Rukia Kilemile; CHADEMA wavurunda kwa Aibu London

Hii article imeandikwa na semi-illiterate? Harakati za kurudisha watanzania zilianza wakati Tony Blair (Labour Party) akiwa Prime Minister, na Mkapa akiwa rais. Na hii ilikuja baada ya kugundulika kuwa wapo watanzania walioomba ukimbizi (waliojilipua) wakijidai kuwa wao ni wasomali lakini baadae ikagundulika walikuwa watanzania. Pia kuna baadhi wanatoka upande wa Zanzibar na waliomba ukimbizi wakati wa machafuko ya Zanzibar. Pili, hali ya kudorora kwa uchumi (kwa UK) ilianza tangu 2008 wakati wa Labour Party na waziri mkuu wakati huo alikwa Gordon Brown. Conservative wamekuta mdodoro wa uchumi tayari umeshashika kasi. Lakini kama chama cha Conservative kinachukiwa sana na waingereza kama anayotaka huyu mwandhishi tuamini, nani alikiingiza madakarani? Watanzania? Kwa kumalizia, madai ya ushoga na usagaji, kama kweli hao watanzania walioko Uingereza wanaudhika sana na hayo mambo kwa nini wanakaa huko? Kwanini wasirudi nyumbani na kuandokana na 'maudhi'? Lakini ni kweli sera ya ushoga Uingereza ni ya kichama (conservative vs labour etc) au ni kitaifa zaidi? Wakati Sir, Elton John anaingia kwenye 'civil partnership' na David Furnish huko Uingereza mwaka 2005, ni chama gani kilikuwa madarakani? Tabia ya watanzania ya kutopenda kujisomea inatugharimu sana!
Nadhani tufikie mahali watanzania tupiganie sera za kimaendeleo na kuachana na marumbano ya kisiasa,watu wengi uvumilivu umewashinda na kuanza kuandika matusi kwenye hizi forum.utashangaa mtu mwenye akili timamamu anahoji(KAMA CHAMA CHA CONSERVATIVE HAKIPENDWI NA WAINGEREZA NANAI ALIKIWEKA MADARAKANI?? Haya kwa mtazamo wako chama cha mapinduzi hakipendwi na watu nani alikiweka madarakani? Tuache ushabiki wa kisiasa na tufokasi maendeleo,wakati tanzania inaamua kuanzisha mfumo wa vyama vingi ilikuwa na malengo ya kuongeza ushindani wa kuitawala na kuikosoa serikali ilyoko madarakani,tangu miaka yote hiyo hakuna chama ambacho kilipambana bila woga kukosoa maovu ya chama kilichoko madarakani ila sasa chadema imeweza kushika hatamu,tunapaswa kumshukuru mungu na kuunga mkono jitihada hizo.lakini wanachama wa chadame hawatoshi kwa chadema sasa kauli mbovu na chuki za wanachama wa chadema siku zote zinatia hofu wanachama wapya wanaopenda kujiunga na chadema.sidhani kama chama chetu kina dhamira ya kiubaguzi na kubezana miongoni mwa wanachama wa chadema na wale wasiokua wanachama,sasa utaona kila mtu akitoa wazo flani lenye chalenji kwa chadema watu wanajibu ovyo na kumtukana hivi tutafika kweli?tunapaswa kutulia kuwaelimisha walio kosea ili tupate wanachama wapya ndani ya chma chetu kitukufu.CHADEMAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunapaswa kuipongeza serikali ya uingereza kwa kurudisha wazururaji makwao. Weee ukitimulia Dar kihalali na ukaambiwa urudi kijijini kwenu kuna ubaya gani? Go East West, home is best.
 
Si mnaona alirekebisha mwaka 2007 pale pale Maarifa Tandika. Dada Hongera sana!. Siasa mchezo mchafu.........!.
0247
F
RUKIA S KILEMILE
0
IV
CIV-F HIS-F KIS-C ENG-F

Kwahiyo unampongeza kwa kujikongoja na Div. IV points 33, ndivyo mnavyofaulu huko kwenu siku hizi!!
Ndio maana nchi haipati maendeleo kama hawa failures ndio wanaoshikilia madaraka katika ofrisi za umma na nyie wapambe wao mnawapongeza kwamba wamerekebisha!! kha...
 
Kwahiyo unampongeza kwa kujikongoja na Div. IV points 33, ndivyo mnavyofaulu huko kwenu siku hizi!!
Ndio maana nchi haipati maendeleo kama hawa failures ndio wanaoshikilia madaraka katika ofrisi za umma na nyie wapambe wao mnawapongeza kwamba wamerekebisha!! kha...
Mkuu Mwita Maranya lazima anayejitahidi tumtie moyo!.

Rukia ameweza kubadilisha F ya Kisw kuwa C. Sikumpongeza kwa kufaulu bali kwa kuongeza juhudi, maana hakufaulu aliendelea

na ZERO yake wala sio IV.

Sijui ilikuwaje lakini nadhani aliunga unga na kufikia hapo alipo!. Na ningependa kumuonya kuwa kama kunasehemu alichakachua

vyeti basi ilitosha kumpatia ajira, asiendelee kuchakachua katika kazi yake maana ataharibu!.
 
ANGALIZO; Hii ni nukushi ya barua pepe ya Bi Rukia Kilemela nimeinukuu www.wavuti.com, si maneno ya Kiganyi wa JF!!

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilipata AIBU kubwa hapa jijini London baada ya Watanzania kuzira kuhudhiria mkutano wao uliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.

Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa. Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.

Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.

Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.

Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.

Katika mahudhurio hayo machache, idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja... wanafikiri hapa ni walipotoka.. ovyoo.”

Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.

Na Rukia Kilemile

rkilemile@gmail.com

Mwandishi wa kujitegea na mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United Kingdom.
Mwandishi si mwana chama wa chochote cha siasa.

My Take; Nani anamfahamu huyu mwandishi wa Ushabiki??

Source: wavuti - wavuti

Kama huyu naye anajiita kuwa ni mchambuzi wa sera za jinsi na uchumi, basi tumekwisha. Hatuna wachambuzi kama watu wanaoandika kama alivyoandika huyu, nao wanaitwa wachambuzi siku hizi. Uchambuzi bila kusoma.

Mwambieni atafute kisha asome hapa;

CHADEMA yataka kauli ya JK kuhusu ushoga

Na hapa;

Mnyika ataka kauli ya JK kuhusu ushoga

Katika hatua nyingine, CHADEMA kimemtaka Rais Jakaya Kikwete atoe tamko na msimamo wa Tanzania kuhusu hatua ya Rais Barack Obama wa Marekani kuidhinisha sheria ya ushoga nchini mwake.


Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye Kata za Mnavira na Mchauru, Jimbo la Lulindi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika alisema ukimya wa Rais Kikwete hauleti picha nzuri katika suala hilo linalopingwa na dini zote.


Kauli hiyo ya Mnyika ilifuatia swali aliloulizwa na Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF), Kijiji cha Rivango, Keneth Khamis aliyetaka kujua ukweli kuhusu taarifa zilizowasilishwa kwao, zikieleza kuwa CHADEMA inaunga mkono ushoga na usagaji, kutokana na kuwa na uhusiano na ushirikiano na chama cha Conservatives cha Uingereza.


Alisema hizo ni propaganda zilizopangwa na CCM ili CHADEMA kisikubalike katika jamii, na kusema kauli iliyowahi kutolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ikiihusisha CHADEMA na kuunga mkono ushoga ni ya unafiki.


Alisema baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuukubali ushoga na usagaji na kutaka iwe sehemu ya masharti kwa misaada inayotolewa na nchi za Magharibi, CHADEMA ilipinga na kuweka wazi kwamba haiungi mkono ‘uchafu’ huo.


Mnyika alisema kutokana na Rais Kikwete kwenda Marekani kwa lengo la kutafuta misaada, kuna dalili ya kuwepo uwezekano wa taifa hilo kupenyeza ajenda ya ushoga na ikakubaliwa na serikali kama ilivyotokea kwa Malawi.


Itakuwa vyema tukimwelewesha huyu anayejiita mchambuzi asiyekuwa mwanachama wa chama chochote! Yaani hajui hata saikolojia ya kawida sana kuwa kadri mtu anavyotaka kujitetea kwa kitu ambacho hajaulizwa wala hajatuhumiwa nacho, ndivyo anavyozidi kuwadhihirishia wenye akili kuwa ni mshirika wa tendo hilo.

Ati mchambuzi asiyekuwa na chama, so what? Kwani hoja za watu zinapimwa kwa critical thinking au kwa mtu kuwa na kadi ya chama! Pole madam analyst. Bao una safari ya mbali kushawishi watu wenye akili kuwa waweza kuwa mchambuzi wa kuaminika. Ni ajabu kweli mtu akisoma hapa hawezi kukutofautisha kabisa na wenzako. Asante kwa kujifunua nguo.

Pole ndugu mchambuzi, jaribu kusoma basi uwe mchambuzi makini uaminike.
 
Mkuu Mwita Maranya lazima anayejitahidi tumtie moyo!.

Rukia ameweza kubadilisha F ya Kisw kuwa C. Sikumpongeza kwa kufaulu bali kwa kuongeza juhudi, maana hakufaulu aliendelea

na ZERO yake wala sio IV.

Sijui ilikuwaje lakini nadhani aliunga unga na kufikia hapo alipo!. Na ningependa kumuonya kuwa kama kunasehemu alichakachua

vyeti basi ilitosha kumpatia ajira, asiendelee kuchakachua katika kazi yake maana ataharibu!.
Hata kama ameunga unga kwa pass hizo ni kilaza sana IQ yake iko chini mno.
 
CCM,
Mbona mmechanganyikiwa sana baada ya kuona Chadema wamefungua tawi UK? mbona nyie huwa mnafanya vimikutano vyenu vinavyohudhuliwa na watu watano au kumi lakini hakuna anayesema kitu.? hii ni dalili tosha kuwa mnawaogopa chadema.

Pia sioni sababu za msingi kuhusisha kampuni ya CHRIS LUKOSI na siasa. hivi ukiwa mmiliki wa kampuni huruhusiwi kuwa mwenyekiti wa chadema? Mbona Abuu faraji ana kampuni yake kama serengeti tofauti ya abuu na chris ni kwamba Serengeti ni kubwa sana na wamefanikiwa sana na abuu faraji kwa miaka yote kumi aliyo kwenye biashara ofisi yake iko kwenye kajichumba kadogo kalikokuwa gereji ya kupaki gari la mwenye nyumba.

Abuu kutwa anashinda ubalozini kujikomba na ni kada wa CCM lakini hamsemi kitu na kuhusu huduma zake kila mtu anajua jamaa ni hovyo sana ndio maana serengeti wana wateja wengi sana.

Mbona CHRIS ALIPOKUWA AKITEMBELEWA NA WABUNGE WA CCM HAMKUSEMA?????
Tunajua mnamuogopa Chris Lukosi kwa sababu mnajua ni kichwa na mnajua ni damage gani atafanya kwa CCM ndio maana mnapiga kelele.
 
Chadema walipata watu kumi.poor organation na kibaya zaidi CV ya mwenyekiti wao chris lukosi ni Utata mtupu.jipangeni upya mmefeli

akili ni mali we mjnga, je wewe mwenye CV nzuri uko wapi sasa hivi kama si kuishi chini ya dola 1 kwa siku na kupiga porojo za kike humu JF!
Ujinga hauna kikomo leo nimeamini na tabia yako ya kufikiria kwa kutumia ugoro na tambaku sasa haya ndiyo madhara yake.
 
IMG_4298.JPG


Si mwanzo mbaya kwa wenye uzoefu wa siasa.
 
national examinations council of tanzania

csee 2005 examination results


s0829 maarifa tandika secondary school


div-i = 0 div-ii = 1 div-iii= 14 div-iv = 69 fail= 28


0040
f rukia s kilemile
35 fld civ-f his-f geo-f eli-f kis-f eng-f bio-f bas-f

source:
http://www.tanzania.go.tz/NectaResults2005/S0829.HTM


umejitahidi na pro chadema kama kawaida wakakumwagia like ! lakini mwandishi wa thread kasema huyu dada anaitwa Rukia Kilemela sasa aliyekurupuka sijui weye au mleta thread ..
 
Hii article imeandikwa na semi-illiterate?

Harakati za kurudisha watanzania zilianza wakati Tony Blair (Labour Party) akiwa Prime Minister, na Mkapa akiwa rais. Na hii ilikuja baada ya kugundulika kuwa wapo watanzania walioomba ukimbizi (waliojilipua) wakijidai kuwa wao ni wasomali lakini baadae ikagundulika walikuwa watanzania. Pia kuna baadhi wanatoka upande wa Zanzibar na waliomba ukimbizi wakati wa machafuko ya Zanzibar.

Pili, hali ya kudorora kwa uchumi (kwa UK) ilianza tangu 2008 wakati wa Labour Party na waziri mkuu wakati huo alikwa Gordon Brown. Conservative wamekuta mdodoro wa uchumi tayari umeshashika kasi. Lakini kama chama cha Conservative kinachukiwa sana na waingereza kama anayotaka huyu mwandhishi tuamini, nani alikiingiza madakarani? Watanzania?

Kwa kumalizia, madai ya ushoga na usagaji, kama kweli hao watanzania walioko Uingereza wanaudhika sana na hayo mambo kwa nini wanakaa huko? Kwanini wasirudi nyumbani na kuandokana na 'maudhi'? Lakini ni kweli sera ya ushoga Uingereza ni ya kichama (conservative vs labour etc) au ni kitaifa zaidi? Wakati Sir, Elton John anaingia kwenye 'civil partnership' na David Furnish huko Uingereza mwaka 2005, ni chama gani kilikuwa madarakani?

Tabia ya watanzania ya kutopenda kujisomea inatugharimu sana!

Umechambua vizuri sana. Thank you very much. Wanaong'ang'ania kukaa UK huku wakikitukuza CCM kamani kweli ni wanafiki au labda wanishi kwa kupewa fedha za EPA! Wao wakae tu sisi huku tunaendelea kuvua magamba na kuvaa magwanda. Kazi kwao
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nobody is perfect kukosea ni jambo la kawaida. Kama CDM wamefanya makosa huko UK tatizo ni nini si watajirekebisha tu? Ifakara nako je msiopenda mafanikio ya CDM mnasmaje?
 
mwandishi wa kujitegemea hata picha moja ya kutuonesha madhari ya mkutano ulivyokuwa hakuna!!! mwandishi au mwandikiwa?
Hao ni watoto wa vigogo wa CCM wapo nje kwa gharama za kodi za walala hoi wanaona CDM ikichukua nchi watarudishwa bongo.
 
All the same tumepata the other side of the coin. Ni ngumu sana mtu anapoona ananyanganywa tonge mdomoni lazima atatapambana kufa na kupona. CDM walichofanya wana CDM tumeridhika yeye aendelee kubwabwaja sisi macho yetu 2015.
Mleta uzi kafanya kazi nzuri tusimlaumu.
 
Back
Top Bottom