- Thread starter
- #21
Kabla hawajafika kuchukua uamuzi huo wamefanya tafiti zozote? Na je wamejifunza nini kutoka DMT, KAMATA, UDA, SHIRIKA LA MELI, ATC nk
Njia za reli zitatumika kama barabara za TANROADS wanavyoweka mizani ili wenye magari mazito walipe ushuru.
Makampuni kama SIMBA CEMENT, BAKHRESA GROUP na METL Mohamed enterprise Tanzania Ltd wanauwezo wa kukarabati mabehewa chakavu 300 ya TRC au kukodisha mabehewa toka nje.
Kisha mabehewa ya kampuni binafsi kutumia njia za reli ya TRC ya mkoloni ambayo serikali ilikarabati kwa kuilipa malipo ya kutumia miundo mbinu ya reli ya TRC. Hiyo ndiyo dhana mpya shirikishi ya sekta binafsi na serikali ktk sekta ya reli.