Rugemalira, Luoga, escrow funds na Mkombozi Commercial Bank

Kwa mwendo huu wa ss utauza kwa hasara maana kama ni nchi makini ingeweza kusimamisha kabisa operation ya Mkombozi Bank.
Banki Ambrosiano ikilala chali ulikuwa umezaliwa? Fuatilia ilimilikiwa na nani na ilikufajye. Ukishapata hayo linganisha na Banki Mkombozi.
 
Usiwe mkali mpaka ilipofika Bank yetu imeshachafuka sana, ianze kujisafisha kwa kuwaonfoa wote waliohusika kwenye sakata hili.

Mimi ni MKATOLIKI Sikubaliani na board member kuwa fusadi, mwizi wa mali za umma, mawili aachie ngazi mwenyewe ay apigwe chini.

Umeshapewa link ya Mkombozi Board Members (Board of Directors | Mkombozi Commercial Bank Plc). Huyo fisadi katika board members ni nani ebu tuambie?
 
Wanajamii tunahatarisha maisha yetu kuwaletea musiyoyajua katika kasha hii ya Tegeta Escrow. Ni wajibu wetu kufichua mauvo yanayofanywa na viongozi wetu wakishirikiana na wapiga diliwa kimataifa ' Fixers' kama kina James Rugemalira.

Wiki iliyopita kuna thread ilianzishwa hapa JF ikawatahadharisha wananchi kutonunua hisa za Mkombozi Commercial Bank kwakua Ghost Owner wa benki hiyo ni mmoja wa watuhumiwa katika kashfa ya Escrow. Mtu huyo si mwingine bali ni James Rugemalira.Ni ukweli usiopingika kuwa Mkombozi Bank inatumika na James Rugemalira katika biashara zake za kitapeli chini ya mwavuli wa Kanika Katoliki.

PLACIDIUS LUOGA NI NANI?

Mnamo tarehe 2.5.2014 siku ya Ijumaa majira ya saa sita mchana kiasi cha shilingi MILIONI 121.2 za Kitanzania (121,200,000) kilihamishwa kutoka Account No: 00120102523901 ya MKOMBOZI BANK ( Akaunti hii inamlikiwa na JAMES LUGEMALIRA) kwenda Account No: 00120100022801 ya benki hiyo hiyo ya MKOMBOZI BANK inayomalikiwa na Bwana PLACIDIUS LUOGA.

Swali huyu Bwana Placidius Luoga ni nani haswa?

Bwana Placidius Luoga ni Kamishna Msaidizi wa TRA ( Deputy Commissioner General TRA) amezaliwa tarehe 7January 1954. Ana Masters of Science in Tax Administration.Uchunguzi niliofanya kwa msaada wa watu wangu wa karibu ndani ya MKOMBOZI BANK inasema mnamo tarehe 18 August 2009 Kamishna huyu msaidizi wa TRA aliteuliwa kuwa Mkurugenzi katika Benki Hiyo ambayo inafanya kazi chini ya mwavuli wa Kanisa Katoliki.

Wengine katika mgao huo pamoja na nyadhifa zao ndani ya Mkombozi Commercial Bank ni hawa wafuatao.


S/NNAMELOCATIONPOSITIONAMOUNT (TZS)
1Rweyongeza ALfred BitungwaDar Es SalaamShareholder40.2Million
2Bishop Methodius KilainiBukobaBoard Member80Million
3Placidius LuogaDar Es SalaamDirector121.2 Million






Acha uzushi wewe. Board Members wa Mkombozi tunaowajua ni hawa:

directors21.jpg
 
kwenye taarifa ya kuzaliwa inaonyesha wazi atakuwa kashafikisha miaka sitini. hoja yako ina mashiko kwa mbaaali
 
Kajipange halafu uje tena…Placidus Luoga hayuko katika TRA tena….kesha staafu..leta umbea unaolingana na ukweli walao

Nawe umejitahidi kuwajibika kachukue malipo yako kwa kazi nzuri. Mtoa thread anaeleza status ya Luoga wakati deal linafanywa sio jana
 
Naambiwa james Rugemalira ni jinamizi (dummy name), hamna mtu kama huyo; na PAP ni kampuni ya ki-Tz na sio singasinga! Wajanja kama wale wa EPA, hiyo ndiyo serikali ya cdm!
 
Kaka as long as ni BANK YA DINI ilitakiwa iwe kwenye MAADILI ya hali ya juu.Haitakiwi kuwa na shareholders ambao ni mafisadi nor board directors.

Tusikwepe ukweli,tutende kinachotakiwa kutendwa,uadilifu wa kanisa uko wapi?

Ndg,

Hujui kuwa wezi wakubwa, mafisadi wakubwa na hata wauaji wakubwa hupenda sana kutumia kanisa kama mwavuli wa kuficha uovu wao?
 
naona mlivyo wehu mmesahau hata wizi unaotutesa wote kwa kukosa huduma za kijamii kama vile dawa kisa kanisa katoliki limeguswa. kwa taarifa yenu maovu mengi ya dunia hii yanapitia huko. wala msipate shida kwenye hii ishu kulitetea. acheni kujitoa fahamu tuipiganie nchi yetu. hilo kanisa halikuendeshi bali nyinyi ndo mnaliendesha kwa sadaka na michango mbalimbali yenu. bila sadaka zenu hakuna hilo kanisa.
tunajua ishu hii imewagonga penyewe. lakini vumilie tu hakuna jinsi.


Kajipange halafu uje tena…Placidus Luoga hayuko katika TRA tena….kesha staafu..leta umbea unaolingana na ukweli walao

Story yako ipo kama picha la UKIMWI, ambapo sterling ndio huwa anakufa! Nimeipenda sana mkuu.......sasa sijui itaendelea wiki ijayo mida kama hii ikiwa na sterling mwingine?

Mwandishi unakimbizwa .......... Kama vile unaandika umejificha kwenye andaki

Acha kupotosha umma we kilaza. Kama una chuki binafsi na benki ya mkombozi funguka na siyo kuendekeza uongo mchana kweupe. Wewe unadhani benki wanapokea pesa kama wanauza nyanya mpuuzi wewe. Hujui kama benki zinaendeshwa kwa taratibu na sheria.
Hivi unajisikiaje unapodanganya umma kuwa hao ni board members wa Mkombozi? Kwa kukusaidia ingia kwenye website ya Mkombozi ujiridhishe na hicho unachosema. Soma hapa -Board of Directors

mimi sio mkatoliki ila kuna watu wana ajenda binafsi na hili kanisa sasa wanataka kutumia hii skendo kutekeleza malengo yao
 
!

Leo tarehe 22 November 2014, huyo Luoga ni mkurugenzi wa benki ya Mkombozi?
wewe mpumbavu kwani wizi wa escrow umefanyika leo? tumia akili zako acha kuburuzwa kisa kanisa. jiulize ni lini hilo kanisa limekuletea chakula zaidi ya wewe kulipelekea sadaka? bila sadaka yako hakuna kanisa. wenzenu ulaya wameyapuuza kweli kweli siku hizi. mmebaki nyie wakuletewa tu.
 
Kwanza niseme mimi ni mkatoliki mzuri sana kiongozi katika level za chini lakini pia msomi KIASI wa chu o kikuu.Ni aibu kubwa sana kwa benki ya kanisa kuingia katika kashfa ya aina hii.nnaamini wameskia kuwa kwa namna flani wamehusika na wizi huu wa iptl,kama hawahusiki wangecome out na kusema lakini wakikaa kimya wanatupruvia kuwa wanahusika.pili hata kama walikuwa hawajui hela za bw rugemalila zilikuwa za 'wizi' haiwafanyi kutokuwa na kosa...kuna kitu wanaita knwo your customer kyc...leo hii mimi mfanyakazi ninaelipwa milioni moja kwa mwezi ktk account yangu...ikitokea account yangu nikaingiIwa bilioni moja... Wanapaswa kuwa flaged na kufuatilia...know your customer aka kyc ni kitu muhimu...katika nchi zilizoendelea bank inalipa billions of fines...mwisho kama kanisa langu katoliki ninasikitishwa kama watakaa kimya sababu walituhimiza kununua hisa za bank yetu kama hawatalishughulikia hili kwa ueledi wataharibu reputation ya kanisa.
 
Jamani acheni ubishi kununua hisa za mkombozi kwa sasa ni kujitia umaskini . watu watakumbuka kwamba wakati wa hisa za tz oxygeni, precission air waliambiwa wakabisha leo hii mtu anahangaika kuuza hisa zake za precission haziuziki na wanao uza wanauza kwa hasara.

Hata kama rugemalila sio board of directors lakini akawa na hisa nyingi tayari anakuwa na kura nyingi ya maamuzi . tuwe makini dalili za mvua ni mawingu hata watu wa DEC waliambiwa hivyo hivyo wakapinga
 
So kilaini ni board member wa mkombozi.
dah...!!

Nazidi kupata wasiwasi. Kilaini ni rafiki mkubwa wa familia ya mkuu wa Kaya. Ni kama alivyo na Membe. Si mnakumbuka ile ishu ya 'Chaguo la Mungu'?
Kwa urafiki wake na wanasiasa ilimfanya akatimuliwa kwenye ofisi ya Jimbo kuu, na kuondolewa kwenye orodha ya Makadinari watarajiwa na orodha ya kurithi kiti cha Pengo.
Ndio maana hata rangi ya kanzu yake imebadilika sasa. Lakini kwa kifupi kufanya kwake siasa kupitia kabisa kwa kumsaidia rafiki yake ilimfanya ashuke kw kiwango hicho.
Sasa napata wasiwasi kwa kupewa mgao huo hasa kwa wakati huu ambao mkuu wa kaya yuko kwenye mwaka wa mwisho, naona kama kuna dalili za mkuu wa nyumba nyeupe kuwa miongoni mwao. Ngoja tuone, wakati utazungumza.
Ova
 
Angeulizwa kwanza aseme huo mgawo ulikuwa wa nini. At least Tiba alisema ni kwa ajili ya shule. Yeye ilikuwa ni kwa ajili gani wakati hana mke wala vitegemezi?

Sidhani kama KANISA tunahitaji pesa za wizi.Alikuwa hana haki ya kuzichukua,sababu kama kiongozi wa kanisa alitakiwa kuonyesha mfano.Je , baada ya hili unadhani kanisa watakuwa na ubavu wa kulisemea hili la ESCROW?

Bank ya Kanisa imepokea pesa,na Kiongozi wa Kanisa,ni aibu kwa Kanisa letu.
 
Benki inachafuliwa na wajinga wasiojua sheria za benki na namna benki zinavyoendeshwa. Halafu hao wote alio wataja sio board members wa Mkombozi Bank ndio maana nimemwambia asome website ya Mkombozi ajiridhishe na hicho alichokiandika.

Issue walikuwa na ndiyo maana board iliamua kuwaondoa,inawezekana baada ya skendo kuibuliwa.
 
Back
Top Bottom