Rufiji,Kibiti na Mkuranga iangaliwe kwa jicho la tatu

ngapoleka

Senior Member
Mar 20, 2013
143
225
Matukio ya mauaji yasiyoeleweka yanayoendelea huko yamenifanya nami nitoe mtazamo wangu japo limekuwa ni jambo la hatari kwa sasa kuzungumzia kuliko kitu chochote.Nafsi yangu inaona nina cha kusema.

Toka matukio haya ya kutisha na kuogofya yaanze kutokea kumetolewa kauli nyingi za kila namna.Zikiwa na mitazamo ya kila mtu kusema anachojua au kuhisi ndio chanzo wa muendelezo huo.Wengi katika watoa maoni wamekuwa hasa ni wale walio katika nafasi mbalimbali za uongozi aidha kwa upande wa usalama au serikali na vyama vya siasa.Ninachotaka kuelezea hapa ni michango hiyo na athari zake ambazo ni chanya na hasi.

Kwanza ni watu wa usalama wamekuwa wakitoa ripoti zao mara nyingi ni kuelezea hasa matukio yanavyotokea.

Pili ni serikali ambao wao hutoa maelezo yao kwa mujibu wa taarifa za watu wa usalama lakini pia kutoa maoni yao na muda mwingine maelekezo kwa kile wanachokijua au kuhisi.Zingatia maelezo ya Waziri mwenye dhamana Mwigulu Lameck Nchemba ambaye aliwahi hata kufanya ziara huko.

Nakumbuka siku ya kwanza kabla hajaenda kule alihojiwa na moja kati ya vyombo vya habari vya nje ya nchi vinavyofanya kazi hapa nchini ,ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa anahisi ni matukio ya kama Visasi kwa Operesheni zinazoendelea kule.Ila baada ya kufika eneo la tukio akatoka na kauli ambayo sasa ndio imeshika kasi kuwa kuna SIASA kule.

Mwisho ni kundi la watu wa vyama ambapo Mbunge wa Rufiji na mwenzake wa Kibiti,hasa wa Rufiji alitamka moja kwa moja katika hali ya kulalamika kuwa wanaCCM wanauwawa,na kuomba serikali kuchukua hatua.

Huku pia ikiwemo taarifa ya kulalamika kutoka kwa Mng'eresa ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM Wilaya kwamba sasa wanachama wanaogopa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi wa chama kwa kuhofia kuuwawa.

Haikuishia hapo funga kazi ilikuwa ni ziara ya Katibu Mwenezi wa CCM taifa Itikadi na uenezi Humphrey Polepole ambaye alitoa lawama kwa vyombo vya usalama na hata kuwatishia wahusika katika usalama na serikali kudhibiti kuuwawa kwa wanaCCM vinginevyo watasababisha watu kupoteza kazi zao.Ilikuwa kauli nzito na ya kutishia.Kweli yaliyofuata siwezi kusema sote tunajua.

Baada ya yote haya sasa ninachotaka kusema au kutolea mawazo ni juu ya yote haya na hali ilivyo sasa Rufiji na Kibiti.

Ni kwamba kauli hii iliyoshikiwa bango sana na hawa wanasiasa leo inafanya hali kuzidi kuwa tete na ya hatari sana.Kwani tayari miji kama Ikwiriri viongozi wote wakiwemo wenyeviti wa vijiji,Vitongoji na madiwani wamekimbia kunusuru maisha yao ambapo mji kama Ikwiriri ambapo CUF ni chama tawala ikiwa inangoza kata zote tatu,vijiji 7 kati ya 9 vilivyopo na vitongoji zaidi ya asilimia 75 hawapo kazini.

Hivi tunapozungumza tayari wenyeviti wa Vijiji wawili ajulikanaye kama Kazi Mtoteke wa Ikwiriri Kati hajulikani alipo na mwenzake Kilumike wa kijiji cha Ikwiriri Kusini sina maelezo yake ila anashikiliwa na hayupo ila kwa kukatwa na nani sijui.

Pia ipo orodha ndefu ya watu ambao hawajulikani walipo.
Hofu yangu kuu ni kuwa kinachoandaliwa sasa kama ni mfuatiliaji wa historia ni kutokea kwa matukio kama yale ya Rwanda na Burundi au kwengine kote yalikotokea mauaji ya wenyewe kwa wenyewe.Mungu anusuru .

Kwanini nasema mauji ni kwamba kuna Interahamwe wameshaanza kazi sasa waziwazi ya kutaja watu hovyohovyo na wanatamba mjini kuwa watawataja wote.Watu hawa wapo wenye historia mbaya kabisa za kiuhalifu wengine waliwahi kukaa jela kwa miaka kadhaa wakituhumiwa kuwapotosha polisi katika kazi zao.

Kamanda mpya kuwa makini utakuja kubeba lawama zitazosababishwa na watu hawa.Si wazalendo hivyo ni wachumia tumbo na watafuta umaarufu kwa mgongo wa matatizo yaliyopo.

Mkumbo huu wameingizwa wanasiasa hasa wa upinzani,wafanyabiashara na kila mwenye mahusiano na upinzani.Hali ni tete sana tuinusuru Rufiji jamani.Watu hawa wa hovyo wanaosambaza Fitna hii kama hawakudhibitiwa muda si mrefu tutasema mengine.

"Siwezi kuwa adui kwa kusema kweli kwani Kweli itatuweka huru."
Mungu ibariki Rufiji,Kibiti na Mkuranga Mungu ibariki Pwani na Tanzania yetu.
 
Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
7,893
2,000
Kwann wanaouwawa ni watu wa ccm peke yake ikihali kata karibu zote zipo chini ya CUF
 
ngapoleka

Senior Member
Mar 20, 2013
143
225
Kwann wanaouwawa ni watu wa ccm peke yake ikihali kata karibu zote zipo chini ya CUF
Hapo palikuwa ndio pa kuanzia kutaka kujua hilo na si kuhusisha wapinzani moja kwa moja tena kwa hukumu bila kusikiliza mawazo na mtazamo wao.
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,535

We p.u.m.b.a.v.u.sana.
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
9,535
2,000
Ni ngumu kupata taarifa kwa wananchi kwasababu tayari polisi washaweka gepu baina yao na raia
Sasa wataunganishaje gape na Wakati askari ndio wanaouwa na hao wananchi?!! Utamfuataje mtu ndani ya kijiji ukashauriane naye ukitoka anakuvizia njiani akuuwe? Hivi mnafikiri vizuri nyinyi?!!
 
PAPAKINYI - SJUT 2013

JF-Expert Member
Jun 5, 2017
367
250
wanasiasa hawa wanatuharibia sana mambo, ndo maana nilimlaani sana mtatiro baada ya kupost ujinga kuhusu hili suala. endelea kutuhabarisha na kutujuza mkuu!!
 
Old - Hand

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
1,594
2,000
Hakuna kitu.... every thing is under control....

Zimebaki siasa na siri ya serikali.
Tu
 
South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,482
2,000
Sasa wataunganishaje gape na Wakati askari ndio wanaouwa na hao wananchi?!! Utamfuataje mtu ndani ya kijiji ukashauriane naye ukitoka anakuvizia njiani akuuwe? Hivi mnafikiri vizuri nyinyi?!!
Mkuu unaelewa umuhimu wa raia ktk kuwabaini waharifu kama hujui mtafute mpelelezi au askari anaweza kukupa ufahamu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom