RUFIJI: Wanafunzi 320 wanasomea chini ya Mti na kujisaidia porini

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
11,440
12,294
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini.

Source: millardayo
 
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini .
Source: millardayo
View attachment 1224757
Kipaumbele chetu ni ndege, SGR, Umeme, barabara, hospital na wahujumu uchumi! Sekta ya Elimu isubiri awamu nyingine tunaenda hatua kwa hatua
 
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini .
Source: millardayo
View attachment 1224757
Bombadier ndiyo kipaumbele chetu hayo maswala ya kusoma tayari tunao wasomi wengi sana kina palamagamba kabudi wanatutosha.
 
ndio maana sitaondoka madarakani ili nirekebishe hayo mambo,,hiyo shule haikuanza wakati wangu huu,waliopita ndio wamefikisha hapo
 
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini .
Source: millardayo
View attachment 1224757
Hii nchi ni kubwa sana na ili iendelee inahitaji kiongozi mwenye plan za muda mfupi na muda mrefu zinazotekelezeka bila kuweka sifa na majigambo mbele

Kwa mfano mimi huwa nikiona hizi shule zilizochakaa na watoto kukaa chini, wengine chini ya miti, walimu hawana ofisi wala furniture za kukalia najiuliza swali moja tu, kwanini serikali iliamua kufuta ada wakati shule nyingi bado hazina miundombinu mizuri?

Kiongozi mwenye plan nzuri, kama kweli aliona gape la hela za elimu asingefuta ada kwanza, hizi pesa zinazopelekwa mashuleni kama fidia ya ada zingepelekwa kuboresha miundombinu kwanza!

Serikali ikasimamia vizuri, zijenge madarasa, maabara, ofisi, vyoo, madawati, vitabu vya kutosha!

Hebu fikiria kwa shule zinazopokea Tsh. Milioni 1 hadi 2 tu kila mwezi kama fidia ya ada, baada ya miaka mitatu tu fedha hizi zingesimamiwa kuboresha miundombinu ya shule tu sasa hivi shule zingekuwa na hali gani?

Ni dhahiri shule zingekuwa na hali nzuri na huenda ndani ya miaka mitatu au mitano tungeondokana na hii kero ya watoto kukaa chini, kusomea chini ya miti, ukosefu wa ofisi, vyoo na maabara

Halafu hapo ndo ada na michango yote vingefutiliwa mbali kabisa!

Kwa mtazamo wangu hili lilitakiwa litekelezwe hivi maana ada kwa ilipokuwa imefika palikuwa sio pabaya! Elfu 20 kwa mwaka, Mzazi na mtoto mwenye nia kweli ya kusoma isingekosekana kwa mwaka mzima
 
Siasa tu na kudandia hoja za upinzani.
 
Siamini kama hali hiyo bado ipo hapa Tanzania hasa Tanzania ya Magufuli na hasa kwenye Mkoa ambao unaongoza kwa uwekezaji wa viwanda. Halmashauri imekwama wapi kwenye suala hili? Mamlaka ya Mkoa haijui jambo hili kweli? Hii wala si ya Serikali kuu hii ni ya Serikali za mitaa. Wakati serikali kuu inapambana na miradi mikubwa ya kitaifa basi serikali za mitaa zipambanae na haya madogo. Mkurugenzi wa Rufiji inabidi ajitathmini kabla Mh Waziri Mkuu hajatia timu hapo.
 
Jana roho iliniuma sana kwa mzee wetu kutoa milioni 5 Tsh cash kwa ajili ya kusaidia shule ya Zambia na wakati ndani ya nchi yetu, bado changamoto kwenye sekta ya elimu ni nyingi!

Hakuishia hapo, bado amewapa tani 25 za korosho bure! kati ya tani 50 walizohitaji kwenda kuanzisha hicho kilimo cha korosho nchini mwao.

Kulikuwa kuna sababu gani ya msingi ya kuwapa hao Wazambia korosho za bure na wakati wana uwezo wa kununua tani zote 50? Hizi sifa za huyu mtawala wetu kwa nini hazina mipaka? Hivi tumeshakua donor country mapema kiasi hiki!
 
Hiyo sio Tanzania hao ni wachonganishi, Tanzania hakuna shule ya hivyo, huoni tunasaidia na wenzetu Zambia wajenge shule za kisasa kama zetu.. Huku elimu ni bure na shule zote zinamadawati hakuna mtoto anayekaa chini, Walimu mishahara yakutosha, shule zina lab za practicals mpaka comp lab za kutosha.. Mnataka nini tena Watanzania kama haitoshi tunajenga maflyover, Matrain ya umeme nk... Chagua CCM 2020, Chagua Magu 2020 tujenge njia nane dar to mwanza, dar to mbeya..
 
Jana roho iliniuma sana kwa mzee wetu kutoa milioni 5 Tsh cash kwa ajili ya kusaidia shule ya Zambia na wakati ndani ya nchi yetu, bado changamoto kwenye sekta ya elimu ni nyingi!

Hakuishia hapo, bado amewapa tani 25 za korosho bure! kati ya tani 50 walizohitaji kwenda kuanzisha hicho kilimo cha korosho nchini mwao.

Kulikuwa kuna sababu gani ya msingi ya kuwapa hao Wazambia korosho za bure na wakati wana uwezo wa kununua tani zote 50? Hizi sifa za huyu mtawala wetu kwa nini hazina mipaka? Hivi tumeshakua donor country mapema kiasi hiki!
Kutoa ni moyo usambe ni utajiri!
 
Back
Top Bottom