RUFIJI: Wanafunzi 320 wanasomea chini ya Mti na kujisaidia porini

Inaonyesha kazi iliyo mbele ya rais, aungwe mikono afanikishe na kubadilisha haya yote.
 
Tatizo siyo tu kuwepo kwa Kiongozi aliyekosa Mipango, Bali kiini cha matatizo kama haya Ni Kuvurugika KWA Mfumo mzima WA Serikali. Tz hakuna Taasisi Imara, Madhubuti ambazo zipo competent ktk utendaji. Rais peke yake hawezi kufanya mambo yote ktk nchi Bali Taasisi husika ndio zingekuwa responsible ktk kutekeleza kazi zake kama hizi za kujenga Shule, hospitali, masoko , n.k.
KWA hali halisi ilivyo Tz, kana kwamba Rais ndiye amekuwa kila kitu, Ni mtaalamu WA kila gani, kiasi kwamba hakuna jambo lolote lile linaweza kufanyika bila ya Rais WA nchi kuridhia kwanza, hopeless kabisa.
Kiongozi bora ni yule anayejenga mfumo madhubuti wa taasisi anayo/anazoongoza.

Tanzania kama sio Afrika yote viongozi tulionao/tunaowapata focus yao ni kujijenga wao na hujiona wao ndio kila kitu na bila yao hapawezi kufanyika kitu

Bado tuna safari ndefu na ili tufike tunahitaji kubali mindset hizi kuanzia kwa watoto kabisa

Mtu anasimama kwa mfano anasema 'nikiondoka haya hayatafanyika' halafu tutegemee mfumo madhubuti wa serikali hapa
 
Donor country halafu watoto wanakaa chini, hebu acheni utani, mzee wa kutembea na fuko la hela hajafika uko.
 
Kuungwa mkono wa deni la heslibu kutolipika? Linaongezeka.
Kiufupi hatuna rais

Mkimpa uhsirikiano mheshimiwa bla kumkwamisha au kuponda kila nzuri analolifanya, nchi itakua kiuchumi hadi ushangae hayo madeni yakifutwa na pia vyuo kuwa bure bila karo.
 
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini.

Source: millardayo
View attachment 1224757
Mlitaka mimi ndio niwajengee choo? Waende wakajisaidie kwenye choo cha diwani au mkurugenzi wa halmashauri...
 
Jana roho iliniuma sana kwa mzee wetu kutoa milioni 5 Tsh cash kwa ajili ya kusaidia shule ya Zambia na wakati ndani ya nchi yetu, bado changamoto kwenye sekta ya elimu ni nyingi!

Hakuishia hapo, bado amewapa tani 25 za korosho bure! kati ya tani 50 walizohitaji kwenda kuanzisha hicho kilimo cha korosho nchini mwao.

Kulikuwa kuna sababu gani ya msingi ya kuwapa hao Wazambia korosho za bure na wakati wana uwezo wa kununua tani zote 50? Hizi sifa za huyu mtawala wetu kwa nini hazina mipaka? Hivi tumeshakua donor country mapema kiasi hiki!
Kuna kibwagizo zilipendwa... "sifa inaua..."
 
Mimi nafikiri kwa kasi aliyonayo Mzee baba, angeanzisha task force moja babukubwa kwa ajili ya kushughulikia kero km hizo za,wanafunzi kukaa chini, wanafunzi kukosa madarasa ya kusomea na mahitaji yao mengine tu,kwani rasilimali ni nyingi sana na zimetuzunguka kila upande.
Kwa mfano jamaa anatowa mzee baba anatowa km 500ml kwa mwezi kwa task force team kukamilisha ivyo viporo vyote, then kunakuwa na team ya ufuatiliaji wa iyo miradi nafikiri kutakuwa na tija kubwa sana.
 
Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya watakua na uwezo Mdogo ,hayo yapo ndani ya uwezo wao
 
Back
Top Bottom