"Tunanunua ndege,na kujenga Standadi gegi na stigulaz goji.....elimu baadae"
Ni mipango tu ya serikali haiko sawa japo umepotoshaPesa Inayonuna Ndege 1 kwa bilion 270 airbus inaweza kujenga shule za kisasa za milion 100 Kila Moja Zaidi Ya 270 Zitakazodumu Kwa Miaka 50 Na Kutoa Ajira Kwa Walimu Kama 2700 Wakati Ndege Sina Uhakika Kama Inaweza Dumu Kwa Miaka 30" Pamoja Na Kufanyiwa Service Kila Mara
Yanaathiri maana hii nchi ni kubwa na watu wako scattered sana ilhali kuwafikia ni changamoto..chumba kimoja cha kisasa cha darasa ni mil.25 with solar na furniture na uwezo wa watoto 45 sasa piga hesabu utapata jibuHivi kweli tunashindwa kujenga madarasa toka uhuru umepatikana? Madarasa yanagharimu kiasi gani? Kununua ndege kunaathiri vipi ujengaji wa hayo madarasa? Hizo hela wanazoiba huko kwenye halmashauri zingejenga madarasa mangapi?
Waafrika buana...tunaishi kwa hisia zetu za kinyonge
Hizo hesabu sio sahihi. Hazina uhalisia. Kila sehemu inategemea upatikanaji wa materials na labor.Yanaathiri maana hii nchi ni kubwa na watu wako scattered sana ilhali kuwafikia ni changamoto..chumba kimoja cha kisasa cha darasa ni mil.25 with solar na furniture na uwezo wa watoto 45 sasa piga hesabu utapata jibu
Baki na ubishi wako hiyo ni average cost inayotumiwa na serikali kujenga madarasa ya kisasa hasa ya sekondariHizo hesabu sio sahihi. Hazina uhalisia. Kila sehemu inategemea upatikanaji wa materials na labor.
Let's not be generalists
Baki na ubishi wako hiyo ni average cost inayotumiwa na serikali kujenga madarasa ya kisasa hasa ya sekondari
Kwa bweni ni mil.75 na kwa vituo vya afya ni mil.500 sasa hutaki unaacha naongea kitu nilichokifanya
Bombadier ndiyo kipaumbele chetu hayo maswala ya kusoma tayari tunao wasomi wengi sana kina palamagamba kabudi wanatutosha.
Kimbunga, sycophants mna shida kweli kweli...msivyokuwa na aibu, mtalamba miguu ya jiwe hadi ndimi zenu zichakae. Hebu soma hii hapa chini.Siamini kama hali hiyo bado ipo hapa Tanzania hasa Tanzania ya Magufuli na hasa kwenye Mkoa ambao unaongoza kwa uwekezaji wa viwanda.
Hizi milioni tano kusaidia shule ya Zambia, inazua maswali kadhaa. Je amejuaje huko Zambia wanayo matatizo kama hajui hapo jirani yake kuna tatizo kubwa zaidi.Jana roho iliniuma sana kwa mzee wetu kutoa milioni 5 Tsh cash kwa ajili ya kusaidia shule ya Zambia na wakati ndani ya nchi yetu, bado changamoto kwenye sekta ya elimu ni nyingi!
Kubwa la sycophants Kimbunga, je unalo jibu hapa?Hizi sifa za huyu mtawala wetu kwa nini hazina mipaka? Hivi tumeshakua donor country mapema kiasi hiki!
Hata waziri ana uwezo wa kununua gari kwani lazma atembelee la serikali na anunuliwe mafuta? Si awe mzalendo tu. Wale ni walipa kodi ni haki yao watoto zao kujengewa na kupewa elimu bora.Mzazi mmoja anaweza jenga nyumba yake lakini wazazi wa watoto 400 wanashindwa jenga madarasa 5 kwa ajiri ya watoto wao mpaka wajengewe na serikali? Mambo mengine ni uninga wa ngozi nyeusi tu kila kitu serikali ndio inawatuma kuzaa.
Je unayo habari kwamba hizo hela unazoita za serikali zinatokana na kodi za wananchi hao hao 400? Na hizo kodi wananchi hao 400 wanazilipa ili watoto wao waweze kusoma katika mazingira yanayoridhisha? Badala yake serikali inazitumia kuwanunulia viongozi wakorofi na walafi magari ya mabilioni na anasa zingine huku watoto wao wakiendelela kusoma chini ya miembe. Kuona vituko vya hovyo kama hivi ni sawa, ni kiwango cha upumbavu unaoweza kuvumiliwa tu na watu kama wewe, pole sana.Mzazi mmoja anaweza jenga nyumba yake lakini wazazi wa watoto 400 wanashindwa jenga madarasa 5 kwa ajiri ya watoto wao mpaka wajengewe na serikali? Mambo mengine ni uninga wa ngozi nyeusi tu kila kitu serikali ndio inawatuma kuzaa.
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.
Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini.
Source: millardayo
View attachment 1224757
Hebu fikiria kwa shule zinazopokea Tsh. Milioni 1 hadi 2 tu kila mwezi kama fidia ya ada, baada ya miaka mitatu tu fedha hizi zingesimamiwa kuboresha miundombinu ya shule tu sasa hivi shule zingekuwa na hali gani?
Hii nchi ni kubwa sana na ili iendelee inahitaji kiongozi mwenye plan za muda mfupi na muda mrefu zinazotekelezeka bila kuweka sifa na majigambo mbele
Kwa mfano mimi huwa nikiona hizi shule zilizochakaa na watoto kukaa chini, wengine chini ya miti, walimu hawana ofisi wala furniture za kukalia najiuliza swali moja tu, kwanini serikali iliamua kufuta ada wakati shule nyingi bado hazina miundombinu mizuri?
Kiongozi mwenye plan nzuri, kama kweli aliona gape la hela za elimu asingefuta ada kwanza, hizi pesa zinazopelekwa mashuleni kama fidia ya ada zingepelekwa kuboresha miundombinu kwanza!
Serikali ikasimamia vizuri, zijenge madarasa, maabara, ofisi, vyoo, madawati, vitabu vya kutosha!
Hebu fikiria kwa shule zinazopokea Tsh. Milioni 1 hadi 2 tu kila mwezi kama fidia ya ada, baada ya miaka mitatu tu fedha hizi zingesimamiwa kuboresha miundombinu ya shule tu sasa hivi shule zingekuwa na hali gani?
Ni dhahiri shule zingekuwa na hali nzuri na huenda ndani ya miaka mitatu au mitano tungeondokana na hii kero ya watoto kukaa chini, kusomea chini ya miti, ukosefu wa ofisi, vyoo na maabara
Halafu hapo ndo ada na michango yote vingefutiliwa mbali kabisa!
Kwa mtazamo wangu hili lilitakiwa litekelezwe hivi maana ada kwa ilipokuwa imefika palikuwa sio pabaya! Elfu 20 kwa mwaka, Mzazi na mtoto mwenye nia kweli ya kusoma isingekosekana kwa mwaka mzima