'Ruksa' kwa watumishi wa umma kushiriki siasa

Nianze kwa kumpongeza Ndg.Myika kwa hoja nzuri na yamsingi.Kwangu mm angalizo langu,ni kwamba KUNA HAJA YA KUFANYA MABADILIKO YA SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA.PENDEKEZO LANGU NI KWAMBA WATUMISHI WAPEWE MIKATABA YA MUDA KAMA ILIVYO KWENYE SEKTA BINAFSI.

HAINGII AKILINI MTU AKIAJILIWA BASI,YAANI KAMA NI MWALIMU AFUNDISHE AU HASIFUNDISHE,MSHAHARA UKO PALEPALE.AFELISHE,HASIFELISHE CHEO CHAKE KIPO PALEPALE. NIONAVYO MM KAMA MTU AMEPEWA MKATABA WA MIAKA 4,MWISHONI TUWE NA UWEZO WA KUTATHIMINI UTENDAJI WAKE,KABLA YA KUONGEZA MKATABA MWINGINE.
 
Inachanganya sana. Waraka huu unafaa uwafikie watu wengi kwa kadiri inavyowezekana hususan watumishi wa umma. Maeneo ya vijijini hasa walimu wanakabiliana na wakati mgumu sana dhidi ya mamalaka zao za juu. Wanatishwa sana. Pengine magazeti yangesaidia kidogo lakini vyama vya siasa inafaa vichukulie hili kama ni pengo muhimu la kuliziba kwa kutoa elimu. Kwa maeneo ya vijijini walimu na watumishi wngine wa kada mbalix2 wanaaminika sana. Iwapo wataendelea kutishwa maana yake watu wengi watabaki na hisia potofu juu ya haki zao za msingi katika ushiriki wa siasa kama tulivyoona katika waraka huu wa Mnyika.
 
Mtumishi anaruhusiwa kushiriki siasa kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Umma(standing orders) 2009 kifungu cha F.20s isipokuwa kwa kuzingatia mashart yafuatayo; Hasuhusiwi 1. kufanya siasa saa zakazi. 2. Kuvaa sare za chama eneo la kz 3. Kuikosoa serikali hadharani 4. Kuajiriwa au kuwa na office ya chama wkt yeye ni mtumishi. Hayo ni baadhi.
 
Habari zenu wadau wenzangu wa JF! Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimemaliza shahada yangu ya kwanza katika Elimu katika chuo kimoja cha umma hapa nchini mwaka huu.Ndugu zangu binafsi nahusudu sana siasa na hata pale chuoni niliwahi kushika nafasi ya ubunge wa kuchaguliwa,swali langu nahitaji kufahamu,, Je endapo nitakuwa muajiriwa wa serikali naweza nikaendelea kufanya siasa hasa za vyama vya upinzani ili kutimiza ndoto zangu?.Tafadhalini naomba ushauri wenu,maana ishatokea watu wengi wanaonifahamu wananitabiria mafanikio makubwa katika siasa.
Kwa kuwa siasa ndio ajira pekee inayolipa tuambie kujipatia utajiri wa kiasi gani?
 
Habari zenu wadau wenzangu wa JF! Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimemaliza shahada yangu ya kwanza katika Elimu katika chuo kimoja cha umma hapa nchini mwaka huu.Ndugu zangu binafsi nahusudu sana siasa na hata pale chuoni niliwahi kushika nafasi ya ubunge wa kuchaguliwa,swali langu nahitaji kufahamu,, Je endapo nitakuwa muajiriwa wa serikali naweza nikaendelea kufanya siasa hasa za vyama vya upinzani ili kutimiza ndoto zangu?.Tafadhalini naomba ushauri wenu,maana ishatokea watu wengi wanaonifahamu wananitabiria mafanikio makubwa katika siasa.
Kwa kuwa siasa ndio ajira pekee inayolipa tuambie kujipatia utajiri wa kiasi gani?
 
Naomba kujua mipaka ya kushiriki siasa kwa mtumishi wa umma na namna anavyoweza kugombea nafasi za uongozi za kiasiasa bila kukiuka taratibu za utumishi....something burns inside me because I'm tired of complaining without trying to publicly speak out!
 
Huu ni mjadala mzito na wa muhimu sana haswa katika taifa letu. Kwa upande wangu naomba nitoe maoni yangu ya kwa nini tulifika hatua tuliyo fika na kwa nini tunaendelea kuwa katika hali hiyo mpaka sasa (swala la utumishi wa umma na ushiriki wa kisiasa). Ni maoni yangu tu kwa hiyo ninapo kosea naomba nirekebishwe.

Kwanza kama ulivyo ainisha hapo juu kiini cha tatizo hili ni mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu. Tanzania tulikua na utawala wa chama kimoja kwanzia 1961-1995 (miaka 34) na tumekua na mfumo w aviami vingi kwanzia 1995 mpaka sasa (miaka 17). Kwa maana hiyo tume tawaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi kwa nusu wa muda ambao tulitawaliwa ndani ya mfumo wa chama kimoja. Tuangalie sasa athari ya hili jambo katika mfumo wetu wa sasa.

Tutambua kwamba kuna kitu kinaitwa political culture (utamaduni wa kisiasa). Huu utamaduni wa kisiasa siyo lazima ulingane na sheria na utamaduni wa kisiasa hujengeka kwa muda mrefu na ni mgumu kuubadili ndani ya kazazi kimoja. Kwa hiyo tutambue kwamba japo 1995 kisheria tuliingia kwenye mfumo wa vyama vingi bado political culture ya wananchi wengi (hii inajumlisha na watumishi wa wakati huo) ilikua ya kichama kimoja. Viongozi wakuu wengi wa kisiasa na kiumma wa sasa walikua ndani ya huo mfumo na ndio maana unakuta kuna hali ya viongozi wa kisiasa wa chama tawala kujaribu kuukandamiza upinzani na pia kuna mentality kwa viongozi wakuu wa umma kwamba wanatumikia chama tawala badala ya wananchi. Ndivyo walivyo kuzwa na ndivyo wanavyo jua. Ndiyo maana mimi nina nadharia kwamba demokrasia ya kweli haitaanza kuchimbuka Tanzania mpaka kizazi cha sasa kinacho ongoza nchi kistaafu au kuondoka kabisa.

Kwa sababu mwanzo tulikua na utawala wa chama kimoja basi pia ajira na kupandishwa cheo kulitokana pia na loyalty (uaminifu) wa mtumishi kwa chama tawala. Kwa vile fikra zetu bado zipo hivyo kutokana na political culture bado kuna ile hali ya kuona kwamba mtu kufanikiwa ndani ya utumishi wa umma kuna tokana na uadilifu wako kwa chama tawala. Kwa hiyo una kuta kuna watu wanaingiza siasa kwenye utumishi wao siyo kwa sababu wana kubaliana na sera za chama tawala bali wanaona wasipo onyesha kujipendekeza kwa CCM basi hawato fika mbali kimadaraka na hatuwezi kuwalaumu hivyo kwa sababu tunaona fika watu wakipandishwa vyeo au kupewa madaraka siyo kwa sababu ya uwezo bali ushabiki.

Tatizo lingine ni kwamba kwenye utumishi wa umma kuna nafasi nyingi za kuteuliwa na raisi au waziri nk (political appointments. Yani mtu ni mtumishi wa umma lakini huteuliwa na mtu ambae anafuata ushabiki wa kichama na hii ni kuanzia wakurugenzi wizarani, makatibu wakuu, taasisi za umma nk. Sasa mtumishi yeyote anaetokana na political appointment ina maanisha kupata hiyo nafasi ni lazima awe ameonyesha uwadilifu kwa chama tawala haswa kutokana na mentality ya viongozi wakuu wa kisiasa wa sasa bado kuwa zao la chama kimoja kwa maana kwamba hata teuzi zao haziangalii zaidi uwezo bali uadilifu kwa chama tawala. Sasa kama mtu ni political appointment kwa huku kwetu ni lazima awe muadilifu siyo kwa wananchi bali aliemuweka. Ukichanganya na ukweli kwamba checks and balance Tanzania ni haipo kabisa utajua kiini cha tatizo. Pia ukweli usio pingika pia ni kwamba mtumishi wa umma akionekana kuwa neutral au kuegemea upinzani basi anaweza asifike popote kiutumishi.

Tatizo lingine ambalo lina mzizi kwenye mfumo wa utawala wa chama kimoja ni kwamba utaona japo kuna nafasi maalumu amabzo zimeainisha ambazo hazitakiwi kuhusika na siasa lakini bado watumishi hao wanatumika kisiasa. Mfano ni polisi. Polisi kikatiba hatakiwi kushiriki kwenye siasa lakini anatumiwa na serikali kwenye maswala ya kisiasa. Haya msajiri wa vyama vya siasa, viongozi wa tume ya uchaguzi, na mwanasheria mkuu wa serikali wote ni teuzi za raisi tena ana wateuwa pasipo kupitishwa na chombo chochote kingine. Sasa hawa hata wasipo kuwa wanachama wazi wa chama fulani mnategemea watamtumikia nani? Pia angali mfano mwingine, mwanasheria mkuu wa zamani (AG) Andrew Chenge alikua ni card holder wa CCM hata wakati alipo kuwa AG (nafasi ambayo haitakiwi kujihusisha na siasa). Pia unakuta mali za umma zina tumika nazo kisiasa.

Kwa hiyo wakuu mimi naona serikali yenyewe ndiyo ina sababisha tatizo hili. Kwa sababu wao wanatoa waraka zinazo limit uhusishwaji wa siasa kwa watumishi wa umma lakini serikali hiyo hiyo huwa tumia watumishi wa umma pale ambapo ina wanufaisha wao. Ni hii double standard ya chama kinacho shikilia serikali ambayo ina wachanganya watumishi wa umma. Kwa hiyo mimi nasema kabisa msitegemee unafuu wowote kwenye hili swala kwa sasa hadi hiki kizazi kilicho lelewa na kukua ndani ya mfumo wa chama kimoja kiondoke. Na siwalaumu maana hata mtu ni vigumu kumbadilisha tabia anapo fikia utu uzima. Hawa viongozi wa sasa wamelelewa tangu utotoni (kisiasa) hadi utu uzima (kisiasa) ndani ya mfumo wa chama kimoja kwa hiyo kubadilika kwa sasa ni haiwezekani.
 
Naomba kujua mipaka ya kushiriki siasa kwa mtumishi wa umma na namna anavyoweza kugombea nafasi za uongozi za kiasiasa bila kukiuka taratibu za utumishi....something burns inside me because I'm tired of complaining without trying to publicly speak out!

Sina uhakika kwa Tanzania ili kwa nchi ambazo zimekomaa kidemokrasia mtumishi wa umma akitaka kugombea nafasi ya kisiasa ni lazima ajiuzulu kwanza kwenye nafasi yake ya utumishi wa umma kabla na si baada ya kugombea. Kwa Tanzania unakuta mtu anaendelea na utumishi wa umma anagombea nafasi ya kisiasa kisha akipata ndiyo anaacha akikosa anaendelea na utumishi wake. Hii si sahihi kabisa. In fact mimi nadhani ni muhimu kuwa na time limit kati ya kujiuzulu nafasi ya umma na kugombea kwenye nafasi ya serikali ili isije mtu anajiuzulu leo kisa kesho anagombea. Kuwa na period ya walau miezi sita au mwaka mmoja kati ya mtu kujiuzulu utumishi wa umma na kugombea nafasi ya kisiasa.
 
kwa uelewa wangu nafahamu kuwa mtumishi wa umma hapaswi kujihusisha na siasa ili aweze kuwahudumia watu wote bila upendeleo lakini naona ni tofauti kwa kitila mkumbo ambaye ni mwalimu wa chuo kikuu lakini anajihusisha na siasa tena ni kiongozi wa chama kimojawapo cha siasa hapa nchini,je kwa wanafunzi ambao hawako kwenye chama chake atawatendea haki?
 
Uzuri mmoja Dk Kitila akiwa chuo huyaacha ya vyama, na akiwa jukwaani huyaacha ya chuo. Hata hivyo hayo ni maandalizi tu ya kuichukua Iramba magharibi miaka miwili ijayo. Tungependa kuona mchumi wa daraja la kwanza anaenda kuhadhiri pale udsm kama ataweza maana asahau ubunge.
 
kwa uelewa wangu nafahamu kuwa mtumishi wa umma hapaswi kujihusisha na siasa ili aweze kuwahudumia watu wote bila upendeleo lakini naona ni tofauti kwa kitila mkumbo ambaye ni mwalimu wa chuo kikuu lakini anajihusisha na siasa tena ni kiongozi wa chama kimojawapo cha siasa hapa nchini,je kwa wanafunzi ambao hawako kwenye chama chake atawatendea haki?

Nenda kajisaidie ulale mama
 
Huyu kitila hafai kabisa kwenye utumishi wa umma, kuendelea kwake kuwa mwajiriwa wa serikali huku akiwa mwanasiasa inaonyesha kabisa ana tamaa, sio mwaminifu wala mwadilifu
 
Weeee!! kwa nini usianze na wakuu wa wilaya/mikoa? polisi/mahakama na usisiemu wao? mshindwe ninyi kuyatenganisha haya, mtafute wanaofuata nyayo zenu?
 
Ndio virusi vyenyewe mana hawezi kuisaliti serikali ya chama kinachompa kula na kun..y.a....sisi waswahili tuna msemo wetu zimwi likujualo halikuli likakwisha..
 
Back
Top Bottom