TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Waziri mkuu mh Majaliwa amefika nyumbani kwa baba mzazi wa Ruge na tayari ameshasaini kitabu cha maombolezo.

Pamoja naye yupo mkuu wa mkoa wa Dsm Paul Makonda hali kadhalika mbunge Dr Mwigulu na Zitto Kabwe

Source Clouds tv!
 
Rip RUGE.mean alikua mtu wa tofauti sana,umaalufu haukuwai kuumpa kibri,pesa azikuawai kumfanya ajione waina flani.coz alijawa na UTU,moyoni.ndo mana Leo kira anamzungumzia kwa mawazo,chanya.RPI bro ckuwai kukuona live but nilikua napata back story zako kua ni mwema sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu laana inawaandama. Yaani walishamtabiria kufa tangu wamvamiena vyombo vya moto. haki ya nani hii laana haitawaacha salama.
 
RIP Ruge yaani bado naona kama siamini nilionana na ruge pale THT wakati nilienda kurekodi aisee tutarudi mavumbini
 
SHAABAN ROBERT!
MIMI sichelei kufa, kudura yake Manani,
Kufa budi nitakufa, mchana ama jioni,
Hufa visivyo na ufa, sembuse aliye duni!
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Kama kufa ni maafa, naona bwana huponi,
Kiumbe hana sarifa, mauti yamo milini,
Nikifa hupati mafa, furaha yako nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Ikiwa kufa kashifa, si peke yangu ufuni,
Ikiwa neno la dhifa, sina mfundo moyoni,
Iwapo kufa sharafa, sifi ninangoja nini?
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni.
Hufa watu wenye sifa, na mafao duniani,
Wapenzi wake latifa, kama Mitume wa dini,
Hufa walaji wa mofa, na walao biriani,
Nakata shingo nusufa, na mkia kiungoni
 
Mbunge wa Kigoma mjini mh Zitto amesema Ruge Mutahaba alikuwa na uwezo wa kifikiri zaidi ya itikadi ya vyama.
Ruge aliweza kuwaunganisha pamoja wanasiasa kutoka CCM, Chadema, ACT nk na kufanya jambo mkiwa wamoja huku itikadi mmeziacha pembeni.

Zitto anasema hata project ya Fursa inayofanyika kila mwaka sambamba na Fiesta walianzisha pamoja mwaka 2012 na kuanza kutekelezwa mwaka 2013

Katika hili nampongeza Ruge kwa kuamini katika falsafa ya maendeleo hayana vyama.

Rip Ruge
Maendeleo hayana vyama!
 
Siku za binadam zinahesabika tangu tumboni mwa mama yake.
pumzika kwa amani.
 
Pia aliwahasa vijana waache kulalamika kwa mamlaka ajira ajira! watumie fursa zilizopo mtaani kujiajili..! Zitto analikumbuka hili?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom