Rukwa: Mwalimu adaiwa kumpiga Mwanafunzi machoni kwa fimbo na kumsababishia upofu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
MWANAFUNZI Nicholaus Kwimba (17) wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kate, Nkasi mkoani Rukwa amepata tatizo la uoni kutokana na kupigwa fimbo na mwalimu wake kwenye macho na kumsababishia kushindwa kuona

Kutokana na kitendo hicho, Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia mwalimu Peter Silamba wa shule hiyo kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia tatizo hilo mwanafunzi huyo.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Mathias Nyange, alisema tukio hilo lilitokea Mei 21 majira ya saa 2:30 asubuhi shuleni hapo wakati akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa kufika shuleni.

Akisimulia tukio hilo mwanafunzi huyo ambaye amelazwa wodi namba tatu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, mwanafunzi huyo alisema mwalimu huyo alikuwa akiwaadhibu wanafunzi waliochelewa kufika shuleni na yeye alikuwa mmoja wao.

“Alipomchapa mwanafunzi mwenzangu ambaye alikuwa wa kwanza kuchapwa, mimi nililala chini kisha mwalimu alinichapa viboko viwili wakati akitaka kunichapa cha tatu niligeuza uso na kumwangalia na kisha alinichapa kwenye macho na ghafla nikaacha kuona na mpaka sasa nipo wodini licha ya matibabu ninayopata lakini bado sijaanza kuona,” alisema.

Kwimba alisema baada ya mwalimu huyo kumchapa fimbo machoni alimwambia ainuke na kuondoka, lakini alishindwa kutembea kwa kuwa alikuwa haoni.

Mama wa mwanafunzi huyo, Grace Sumuni, alisema baada ya kupata taarifa za mtoto wake kupata upofu baada ya kuchapwa na mwalimu, alikwenda shuleni hapo akiwa ameongozana na baba yake mzazi kisha kumchukua kwa ajili ya matibabu.

“Kwa kuwa huduma za macho zinapatikana Sumbawanga mjini, tuliamua kumkimbiza hospitali ya mkoa ambako alipokewa na kupewa kitanda hatimaye alianza kupatiwa matibabu,” alisema.

Mama huyo alisema familia haitaki kesi bali wanachohitaji ni kushirikiana na mwalimu huyo katika matibabu ya mtoto wao, ili aponea haraka na kuendelea na masomo. Pia aliwashauri walimu kuangalia maeneo ya kuwachapa wanafunzi ambayo hayatawaletea madhara makubwa.

Mhudumu wa wodi aliyolazwa mwanafunzi huyo, Marietha Mwanakatwe, alisema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri tofauti na alipofikishwa kwa kuwa amepatiwa matibabu na ametolewa bandeji iliyokuwa imefungwa usoni.

Kamanda Nyange alisema kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa ili kujibu tuhuma zitakazomkabili.
 
Huyo siyo mwalimu anaabisha taaluma ya ualimu na kudhalilisha heshima ya mwalimu kumbuka mwalimu na mwanafunz wanategemeana adhabu hiyo imepitiliza huyo mwalimu amekosa umakini jamani?
 
Eeh jaman, walimu tena?

Eeh Mungu, wanusuru Walimu. Jamii haiwapendi na haiwahitaji tena.

Jamii imekua ikipotosha ukweli na kuandika habari za upande mmoja.
 
Back
Top Bottom