Rukia Bruno hatunae tena

BadoNipo

Senior Member
Jul 4, 2008
170
28
Source - Michuzi-blog.com


MNENGUAJI maarufu wa Bendi ya FM Academia, Rukia Bruno amefariki jana mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam .

Balozi Credo aliyejitambulisha kama kaka wa Mwanamuziki Nyoshi el Saadat ambaye mkewe amefariki, amsema shemeji yake alikuwa Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kujifungua mtoto aliyefariki wiki moja iliyopita na kuzikwa hospitalini hapo.

"Habari za msiba za Bruno ni kweli na upo Sinza nyumbani kwa Nyoshi ambako familia ya marehemu ipo katika kikao cha kupanga siku ya maziko ya marehemu yatakayofanyika siku yoyote kuanzia sasa," alisema Credo.

Aidha, Bruno alisema hafahamu chanzo umauti wa Rukia ambaye ameacha mume na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Stallone.

Kabla ya kuwa bendi ya FM Academia mnenguaji huyo alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, Bendi ya Tamutamu ambazo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuwapa burudani mashabiki.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi - Amina
 
Back
Top Bottom