RUFIJI: Wanafunzi 320 wanasomea chini ya Mti na kujisaidia porini

kandamatope

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2018
Messages
298
Points
250

kandamatope

JF-Expert Member
Joined May 19, 2018
298 250
Fikra za kishamba kutoka kwa mtoa hoja,
Watu wanatoa michango ya harusi mbaka laki tano, nyumbani kwake mwaka mzima mbaka unaisha mkewe chupi mpya hana,.. Na maisha yanakwenda bila lawama.. Ni kawaida sana
Sio Kila kitu kwako kimetimizwa ndio uweze kutoa misaada, kwa binaadam wa kawaida hilo aliwezekani,
hakuna mtu hapa duniani anayetimiza kila kitu katika familia yake, kisha ndio atoe msaada binaadam huyo ayupo duniani..
 

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
15,946
Points
2,000

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
15,946 2,000
"Tunanunua ndege,na kujenga Standadi gegi na stigulaz goji.....elimu baadae"
Hivi kweli tunashindwa kujenga madarasa toka uhuru umepatikana? Madarasa yanagharimu kiasi gani? Kununua ndege kunaathiri vipi ujengaji wa hayo madarasa? Hizo hela wanazoiba huko kwenye halmashauri zingejenga madarasa mangapi?
Waafrika buana...tunaishi kwa hisia zetu za kinyonge
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
3,662
Points
2,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
3,662 2,000
Pesa Inayonuna Ndege 1 kwa bilion 270 airbus inaweza kujenga shule za kisasa za milion 100 Kila Moja Zaidi Ya 270 Zitakazodumu Kwa Miaka 50 Na Kutoa Ajira Kwa Walimu Kama 2700 Wakati Ndege Sina Uhakika Kama Inaweza Dumu Kwa Miaka 30" Pamoja Na Kufanyiwa Service Kila Mara
Ni mipango tu ya serikali haiko sawa japo umepotosha
Kwa sasa chumba kimoja cha darasa cha kisasa ni mil.25,,sasa kwa pesa hiyo serikali ingeweza kujenga shule mpya za kisasa 540,,huku hiyo shule ikiwa na block 7 zenye vyumba 14 vya kisasa(wanafunzi 650),,matundu 10 ya vyoo vya kisasa,,ofisi ya walimu ya kisasa na nyumba 2 za watumishi ambapo vyote hivyo vinakwenda kwa mil.500
Force account ingetumika kama vituo vya afya nguvu ndogo ya wananchi ingetumika hizo shule zingepata maji ya uhakika na samani
Ni vyema serikali ipitie upya vipaombele vyake ili matatizo madogo madogo kama haya tuyamalize hasa awamu ya pili ya uongozi wake.Ukitenga miaka mitano mfululizo hizo pesa ni zaidi ya shule za kisasa 2200 zitajengwa na huenda tatizo likawa limepungua kwa zaidi ya asilimia tisini
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
3,662
Points
2,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
3,662 2,000
Hivi kweli tunashindwa kujenga madarasa toka uhuru umepatikana? Madarasa yanagharimu kiasi gani? Kununua ndege kunaathiri vipi ujengaji wa hayo madarasa? Hizo hela wanazoiba huko kwenye halmashauri zingejenga madarasa mangapi?
Waafrika buana...tunaishi kwa hisia zetu za kinyonge
Yanaathiri maana hii nchi ni kubwa na watu wako scattered sana ilhali kuwafikia ni changamoto..chumba kimoja cha kisasa cha darasa ni mil.25 with solar na furniture na uwezo wa watoto 45 sasa piga hesabu utapata jibu
 

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
15,946
Points
2,000

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
15,946 2,000
Yanaathiri maana hii nchi ni kubwa na watu wako scattered sana ilhali kuwafikia ni changamoto..chumba kimoja cha kisasa cha darasa ni mil.25 with solar na furniture na uwezo wa watoto 45 sasa piga hesabu utapata jibu
Hizo hesabu sio sahihi. Hazina uhalisia. Kila sehemu inategemea upatikanaji wa materials na labor.
Let's not be generalists
 

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
3,662
Points
2,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
3,662 2,000
Hizo hesabu sio sahihi. Hazina uhalisia. Kila sehemu inategemea upatikanaji wa materials na labor.
Let's not be generalists
Baki na ubishi wako hiyo ni average cost inayotumiwa na serikali kujenga madarasa ya kisasa hasa ya sekondari
Kwa bweni ni mil.75 na kwa vituo vya afya ni mil.500 sasa hutaki unaacha naongea kitu nilichokifanya
 

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
15,946
Points
2,000

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
15,946 2,000
Baki na ubishi wako hiyo ni average cost inayotumiwa na serikali kujenga madarasa ya kisasa hasa ya sekondari
Kwa bweni ni mil.75 na kwa vituo vya afya ni mil.500 sasa hutaki unaacha naongea kitu nilichokifanya
Wala sibishani. Hela zinaliwa mno huko kwenye halmashauri. Sababu ya kufikiria kulalamika kunasaidia, tunahamisha goli. Eti kununua ndege. Sio kweli. Tunazidanganya nafsi zetu. Shida yetu ni wizi uliopitiliza
 

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,730
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,730 2,000
Siamini kama hali hiyo bado ipo hapa Tanzania hasa Tanzania ya Magufuli na hasa kwenye Mkoa ambao unaongoza kwa uwekezaji wa viwanda.
Kimbunga, sycophants mna shida kweli kweli...msivyokuwa na aibu, mtalamba miguu ya jiwe hadi ndimi zenu zichakae. Hebu soma hii hapa chini.
Jana roho iliniuma sana kwa mzee wetu kutoa milioni 5 Tsh cash kwa ajili ya kusaidia shule ya Zambia na wakati ndani ya nchi yetu, bado changamoto kwenye sekta ya elimu ni nyingi!
Hizi milioni tano kusaidia shule ya Zambia, inazua maswali kadhaa. Je amejuaje huko Zambia wanayo matatizo kama hajui hapo jirani yake kuna tatizo kubwa zaidi.
Hizi sifa za huyu mtawala wetu kwa nini hazina mipaka? Hivi tumeshakua donor country mapema kiasi hiki!
Kubwa la sycophants Kimbunga, je unalo jibu hapa?
 

msindikizaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Messages
1,298
Points
2,000

msindikizaji

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2010
1,298 2,000
Mzazi mmoja anaweza jenga nyumba yake lakini wazazi wa watoto 400 wanashindwa jenga madarasa 5 kwa ajiri ya watoto wao mpaka wajengewe na serikali? Mambo mengine ni uninga wa ngozi nyeusi tu kila kitu serikali ndio inawatuma kuzaa.
Hata waziri ana uwezo wa kununua gari kwani lazma atembelee la serikali na anunuliwe mafuta? Si awe mzalendo tu. Wale ni walipa kodi ni haki yao watoto zao kujengewa na kupewa elimu bora.
 

Mag3

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Messages
10,730
Points
2,000

Mag3

JF-Expert Member
Joined May 31, 2008
10,730 2,000
Mzazi mmoja anaweza jenga nyumba yake lakini wazazi wa watoto 400 wanashindwa jenga madarasa 5 kwa ajiri ya watoto wao mpaka wajengewe na serikali? Mambo mengine ni uninga wa ngozi nyeusi tu kila kitu serikali ndio inawatuma kuzaa.
Je unayo habari kwamba hizo hela unazoita za serikali zinatokana na kodi za wananchi hao hao 400? Na hizo kodi wananchi hao 400 wanazilipa ili watoto wao waweze kusoma katika mazingira yanayoridhisha? Badala yake serikali inazitumia kuwanunulia viongozi wakorofi na walafi magari ya mabilioni na anasa zingine huku watoto wao wakiendelela kusoma chini ya miembe. Kuona vituko vya hovyo kama hivi ni sawa, ni kiwango cha upumbavu unaoweza kuvumiliwa tu na watu kama wewe, pole sana.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,612
Points
2,000

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,612 2,000
Shule ya Msingi King'ongo inakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ya wanafunzi wake 320 kati ya 444 kusomea chini ya miti na kukaa chini huku wanafunzi 124 pekee ndio ambao wanasomea darasani tena ni wale ambao wana Mitihani ya Taifa.

Shule hii ipo katika Kata ya Muhoro iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo wanafunzi hao wote 444 wanatumia choo kimoja kilichozungushiwa makuti chenye matundu mawili tu tena hadi walimu wao 9 wanatumia choo hicho, huku wengine wakilazimika hata kujisaidia porini.

Source: millardayo
View attachment 1224757
Rufiji hakuna wanaume?
 

mbongopopo

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2008
Messages
1,167
Points
1,225

mbongopopo

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2008
1,167 1,225
Hebu fikiria kwa shule zinazopokea Tsh. Milioni 1 hadi 2 tu kila mwezi kama fidia ya ada, baada ya miaka mitatu tu fedha hizi zingesimamiwa kuboresha miundombinu ya shule tu sasa hivi shule zingekuwa na hali gani?
Una points nzuri, pia tatizo kubwa sana ni watendaji wake wanao muwakilisha katika kazi mbalimbali.
Kwa sasa wanapokea ili wazitumieje?
 

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
871
Points
1,000

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
871 1,000
Hii nchi ni kubwa sana na ili iendelee inahitaji kiongozi mwenye plan za muda mfupi na muda mrefu zinazotekelezeka bila kuweka sifa na majigambo mbele

Kwa mfano mimi huwa nikiona hizi shule zilizochakaa na watoto kukaa chini, wengine chini ya miti, walimu hawana ofisi wala furniture za kukalia najiuliza swali moja tu, kwanini serikali iliamua kufuta ada wakati shule nyingi bado hazina miundombinu mizuri?

Kiongozi mwenye plan nzuri, kama kweli aliona gape la hela za elimu asingefuta ada kwanza, hizi pesa zinazopelekwa mashuleni kama fidia ya ada zingepelekwa kuboresha miundombinu kwanza!

Serikali ikasimamia vizuri, zijenge madarasa, maabara, ofisi, vyoo, madawati, vitabu vya kutosha!

Hebu fikiria kwa shule zinazopokea Tsh. Milioni 1 hadi 2 tu kila mwezi kama fidia ya ada, baada ya miaka mitatu tu fedha hizi zingesimamiwa kuboresha miundombinu ya shule tu sasa hivi shule zingekuwa na hali gani?

Ni dhahiri shule zingekuwa na hali nzuri na huenda ndani ya miaka mitatu au mitano tungeondokana na hii kero ya watoto kukaa chini, kusomea chini ya miti, ukosefu wa ofisi, vyoo na maabara

Halafu hapo ndo ada na michango yote vingefutiliwa mbali kabisa!

Kwa mtazamo wangu hili lilitakiwa litekelezwe hivi maana ada kwa ilipokuwa imefika palikuwa sio pabaya! Elfu 20 kwa mwaka, Mzazi na mtoto mwenye nia kweli ya kusoma isingekosekana kwa mwaka mzima
Tatizo siyo tu kuwepo kwa Kiongozi aliyekosa Mipango, Bali kiini cha matatizo kama haya Ni Kuvurugika KWA Mfumo mzima WA Serikali. Tz hakuna Taasisi Imara, Madhubuti ambazo zipo competent ktk utendaji. Rais peke yake hawezi kufanya mambo yote ktk nchi Bali Taasisi husika ndio zingekuwa responsible ktk kutekeleza kazi zake kama hizi za kujenga Shule, hospitali, masoko , n.k.
KWA hali halisi ilivyo Tz, kana kwamba Rais ndiye amekuwa kila kitu, Ni mtaalamu WA kila gani, kiasi kwamba hakuna jambo lolote lile linaweza kufanyika bila ya Rais WA nchi kuridhia kwanza, hopeless kabisa.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
46,740
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
46,740 2,000
Nilipita Muhoro miaka ya 90. Mji ulikuwa unanunuka mavi.

Mpaka leo bado hali haijabadilika sana naona.
 

Easyway

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
2,491
Points
2,000

Easyway

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
2,491 2,000
Shauri yao kwani wanasoma watoto wetu?
Sisi viongozi hatusomeshi watoto wetu hizo shule ni shule zenu ninyi wapiga kura.
 

Forum statistics

Threads 1,343,347
Members 515,021
Posts 32,781,651
Top