Rukia Kilemile; CHADEMA wavurunda kwa Aibu London

Mbona wewe ndio umekurupuka kuanza kutoa mialiko kwa watu na kuwalaumu wengine kabla hujasoma vizuri thread.

Ha ha ha Siku hizi Aanahisi amepwaya Kila akiona Nondo za CDM lazima amwalike chama Bwaha bwaha bwaha
 
Last edited by a moderator:
Ritz
Hivi inakuwaje kwa Mtanzania Unayeishi Uingereza Unalaumu Sera ya Ushoga ya Uingereza halafu Bado unang'ang'ania Kuishi Uingereza tena kwa Njia za Panya? Lazima uwe shoga unless Ungeonesha kukataa kwa

1. Kuondoka Katika Hiyo Nchi
2. Kuonyesha Kuchukizwa na Serikali ya CCM Kuendelea Kupokea Misaada Under Conditions za Cameroon

Kama Hufanyi Moja kati ya Hayo na Wewe ni WAREWARE tu
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama mtu mjinga hivi yuko Uingereza!! Amesoma wapi huyu?!

Tuujadili usahihi au la wa ujumbe na tusimjadili mjumbe. Ni kweli kwamba jamaa kagonga mwamba? Mbona hatujaonyeshwa picha za mkutano huo kinyume na tabia ya magwanda? Jamaa kaangukia pua, alidhani pale ni Unga Limited!
 
Siwapati vizuri baadhi ya wachangiaji Kiganyi kawawekea mezani Rukia Kilemile mumdadavue lakini mnamrukia bila kusoma post nzima. Obviously muandishi ni pro magamba kazi kwetu kumshushua na uandishi wake shalo shalo
 
Last edited by a moderator:
Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.

Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.

Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.

Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.

Katika mahudhurio hayo machache, idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja... wanafikiri hapa ni walipotoka.. ovyoo.”

Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.

Na Rukia Kilemile

rkilemile@gmail.com

Mwandishi wa kujitegea na mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United Kingdom.
Mwandishi si mwana chama wa chochote cha siasa.

My Take; Nani anamfahamu huyu mwandishi wa Ushabiki??

Source: wavuti - wavuti
[/QUOTE]

Rukia unawakilisha aina ya Watanzania wengi sana ambao wanaishi Uk,kwanza kwa mtazamo wa kawaida sana,haimpi shida mtu aliye elimika hata kidogo tu,kujua kua uwezo wako wa uchambuzi wa mambo ni mdogo sana kutokana na uandishi wako huu,napata shaka kama wewe ndio mmoja wa wachambuzi wa mambo ya jinsia na uchumi,basi taifa letu linaelekea kukosa wachambuzi,juu juu tu nimegundua wewe una chuki za wazi na Serengeti Freight nadhani labda kwa kua ni kampuni inayomilikiwa na Watanzania waliojipgania kifikra mpaka kuanzisha kitu kama iko,kwa hiyo hapo ni wivu na uvivu ndin umekusuma kuichukia Serengeti,hiyo ndio hulka ya Watanzania wengi waishio Uk,ni wivu,fitina na majungu ndicho wanachopenda kumfanyia yule aliyefanikiwa,tuko tofauti sana na majirani zetu Wakenya ambao wao wanajua nini walikuja kufanya huko,pili una chuki na serikali ya conservative kwa kua wewe ni mmoja ya wale Watanzania waliokimbilia Uk alafu haukujua unakwenda kufanya nini,ukaishia kwenye home cares,warehouses au u kitche porter,so umekuja kustuka late kua umepoteza uhalali wa kuish Uk unabaki kutupa lawama kwa conservative kua wanafukuza wageni,elewa hiyo ni nchi ya Waingereza inayoendeshwa kwa sheria zao kwa manufaa ya wananchi wao,hakuma nchi duniani siku hz inayokumbatia illegal immigrants kama wewe,usiwasemehe Waingereza juu ya conservative wakati hatuwasikii wao kulalamika,kama kuanguka kwa uchumi,ni dunia nzima uchumi ulianguka!hv unajua kilicho waondoa labour madarakani??na mambo ya kudeport illegal immigrant kama wewe unadhani yameanza kipindi hiki cha conservative?labda uwe mgeni na nchi zilizoendelea ndio unaweza kuanika utumbo kama uliouanika hapa!unasema sera za ushoga na usagaji za ni za cnsvrtv,unajua ushoga na usagaji ulianza lini Uk?upeo wako ni mdogo sana wewe,rudi nyumbani upate hata elimu ya watu wazma,haujachelewa najua huko huwezi pata elimu,utaishia kufanya kazi za ajabu bila kuelimika,tatizo wengi wenu bado mna mawazo kua Watanzania ni wale wale mliowaacha,matokeo yake mkiwa deported mnaishia kuaibika na kua frastuated,Tanzania vyuo ni vingi sana sasa hv,na fee ni affordable,rudi nyumbani Rukia,mimi nimesoma huko for 4 yearz,maisha ya Watanzania wengi huko ni yasiyo na matumaini kabisa mbeleni,tofauti na wengi tunavyofikiria kua mnaishi kwa asali na maziwa!na kwa taarifa yako Chadema huku nyumbani ndio chama kinachopendwa zaidi na wasomi na hata vijana kwa kua wame elimika,no wonder umeandika utumbo huu,ni ukosefu wa elimu na hata fikra kidogo ndio umekusukuma
 
Mkuu FJM maelezo yako yako very clear.
Tangu maandalizi ya uzinduzi wa tawi hilo yaanze wanamagamba kwa ushirikiano mkubwa na wanamagamba b wamekuwa wakimbwela mbwela hapa JF na kila aina ya propaganda.
Mimi nasema hata kama walikuwa 15 bado ni mafanikio makubwa kwani kila kitu ni hatua.
Mwaka jana 2011 mwezi wa saba nilianzisha tawi la Chadema hapa Ukonga na wanachama 19 lakini hadi mwezi wa nne mwaka huu tawi hilo lilikuwa na wanachama 116. Jambo la muhimu ni viongozi pamoja na wanachama wenzao kufanya kazi zao kikamilifu na kujituma watu wataongezeka tu as long wana mahali (ofisi) pa kuwapata.
 
Last edited by a moderator:
Chadema walipata watu kumi.poor organation na kibaya zaidi CV ya mwenyekiti wao chris lukosi ni Utata mtupu.jipangeni upya mmefeli
 
Chadema walipata watu kumi.poor organation na kibaya zaidi CV ya mwenyekiti wao chris lukosi ni Utata mtupu.jipangeni upya mmefeli

Mbona wewe umeng'ang'ania Cv ya Lukosi?wewe Cv yako ikoje?ni wazi uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo sana!Lukosi kwa kushirikiana na Watanzania wenzake kama Richard ameweza kuanzisha kampuni tena katika nchi iliyoendelea na isiyo na magumashi,ametoa ajira na amejiajiri pia,wewe hauoni kama huyu mtu iq yake ni kubwa na cv yake inastahiki?in life hata ukiwa na phd alafu ukashndwa kutransform hiyo phd ikusaidie wewe na iwasaidie inakua haina maana na ni wazi kua unakua umeji prove failure,elimu za vyeti tu,elimu ni zaidi ya makaratasi tunayokabidhiwa vyuoni!jaribu kushirikisha ubongo wako katika kufikiri!usiendeshwa na ukariri
 
Hivi utamaduni wa kujadili waleta hoja badala ya hoja yenyewe ndio trend mpya JF au ni upepo tu ambao utapita?
 
Tuujadili usahihi au la wa ujumbe na tusimjadili mjumbe. Ni kweli kwamba jamaa kagonga mwamba? Mbona hatujaonyeshwa picha za mkutano huo kinyume na tabia ya magwanda? Jamaa kaangukia pua, alidhani pale ni Unga Limited!

Aisee umenichekesha sana mnyalukolo!!! hahahahahahahahahahahahaha
 
ANGALIZO; Hii ni nukushi ya barua pepe ya Bi Rukia Kilemela nimeinukuu wavuti - wavuti, si maneno ya Kiganyi wa JF!!Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana kilipata AIBU kubwa hapa jijini London baada ya Watanzania kuzira kuhudhiria mkutano wao uliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa. Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.Katika mahudhurio hayo machache, idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja... wanafikiri hapa ni walipotoka.. ovyoo.”Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.Na Rukia Kilemile rkilemile@gmail.comMwandishi wa kujitegea na mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United Kingdom.Mwandishi si mwana chama wa chochote cha siasa.My Take; Nani anamfahamu huyu mwandishi wa Ushabiki??
Source: wavuti - wavuti
Mbona jicho la tatu linamwona wazi kuwa mwandishi huyu ni gamba.Wewe ni sawa na Alsahaf aliyekuwa waziri wa Iraq wakati wa Sadam,wkt ukijaribu kutukatisha tamaaSisi tunakaza mwendo.
 
Chadema walipata watu kumi.poor organation na kibaya zaidi CV ya mwenyekiti wao chris lukosi ni Utata mtupu.jipangeni upya mmefeli

Nimegundua kwamba wale waliojilipua na ambao wamekuwa wakipata unafuu wa kupata japo mlo mzuri wakati wa hafla za ccm ndio wanapiga kelele hapa.
Kwani watu kumi unaona ni wachache? Unadhani kama hawatoshi kuwatisha ccm kwanini mnahangaika kuwapondea?
Watu wako UK wameanzisha makampuni yao na kutoa ajira halafu wewe unabaki kuropoka kama mlevi wa mataputapu!
 
Magamba na propaganda za mwisho mwisho kabla ya kukizika mapema baada ya uchaguzi uvccm.
 
No comment.. Mzee Mwanakijiji jibu barua ingine hiyo mkuu chama mambo yameiva Uingereza, mkuu wangu Mkandara tunaomba mawazo yako.
Hizi ni siasa ambazo siwezi kuchangia maana zimeandikwa kishabiki zaidi..Kama swala lingekuwa lile lile walioomba mkutano huu uahirishwe muda na venue kwa sababu ya mfungo wa Ramadhan, ningekuwa nao lakini haya ya Conservative kusema kweli sioni umuhimu wake kwangu. Mbona hao Liberal na PM wao Blair ndio waliotuuzia rada na tukapigwa kanyanga, ndio walomchagua Mkapa kuwa mwenyekiti msaidizi wa baraza la kuchungua Corruption nchi maskini.. Ati Mkapa ndiye hakimu wa rushwa! Kama isingekuwa mbunge wa Conservative tusingeyajua haya.

Hawa watu wenyewe wakimbizi UK, halafu wanaitaka haki ya wakati wao sio wakimbizi bali wahamiaji tu, na hawataki kufuata sheria za uhamiaji isipokuwa kwa njia za kona. Maisha ni magumu UK na dunia yote, sii kwa sababu ya Uhafidhina isipokuwa ni hali halisi ya uchumi wa UK ndio hivyo unaporomoka. Walizoea sana kuendeleza uchumi wao kwa kutumia makoloni sasa duru limepinduka mataifa yote makubwa yanalazimisha kutafuta vibaraka nchi maskini ama kuwekeza China kwenye viwanda na cheap labour..

Swali na kujiuliza ni Je, kuna mpango gani Chadema wakuuza nchi kwa Muingereza?.. JK kesha uza kwa Marekani na tayari Africom wameingia nchini kututawala kiuchumi. Tumeuza koloni wenyewe kjwa Mmarekani hivyo tutegemee ya haiti ilikuwa na Marekani kwa miaka 200 lakini bado maskini maana hawa ni wajinga na maskini kama sisi..Maswala ya Usenge, kwetu sisi hayana itikadi ni swala la mila na utamaduni ambao aidha kuna watu hanaupenda na wengine hawaupendi kutokana na sababu nje kabisa ya siasa ama itikadi za vyama.

Na ndio maana nawaomba sana Watanzania wawe makini na hii Liberalism maana unaweza jikuta wewe ni Conservative kuliko huyo Cameroon wa Uingereza, ama liberal wa ukaunga mkono Ushoga. Conservative wa sehemu nyingine hawaruhusu kabisa ushoga acha mbali ndoa za mashoga kwa sababu wanaenzi mila na utamaduni ulounda taifa lao. Cameron ni Conservative legelege, pengine hawa Anglican wanaunga mkono ushoga hivyo ndio maana naye kalegea. lakini sioni kabisa mahusiano ya watu kutohudhuria makutano haya kwa sababu zilizowekwa..
 
Mimi ninavyomjua Lema bado sana anauwezo mdogo sana Sasa ikifika kwenye kutoa maamuzi ya haraka ndo kabisaa hamna kitu.Elimu ndugu zangu muhimu sana alivyopigwa chini Arusha akakurupuka sitakata rufaa bila hata kufikiria lakini kilicho fuata kila mtu anajua mbowe alifanya uamuzi gani kwa huyu bwana mdogo.Na ndio anayempandisha ndege hadi huko ili asije akajinyonga na siasa
 
Mkuu Ritz ngoja nimwite na chama Nina Maswali Mawili

1. Serikali ya Cameroon Ilitangaza Masharti ya Misaada ikiwa ni Nchi Kama Inahitaji Misaada ni Lazima ikubali kuheshimu Haki za Msahoga

Sasa

a. Cameroon hajawahi kubatilisha Kauli yake na Wakati huo huo Mkuu wa Kaya mara kwa Mara amekuwa akikwea Pipa kwenda Kwa Cameroon kuomba Misaada

Je

Serikali kupitia kwa Mkuu wa Nchi Imekubali Masharti ya Cameroon?

Naomba Majibu Mkuu

Albedo;
Unajua wengi wa pro Chadema ni watu mnaokurupuka bila kuja undani wa tatizo lenyewe, tamko la Cameroon lilikuwa na lengo la kutafuta namna na kumbana Raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe, binafsi nimeyashuhudia Harare jinsi gani Mugabe anavyopiga vita ushoga si vitu vya kusoma kwenye magazeti; tamko la Cameron halikuwa tamko rasmi la serikali ya uingereza na isitoshe viongozi wa nchi Afrika ikiwemo Tanzania walimueleza wazi kama ni misaada na akae nayo hawako tayari kushurutishwa kwenye kinyume na tamaduni za nchi zao; Mh. Raisi anapokwenda Uingereza anakwenda kwa mialiko ya mashirika mbalimbali ya kimataifa na si kila anapokwenda anakwenda kwa mualiko wa serikali ya uingereza; katika masuala ya uchumi ni kweli Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji msaada kutoka Uingereza hali kadhalika Uingereza inahitaji ushirikiana na Tanzania kwa maendeleo yake; unafikiri makampuni ya uingereza yaliyopo Tanzania yanakuja tu? Ni sababu ya ushirikiano wa kiuchumi kati yetu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom