Rukwa: Mume amnyonga na kumkata na shoka mkewe kwa tuhuma za kutoa mimba yake bila ruhusa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
POLISI mkoani Rukwa wanamtafuta kijana mkazi wa mtaa wa Kanisa Katoliki Manispaa ya Sumbawanga, Joseph Kalolo ‘Mwamba’ (35) kwa tuhuma za kumnyonga mkewe na kuutenganisha mwili sehemu mbili kwa shoka.

Inadaiwa kuwa baada ya ‘Mwamba’ kumuua Maria Kaozya (30), alimchukua mtoto wao akamkabidhi kwa mama mkwe wake na kisha akaenda kusikojulikana. Inadaiwa kuwa mama huyo hakujua kama ‘Mwamba’ alikuwa amemuua binti yake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo amethibitisha tukio hilo. Alieleza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa kifamilia lakini hakufafanua kwa undani.

Awali mtoaji taarifa alidai kuwa ‘Mwamba’ aliondoka nyumbani kwake akaenda mkutafuta riziki sehemu nyingine. Alikaa huko kwa zaidi ya miezi mitatu bila kuwasiliana na mkewe aliyekuwa mjamzito wakati huo.

“Mjamzito huyo aliishi kwa dhiki kubwa kwani mumewe alikata mawasiliano na hakumtumia fedha za matumizi hivyo mama huyo aliamua kuitoa mimba hiyo”alidai mtoa taarifa.

Siku chache baada ya Maria kutoa mimba, mumewe alirudi nyumbani na kumhoji alipeleka wapi ujauzito huo na alijibiwa kuwa ameitoa, kwa sababu endapo angejifungua asingemudu kumlea mtoto wao na ndipo mgogoro wa kifamilia ulipoibuka.

Kamanda Masejo alisema kuwa mauaji hayo yalitokea Agosti 9 mwaka huu saa 11 alfajiri katika Mtaa wa Kanisa Katoliki Kata ya Mafulala Manispaa ya Sumbawanga.

Alisema mtuhumiwa huyo alikimbia na kujificha kusikojulikana baada ya kufanya uhalifu huo. Alisema kuwa mtuhumiwa bado hajakamatwa na juhudi za Polisi za kumtafuta zinaendelea.

Chanzo: HabariLeo
 
RIP MARIA....bado nawaza sana huu utegemezi in the name of ndoa, kina mama amkeni mpambanie maisha yenu na watoto wenu hawa wanaume sio wa kuwategemea sana....ila mwamba umezingua ungerudi tu huko chimbo ukayasake maisha, sifa ya mwanaume ni kuhudumia
 
Nikirudi na hasira hasira nizoeee, ila bado bila bila niombeee..

Mwamba alikua ana fight watoboe usikutehuo ukimya hata simu hana, huku mkewe nae kaona zzz kakata tamaaa katoa mimba...

Umasikini mbaya sana ndugu zangu mtu unachanganyikiwa kabisa kama hvo hapo haonwote walikua wamedata

WHAT IS BETTER THAN MONEY
 
RIP MARIA....bado nawaza sana huu utegemezi in the name of ndoa, kina mama amkeni mpambanie maisha yenu na watoto wenu hawa wanaume sio wa kuwategemea sana....ila mwamba umezingua ungerudi tu huko chimbo ukayasake maisha, sifa ya mwanaume ni kuhudumia
Kama una uwezo wa kumpa mimba muwezeshe pia kiuchumi ili aweze kulea hao watoto, msitulimbikie majukumu yote kina mama, tubebe mimba, tulee familia, tutafute hela we kazi yako kuweka shahawa tu?
 
Huyo jamaa alikuwa hana uwezo tena wa kugegeda? Maana bado alikuwa na nafasi ya kutia mimba nyingine na kupata mtoto.
Hawa vijana wa miaka hii ni shiidaa..maisha yakiwabana wanahamishia hasira kwa familia zao.
Akikamatwa mniite nije nimchune ngozi ya pumbu bila ganzi.
 
Kama una uwezo wa kumpa mimba muwezeshe pia kiuchumi ili aweze kulea hao watoto, msitulimbikie majukumu yote kina mama, tubebe mimba, tulee familia, tutafute hela we kazi yako kuweka shahawa tu?
Duuuu! Kwahiyo unamaanisha kama tunaweza kuwapa mimba basi tuweze kuwapa na hela?
 
Huo ni ukatili dhidi ya wanawake. Kwanza mimba nyingi hua zinatoka zenyewe.

Huyo jamaa akamalizie maisha yake yote gerezani, atapata na muda wa kubeba mimba akiwa huko ili azae mtoto, mpuuzi huyo
 
Back
Top Bottom