Rugemalila atoa notisi kwa taasisi 6 akiomba aondolewe kwenye kesi ya Uhujumu Uchumi

KITAULO

JF-Expert Member
Apr 27, 2018
1,926
2,777
Mfanyabiashara James Rugemalila, ametoa notisi kwa taasisi tisa, ikiwemo Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Gavana wa Benki Kuu, DCI, TRA, Wakili Mkuu wa Serikali, Kamishna wa Magereza pamoja na kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini akiomba amtoe kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili.
Rugemalira-1-600x357.jpg

Rugemalila ameyabainisha hayo leo Februari 13, 2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa ajili ya kutajwa na kusema kuwa asipofanya hivyo atawasilisha hoja rasmi za kuondolewa katika kesi hiyo Mahakamani. ambapo upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Wankyo Simon alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya Wakili Wankyo kusema hivyo Rugemalila alinyoosha mkono akiomba kuzungumza na aliporuhusiwa alidai kuwa notisi alizoziandika na kuzituma zote zimepokelewa sehemu husika na hivyo alitarajiwa leo kuachiwa na kuondolewa katika shauri hilo.

“Nilitegemea leo Jamhuri waje na ufafanuzi juu ya barua niliyoandika kuhusu Benki ya Standard Chartered kukwepa kodi, sheria haitekelezwi, jana nimetoa notisi na kuisambaza na imepokelewa kote,” amesema Rugemalila.

Rugemalira pamoja na mmiliki mwenza wa zamani wa kampuni ya IPTL, Harbinder Sethi, wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwemo utakatishaji wa fedha, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, utakatishaji wa fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27 za Tanzania, makosa ambayo wanadaiwa kuyatenda jijini Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

JE NI KWELI BABU ANAUBAVU WA KUTOA NOTICE KWA VYOMBO NYETI VYA SERIKALI ????

UPDATES TAREHE 27/02/2020

https://millardayo.com/mahakama-imepokea-maombi-ya-rugemalira-kutaka-aondolewe-katika-kesi/#respond

1-1-1-660x400.jpg


Leo February 27, 2020 Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu imekubali kupokea hoja za maombi ya mfanyabiashara James Rugemalira anayetaka kuondolewa kwenye kesi ya utakatishaji fedha wa Sh. Bil 309.4.

Hatua hiyo inakuja wakati shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili y kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa utetezi, John Chuma amedai kuwa mteja wake ameshawasilisha hoja za pingamizi la awali lakini hajapata majibu yoyote kutoka upande wa Jamuhuri.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai baadhi ya nyaraka amezipata leo mahakamani hapo na kuwa upande wa Jamhuri upo tayari kusikiliza hoja hizo kwa njia ya mdomo kama nyaraka hizo zimeshaingizwa kwenye kumbukumbu ya mahakama hata kwa wakati huo kama ratiba ingeruhusu.

Wankyo amedai mshtakiwa wa pili amekua anajiwasilisha mwenyewe huku akiwa na uwakilishi wa mawakili hivyo anapaswa kusema kama amewaacha ama wanaendelea.

Akijibu suala hilo, Rugemarila amedai kuwa amekua na wawakilishi hata zaidi ya thelasini lakini kuna hoja lazima aziwasilishe mwenyewe na kuwa hilo jambo walitakiwa kulalamika mawakili wake na sio yeye kwani sheria inamruhusu kujiwakilisha.

Baada ya hoja hizo, Hakimu Shaidi Shaidi ameahirisha shauri hilo hadi Machi 12, 2020 litakuja kutajwa na upande wa jamuhuri kuwasilisha majibu.

Mbali na Rugemalira, washitakiwa wengine ni Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power (IPTL) na Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege.

Makandege anadaiwa kuwa, kati ya Oktoba 18, 2011 na Machi 19, 2014 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, Kenya, Afrika Kusini na India, akiwa na wenzake walikula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Pia anadaiwa kuongoza genge la uhalifu, katika nchi hizo, akiwa si mtumishi wa Serikali akishirikiana na watumishi wa umma kwa kuratibu na kufadhili mpango wa uhalifu.

Katika mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Makandege anadaiwa kuwa kati ya Januari 23, 2014 na Februari 2014, alijipatia dola 380,000 katika benki ya Stanbic iliyopo Kinondoni na dola 600,000 katika benki ya UBL Bank(T) Ltd iliyopo wilaya ya Ilala, fedha zilizotoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa nyakati tofauti.

Washitakiwa Seth na Rugemalira kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27 kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo Juni 19, 2017.

 
Huyu mzee anazidi kujiharibia. Akitaka kufuata sheria watafia ndani. Walishapewa nafasi,wangeitumia ile nafasi. Kama bado ipo washaurini waitumie. Hiki sio kipindi kizuri kwake cha kupambana kisheria. Aandike barua ya kulipa kile kinachowezekana ili asamehewe.

Fikiria kama anamiliki mfano trillions 3 (ambazo najua anamiliki zaidi ya hizo). Labda Wamemwambia alipe trillion 1.7 hivi. Kwa nini uzing'ang'anie huku ukiendelea kuteseka?.

Kwanza umri umemtupa mkono,hizo atakazobaki nazo pamoja na miradi yake mingine ataishi anakula mpaka kufa,na atawachia wengine. Kwa umri ule ni muda wa kuweka mambo yake sawa. Huku akiondokana na kukwaruzana na mamlaka. Kuna haja gani upende mali kuliko afya yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uhai hauna umri si ajabu(siombei) wewe kesho usiamke mwenzio anamiaka mingi mbele! Muhimu ni haki itendeke!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaelewa vizuri uhalisia wa lugha yangu ya kumaanisha umri. Kufa najua yoyote anakufa muda wowote. Kwa hiyo wewe unaona aendelee kuzing'ang'ania hela ingali bado anasoteshwa jera,kwa kitu ambacho anaweza kukitatua?.

Hata kama ana miaka mia 200 tena mbele,hiyo miaka ina maana gani ukiwa kwenye mateso?. Wakati huo huo uwezo wa kuwa huru uko mikononi mwake,ni kiasi kadhaa kiende anakodaiwa,then arudi uraiani akiwa huru aendelee kuishi hiyo miaka yake mia 2,akiwa huru. (Sheria duniani haki mbinguni)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee anazidi kujiharibia. Akitaka kufuata sheria watafia ndani. Walishapewa nafasi,wangeitumia ile nafasi. Kama bado ipo washaurini waitumie. Hiki sio kipindi kizuri kwake cha kupambana kisheria. Aandike barua ya kulipa kile kinachowezekana ili asamehewe. Fikiria kama anamiliki mfano trillions 3 (ambazo najua anamiliki zaidi ya hizo). Labda Wamemwambia alipe trillion 1.7 hivi. Kwa nini uzing'ang'anie huku ukiendelea kuteseka?. Kwanza umri umemtupa mkono,hizo atakazobaki nazo pamoja na miradi yake mingine ataishi anakula mpaka kufa,na atawachia wengine. Kwa umri ule ni muda wa kuweka mambo yake sawa. Huku akiondokana na kukwaruzana na mamlaka. Kuna haja gani upende mali kuliko afya yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyepesi nyepesi ni kuwa ameamua kupambana mpaka aone mwisho wake.
 
Back
Top Bottom