Rufaa za Mitihani ya NECTA: Kesi ya mbuzi kupelekwa kwa chui

Je ile dhana ya kwamba mtu alikuwa hana uwezo mzuri darasani, ila Necta kaja kafaulu vizuri? Maajabu gan yanatokea km mtu alikuwa hana uwezo miaka miwili lakin mwisho anafaulu?
na vipi nafasi ya CA (continous assignment) katika matokeo ya mwsho ya mwanafunzi wa A level? Nauliza hivyo sababu my Ex classmate alikuwa na div 1, mpk tunamaliza 6, ila matokeo yametoka ana div.3 ya mwisho? Naomba mwongozo wenu mlio katika tasnia husika. nawasilisha.

Jamani, usahihishaji wa mitihani yote ya NECTA ni very accurate and fair. Mtu akifeli asipoteze muda wake kukata rufaa, kila swali hupitiwa na wataalamu wasiopungua wanne wa somo hilo, wote wakiwa na nia ya kumtendea haki mtahiniwa ambaye hata hawamjui. Kwa hiyo ukisikia mtu kafeli ujue ni kweli kafeli. Sitaki kueleza mengi maana mambo ya marking ni siri, ila tu watu wasipoteze muda kukata rufaa!!
Nadhani ungetumia neno fair peke yake ningekuelewa, lakini kusema accurate wakati kuna atu wanakata rufaa na kunakuwa na mabadiriko ya matokeo, si sahihi sana.
Turudi kwenye hoja. Mtoa mada anataka kiwepo chombo tofauti kitakachoshughulikia rufaa, siyo baraza lile lile lililoshahihisha. Hata mahakamani huwezi kukata rufaa ikasikilizwa na hakimu yuleyule aliyeihukumu mwanzo.
Haki ionekane kuwa inatendeka!

Mwanafunz akishakata rufaa,NECTA huwaandikia barua walimu kwa ajili ya re-marking,walimu huenda kusahihisha kama kawaida,wapo wanafunz ambao hufanikiwa,,,,,,,kwa mfano mwaka jana kuna mwanafunz alifel baada ya kukata rufaa kuna mwalim akaenda kusahihisha ikagundulika kuwa yule mwanafunz alikosea kuandika namba za maswal,baada ya kusahihishiwa akafaulu zaid jambo ambalo hata NECTA liliwashtua,ilimlazmu mwalim husika aandike barua kwa katibu mkuu mtendaj dr ndalichako
Nimekuwa nikifuatilia matokeo ya rufaa zinazoombwa na watahiniwa wanapohisi kuonewa katika usahihishaji wa Mitihani mara baada ya Matokeo kutolewa na Baraza la Mitihani. Haya ni pamoja na matokeo ya Form IV,VI,Vyeti na Diploma za Ualimu.

Mara nyingi rufaa zote(angalia matokeo ya sasa website ya NECTA), matokeo yake huwa hayabadiliki. Wao wanaandika "Hayajabadilika"

Huko nyuma wakati niko shule ilikuwa ni kawaida walimu kama binadamu, kupitiwa na kukosesha mwanafunzi swali alilofanyavizuri. Na ni kote, Chekechea hadi vyuo. Inakuwaje NECTA kusiwe na binadamu wa namna hiyo wakati tunaambiwa wasahihishaji hukusanywa kutoka taasisi zilezle ambako tumekuwa tukishuudia kasoro hizo za kibinadamu? yahani warufaa woote hakuna aliyeshinda!!! Wote hakuna aliyekuwa na busara na kupima alichofanya kuwa hakistahili kukatiwa rufaa!!

Hivi ni sahihi na kuwatendea haki watahiniwa, rufaa zao kurejewa(kupitiwa upya) na taasisi ileile inayotuhumiwa kusahihisha vibaya? Nahisi Necta hawawezi tenda haki kwa sababu:

1) Wao ni watuhumiwa wa kutokutenda haki katika usahihishaji wa mwanzo

2) Wataacha matokeo yawe yaleyale ili kuficha udhaifu uliofanyika mwanzo

3) Wastahiki wa kushinda rufaa hawatapewa ushindi kwa kuofia hata wale wasiositahiki watakuwa wamepoteza imani kwa wasahihishaji.

Maoni yangu: Kuwepo na chombo au Kamati maalumu baada ya matokeo ambayo itafanya kazi hiyo badala ya kufanywa na Baraza. Kamati hiyo isiwe na mafungamano yoyote na NECTA. Ikibidi warufani wenyewe walipie gharama za kurejea usahihishaji. Baraza linaweza kuwekewa utaratibu kupitia kile kilichofanywa na kamati hiyo itakayojitegemea. Hapa Warufaa watakuwa wametendewa haki. Mnasemaje?

Back
Top Bottom