Hali inayoendelea Rufiji na Kibiti si ya kufumbia macho,kwani hali ni mbaya sana.
Matukio yanayotokea mpaka hivi siku za karibuni za mauaji hususan ktk miji ya Ikwiriri na Jaribu si vya kuungwa mkono na mtu yeyote ambaye ana matumizi sahihi ya akili zake.
Lakini ajabu iliyopo sasa ni hiki kinachoitwa Operation Maalum inayoendelea.Kama utaongea na watu wa maeneo husika watakuambia wazi kuwa sasa hakuna operation ya kusaka wahalifu wale bali ni kutoa mateso makubwa kwa raia ambao ilitegemewa kuwa bega kwa bega na wana usalama walioko kule.
Lakini ajabu iliyo kubwa ni hiki kinachoendelea sasa ambapp polisi ndio wamekuwa watesaji wakubwa wa raia.Udhalilishaji ni mkubwa sana watu wanapigwa tena bila sababu za msingi mbaya zaidi hawachagui hata mgonjwa,mjamzito,mtoto,mwanamke,mzee,kijana wote ni vipigo visivyo na ukomo.
Sasa raia wanajiuliza wana usalama hawa wamekuja kusaidia kusaka wahalifu au kuwatesa wanachi?
Inastaajabisha namna ambavyo wananchi wanabebeshwa shida isiyo na sababu.
Kulala saa 12 jioni ambako bado hakujatoa tija yoyote mpaka sasa maana toka itolewe amri hiyo mauaji yanaendelea kutokea.
Jeshi na watu mahiri ktk kufanya upelelezi wangetumika kuchunguza matukio haya.Kubwa ya yote ni kutafuta CHANZO si kufanya hiki kinachofanyika ambapo chuki inapamba sana kwa raia dhidi ya vyombo vya ulinzi na usalama.Hali hii itafanya kazi kuwa ngumu sana ya kupata suluhisho ya matukio haya.
Raia wanaelekea kuchoka njaa haina adabu.
Huu ni ushauri wa bure.