Ruksa menejimenti TRL kuondoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ruksa menejimenti TRL kuondoka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Sep 21, 2009.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Na, Fidelis Butahe

  BAADA ya mvutano wa muda mrefu hatimaye serikali imesema ruksa kwa Menejimenti ya Kampuni ya Reli nchini (TRL) kuondoka.

  "Kama (TRL) hawataki, basi waondoke sina majibu mengine ya kukueleza," alisema katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu, Omari Chambo, alipoulizwa kuhusu barua ya menejimenti ya kampuni hiyo ya tishio la kuondoka kama hakutakuwa na muafaka katika muda wa siku 60.

  Tamko hilo la serikali limetolewa siku chache baada ya menejimenti ya TRL kutoa notisi ya siku 60 kushinikiza kuharakishwa kwa muafaka baina ya serikali na kampuni ya Rites ya India ambayo inamiliki asilimia 51 ya kampuni hiyo.

  Kwa mujibu wa notisi hiyo ifikapo Novemba 9, 2009 kama hakutakuwa na muafaka baina ya serikali na Rites, menejimenti itafungasha virago na kuondoka nchini.

  Serikali inamiliki asilimia 49 za hisa za TRL.

  Hatua hiyo imekuja siku chache mara baada ya Rites kuzuia injini zake 25 na mabehewa 23 kushinikiza ilipwe Sh10.4 bilioni ambazo ni gharama za kukodi vyombo hivyo.

  Uamuzi huo ulisababisha menejimenti ya TRL kuiandikia serikali notisi hiyo ya siku 60.

  Imeelezwa kuwa msukumo mwingine wa menejimenti kuandika notisi ulitokana na wafanyakazi kuamua kufufua injini 23 aina ya 8834 class na 8906 class ambazo zilianza kazi kwa kuvuta mabehewa mengi tofauti na injini za kukodi.

  Wafanyakazi hao walifikia hatua ya kufufua injini hizo pamoja na mabehewa, baada ya TRL kufuta safari tatu za treni kwenda Kigoma na Singida, huku wakitishia kusimamisha vichwa vya treni na mabehewa yaliyokodishwa.

  Chambo aliiambia Mwananchi kwa kifupi kuwa, kama menejimenti inataka kuondoka, serikali itaipa ruhusa kwa mikono miwili.

  "Hiyo notisi ni kweli tumeipata... kama hawataki basi waondoke sina majibu mengine ya kukueleza," alisema Chambo.

  Mmoja wa maofisa wa Rahco ambaye hakutaka kutajwa jina lake kwa kuwa sio msemaji, aliliambia Mwananchi kuwa notisi hiyo wanayo na kusisitiza kuwa yapo mambo mengi ambayo menejimenti ya TRL imeyawasilisha ili yafanyiwe kazi na serikali.

  "Ni kitu cha kawaida kisheria hasa katika masuala ya mikataba kama mtu unataka kufanyiwa kitu fulani ni lazima uandike notisi na kama ikishindikana hapo ndio utaweza kuchukua hatua," alisema ofisa huyo.

  "Yapo mambo mengi ambayo wameyawasilisha kwa serikali ili yatekelezwe. Hiki si kitu cha siri tena, kwa kweli vitu wanavyodai ni vingi sana."

  Mkurugenzi mtendaji wa TRL, Hundi Chaudhary alisema hana cha kuzungumza kwa kuwa masuala ya mkataba ni siri kati ya serikali na Rites.

  “Sina cha kuzungumza haya mambo ya mkataba ni siri, mimi sina cha kuzungumza” alisema Chaudhary

  Wiki iliyopita Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema serikali haitasita kuuvunja mkataba wa TRL iwapo haitafikia muafaka na mbia mwenzake katika baadhi ya vipengele vyenye utata.

  Alieleza kusikitishwa na hali ya usafiri wa reli lakini akasema serikali haiwezi kusitisha mkataba nje ya makubaliano kwani itaharibu sifa ya uwekezaji nchini.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo waliliambia gazeti hili kuwa, mgogoro uliopo hivi sasa kati ya serikali na Rites ni ulipaji wa fedha kwa wafanyakazi kabla ya Rites haijaingia ubia na serikali.
  "Unajua serikali iliingia ubia na Rites mwaka 2007, lakini kabla ya hapo wafanyakazi walikuwa wakidai fedha nyingi tu. Kwa hiyo hiyo notisi iliyoandikwa ni kwamba mwekezaji anataka fedha hizo zilipwe na serikali, halafu wafanyakazi wakishalipwa yeye atakuwa na uwezo wa kuwafukuza kazi na kuajiri upya," kilisema chanzo hicho.​

   
 2. K

  Koba JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  eti mkataba ni siri? hawa matapeli na wababaishaji upande wa serikali ya CCM matokeo yake ndio haya!
   
Loading...