Rukwa: Mwanamke apigwa mawe hadi kufa kwa tuhuma za ushirikina

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
363
500
JESHI la Polisi mkoani Rukwa linawasaka watu wasiojulikana kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga mawe, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Maria Birika (40), mkazi wa Kijiji cha Myunga, Kata ya Mkali, wilayani Kalambo.

Imeelezwa kuwa watu hao wamemfanyia kitendo hicho kwa kumtuhumu kujihusisha na vitendo vya kishirikina.

Tukio la mauaji ya mwanamke huyo lilitokea Juni 26, saa 12:00 jioni baada ya watu hao kufika nyumbani kwake na kumkuta mtoto aliyefahamika kwa jina Given Lameck (15), akiwa amefungiwa nyumbani kwa mwanamke huyo, huku akiwa amefungwa kitambaa chekundu usoni.

Kabla ya mauaji hayo, mtoto Given alipotea nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha, ndipo harakati za kumtafuta zilianza, na kwamba ndugu zake walimtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, alisema baada ya jitihada za kumpata mtoto huyo kushindikana, waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji kisha kuendelea kumtafuta.

Alisema baada ya kumtafuta kwa muda mrefu walifanikiwa kumkuta nyumbani kwa mwanamke huyo akiwa amefungiwa ndani na amefungwa kitambaa chekundu usoni, huku akionekana kana kwamba amechanganyikiwa kutokana na kuongea vitu visivyoeleweka.

Baada ya kupatikana kwa mtoto huyo, ndipo watu waliokuwa wakimtafuta walipo hamaki na kushikwa na hasira na kuanza kumpiga mwanamke huyo kwa mawe na vipande vya matofali vilivyokuwa karibu na nyumba yake na kumsababishia majeraha makubwa, kuvuja damu nyingi na kufariki dunia kutokana na kukosa matibabu ya haraka.

Kamanda Masejo alitoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Rukwa kuachana na imani za kishirikina katika matukio yanayotokea mkoani humo, kwa kuwa imani hizo zimekuwa chanzo cha vifo vingi vinavyotokana na kujichukulia sheria mikononi.

Chanzo: IPP Media
 

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,370
2,000
Haya ni mauaji ya kikatili sana haikubaliki Jeshi la polisi lifanye liwasake hao wahuni.
 

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
3,564
2,000
Haya ni mauaji ya kikatili sana haikubaliki Jeshi la polisi lifanye liwasake hao wahuni.
Hao wahuni hawana hatia yeyote...huyo mama alihukumiwa kama mwizi wa vitu vya watu...hivi kwani watu wakiua maua jambazi kosa lipo wapi? huyo mama kakutwa na mtoto aliyeibiwa,,,kwahyo ni mwizi..sioni kosa la hao jamaa
 

mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
3,564
2,000
Mjinga ni wewe usiyeelewa comment yangu...nimekwambiya huyo mama ni mwizi kama wezi wengine tu..iweje akae na mtoto wa mtu wakati anatafutwa? Tena amfungie chumbani na kumgeuza akili ,,,,Leo uibiwe gari na vitu vya thamani,, uvikute nyumbani kwangu ,,,nani mwizi?je utachukuwa hatua gani?watu kama hao ndy wanarudisha nyuma maendeleo ya watu,,,wanga na wachawi...kuna watu wangapi wanauliwa na wanainchi wenye hasira Kali?msitete upuuzi
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
2,718
2,000
Yangotokea ulaya ungeona Miafrica ya Buza au Kakora inapost Black Lives Matter kwe he Status zao za Watsap.


Ila huyu mama kauawa na manyani wenzake tunaona kawaida tu. Kweli Miafrica sisi Ni laana.
Umekulia wapi ndugu yangu hadi hili suala lionekane jipya kiasi hicho !!!

Sihalalishi chochote ila ukikaa maeneo yenye ushirikina ndio utaelewa hayo masuala ya watu kutoweka kimazingira tatanishi au vifo ambavyo havieleweki..

Imagine ndugu yako katoweka halafu unakuja kupata taarifa kawekwa kishirikina na mtu.. mnaenda kumuokoa huku akiwa hajielewi, unadhani ukikutana na mtu alieyafanya hayo utamchekea !!!!!

Kuua sio sawa lakini hata marehemu ni muhalifu tu na huwezi jua wasingempata alikuwa na mpango nae gani
 

promethus

Senior Member
Feb 22, 2016
161
250
Huwa nashangaa sana michango ya watu humu wanaojifanya eti ni werevu kumbe n wajinga wa kutupwa.
Ushirikina upo sana Rukwa hasa maeneo ya vijijini waliowahi kuishi huko wanaweza kuwa mashuhuda wazuri wa hayo mambo.

NB:kila binadamu ana haki ya kuishi sikubaliana kabisa na kitendo cha watu kujichukulia sheria mkononi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom