mtoto wake kwa kwanza kwamba yote hayo aliyowaaminisha watu hayakuwa kweli ayapuuze na mtoto wake alitoa ushuhuda huo msibani na kila mtu alishangaa.

Mfano, alikuwa anaelezea dhana ya kwamba mtu anafariki dunia halafu ukienda kwa waganga wanakuaminisha kuwa atapatikana, lakini hakuna aliyekwisha kufariki dunia na waganga wakamrejesha kwa ndugu zao. Na hata kama ingewezekana inakuwaje tuite uchawi/ushirikina? Hata mimi niliyoyaandika siyo kwamba sikuyafanyia kazi maana na mimi nilizaliwa kwenye jamii iliyokuwa inaamini uchawi na nilikulia kwenye jamii hiyo hiyo na niliamini huo uchawi/ushirikina ingawa sikuwa na sababu yoyote ya kuamini hivyo. Wilayani kwetu watu walichelewa kujenga kwa sababu ya kuogopa kurogwa na walioona kuwa wale waliotuhumiwa kuwa wachawi/washirikina nao wanafariki dunia na familia zao pia ni duni na ni sasa tu vijana wameenza kuchangamkia fursa za biashara na kujenga. Elimu ya sekondari nilisoma mbali na nyumbani na nakumbuka kwa kuogopa kurogwa mama aliniomba nisiwe naenda likizo nyumbani, lakini nilimwambia ni heri waniroge kuliko kutoenda nyumbani likizo na nilikuwa nawaambia watu lini nitafika na lini nitaondoka wakati wengine huwa wanafika na kuondoka bila watu wengine kujua. Mimi nimeamua kuishi maisha yangu na siwezi kuishi maisha ya wengine.

Kwa sasa ukiwaambia vijana wa kwetu ya uchawi/ushirikina hawakuelewi ingawa wengine ambao maisha bado yanawachenga wanadhani wachawi ndio wamewafanya hivyo walivyo. Ni 'useless' and unfounded to draw a conclusion kwamba ugonjwa, 'physical deformity', majanga na ajali vinaletwa na wachawi au watu tunaowadhania kuwa ni wabaya wetu katika jamii. Na ndiyo maana tuna'resort' kwenye kuua wazee as if hatutazeeka. What a pity! Hata mtu anihubiri kiasi gani imani ya uchawi kwangu "NO" ingawa pia nimekutana na misukosuko mingi ya maisha ambayo kwa mtu mwingine angewashika watu wengine uchawi. Hata dissertation yangu ya kwanza niliandika kuhusu dhana ya 'evil' na nyingine kuhusu imani ya ushirikina/uchawi. Kwangu jambo ambalo hatujui limetokeaje hatuwezi kusema kwa uhakika kwamba limesababishwa na wachawi/washirkina au uchawi/ushirikina.

You cannot claim a fact you cannot justify or at least prove it. If you do then that is wrong or erroneous reasoning. Kuna watu huwa nawaambia kwa nini ukiwaona watoto wa mbwa au paka kwa mbali let's say mita 100 hivi halafu ukiulizwa ni yupi paka au mbwa jike utoe jibu? Ni 'ridiculous'! Usipojua kuwa na uhakika na jambo suspend judgement mpaka hapo utakapojiridhisha kwamba ni kweli. Watu wengi tunakimbilia kuhukumu watu na kuwachoma moto, lakini hatuna uhakika wowote kwamba ndio wamefanya hilo tukio. Nikama utoke nyumbani na kumwacha mfanyakazi na ukirudi jioni ukute laptop yako imepasuka na halafu useme yeye ndiye kaipasua. Unajuaje? Ulimwona akiipasua?
 
Kwa maelezo haya huu uzi umeufunga kabisa ni bahati mbaya sana waliokaririshwa uchawi hawatakubali kirahisi.

Haya ni mauaji ya kikatili sana haikubaliki Jeshi la polisi lifanye liwasake hao wahuni.
Mkuu umeangalia upande mmoja tu wa shilingi, je kisababishi haukioni?

Jihisi kupotelewa kitatanishi na mwanao kipenzi wa kuzaa, halafu kwa kudra, apatikane kafichwa kwa kigagula huku kajazwa matakataka!

Hilo la kufuata sheria utalikumbuka kweli?

Mkuu kuna mambo ya kuvumilia, lakini mengine ni mtihani sana.
 
Kuua sio suluhisho la kumaliza tatizo

Back
Top Bottom