mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,873
- 18,433
Nilisikiliza kwa makini kipindi chote alichotumia Ruge kuueleza umma kile walichokiita KILE KILICHOTOKEA.
Ruge aliulizwa swali muhimu sana na mmoja wa walioshiriki kipindi hicho. Swali lilikuwa: Makonda alikaa muda gani pale studio? Ruge alijibu bila kusita wala kupepesa macho na kwa kujiaminj kuwa alitumia dakika 20!
Lakini ile clip iliyo-leak inaonyesha kuwa aliingia 22:46 na akatoka 23:23. Kwa hiyo alitumia dakika 37!
Kumbukeni kuwa tukio ni la tarehe 17/3/2017 na kipindi cha nini kilichotokea kilikuwa tarehe 20/3/2017. Kwa hiyo ni lazima mkanda wa CCTV walikuwa wameshausoma tayari na moja ya kitu muhimu kwenye mkanda huo ni kubaini mwanzo na mwisho wa tukio! Kwa hiyo wakati wa kipindi Ruge alikuwa anajua muda halisi uliotumika kwenye uvamizi. Lakini pamoja na kujua aliamua kudanganya!
Kumbukeni pia kabla ya kipindi alikuwa ameshahojiwa na polisi kuhusu tukio hilo! Kwa weledi wa polisi ni lazima suala la muda uliotumika liliulizwa na bila shaka polisi walimtaka awasilishe mkanda wa CCTV kama kitendea kazi chao!
Kwa hiyo cha kujiuliza ni kwa nini aliamua kudanganya? Jibu ni kwamba kulikuwa na kitu kinafichwa! Je kitu gani kinafichwa? Hapo ndipo nawaalika wadau tudadavue!
Kwa maoni yangu, lengo ni kuficha baadhi ya mambo aliyoyafanya Makonda na msafara wake! Tufikiri, mtu mwenye hasira, akiwa na silaha akakaa kwako kwa dk 37 atakuwa anakupa soda? au story tamu? Jibu ni hapana!
Sana sana huo muda atautumia kukupa kibano na vitisho! Nadhani aina ya vibano na vitisho hivyo ndivyo ambavyo Ruge ameamua kuvificha kwa manufaa ya rafiki yake!
Nadhani pia ile document aliyoifuata pale wahusika hawakumpa kwa hiari yao! Kulikuwa na majibizano yaliyochukua muda na huenda walilainishwa kwa kipigo!
Huenda pi kama Makonda alikuwa amewalipa "ujira" wa kazi hiyo, basi wahusika walikuwa wanadaiwa waziteme hizo pesa maana kazi hawajaikamilisha!
Huenda pia wale vijana waliifanya hiyo kazi kwa Mali kauli wakiamini kuwa mwisho wa siku mkuu atatoa "asante". Sasa wanadai asante yao ili watoe mkanda! Huenda hilo ndilo lililopelekea kipigo kinachodaiwa!
Kumbukeni pia Ruge alikanusha kuwa vijana wake walipigwa. Japo anasema wana hali mbaya na wameomba likizo!!!! Nini kimesabsbisha hiyo hali mbaya?
Majibu ya uhakika anayo Ruge! Ruge tuambie jinsi makonda alivyozitumia dakika 37 pale studio! Mkanda wote wa CCTV unao! Ikiwezekana uachie mkanda wote sebuleni kwa manufaa ya umma!
Maana hata huyo aliyelikisha bado kuna vitu alivibana!
Nadhani sababu nyingine ya Ruge kudanganya ni kumwepushia rafiki yake dhana ya kuteka document kwa mtutu wa bunduki! Anamwepushia dhana ya ujambazi! Maana kupiga kunadhihirisha kuwa document iliporwa kwa mtutu na haikutolewa kwa hiari hivyo kufanya tukio lote kuwa la ujambazi!