Rukwa: Mwanafunzi aozwa kwa Mahari ya Tsh. 330,000 na Nguruwe mmoja

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
MKAZI wa Kitongoji cha Mabatini, wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Kennedy Fumpa (37), amekamatwa kwa tuhuma za kumuoa mwanafunzi wa darasa la tatu baada ya kulipa mahari ya Sh. 330,000 pamoja na nguruwe mmoja.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa), alikuwa darasa la tatu na alilazimika kuacha shule baada ya bibi yake aliyekuwa akimlea kupokea mahari hiyo hivi karibuni na mjukuu wake kuhamia kwa mwanamume huyo ili wakaanze maisha ya ndoa ya mume na mke.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Godfrey Kalungwizi alisema serikali ya kijiji ilipata taarifa kutoka kwa uongozi wa shule kuwa mwanafunzi huyo amekuwa mtoro shuleni kwa muda mrefu ndipo jitihada za kumtafuta zikaanza.

Alisema baada ya jitihada za uongozi wa kijiji kumtafuta mwanafunzi huyo na kumbana bibi aliyekuwa anamlea, alieleza kuwa alikwisha pokea mahari na mjukuu wake huyo tayari amekwisha olewa.

"Baada ya kufuatilia tulibaini kuwa bibi huyo alimuoza mjukuu wake kwa mahari ya Sh. 400,000, ambapo alipokea Sh. 330,000 taslimu na mnyama aina ya nguruwe mwenye thamani ya Sh. 70,000 na kukamilisha kiwango cha mahari alichopangiwa na kumchukua mwanafunzi huyo," alisema.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule aliyokuwa akisoma mwanafunzi huyo, Josephat Joseph, alisema alikuwa haudhurii masomo na kwamba akaorodheshwa katika wanafunzi watoro wa muda mrefu mpaka uongozi wa shule ulipotoa taarifa kwenye serikali ya kijiji na kukamatwa akiwa tayari ameolewa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali, alithibitisha tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Oktoba 15 na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani. Alisema kisichokubalika ni kumbadilisha mtoto wa kike na nguruwe na sheria ya kumlinda mtoto ipo lazima ifuate mkondo wake.

IPPMEDIA
 
Jamaa huyu achapwe viboko 1500 akiwa uchi na akatwe kichwa chake cha dushe ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wasanii wenye matamanio.
 
Daaaahhhh siku zinaenda kasi sana, kumbe Piter Lijualikali sasa hivi ni muheshimiwa mkuu wa wilaya.
 
Nahisi ni ushirikina wa Rukwa, Miaka 37 kuoa miaka 11? Labda kama ni mental case vinginevyo pawepo na influence nyingine.
Miaka 37 hakujua consequences za kitendo alichokifanya? hakupata hata rafiki wa kumshauri?
 
Magereza siku hizi hamna shuruba kabisa. Watu hawaogopi kuingia kabisa. Mtu akiingia akitoka anaendeleza mishe zile zile. Mtu anatakiwa akitoka huko ata akiokota smart anapeleka kituoni.
 
Magereza siku hizi hamna shuruba kabisa. Watu hawaogopi kuingia kabisa. Mtu akiingia akitoka anaendeleza mishe zile zile. Mtu anatakiwa akitoka huko ata akiokota smart anapeleka kituoni.
 
Back
Top Bottom