Rufaa yamtoa gerezani diwani wa CHADEMA

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mbeya. Ikiwa ni takribani mwaka mmoja na mwezi mmoja tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani, Diwani wa Kata ya Iganjo jijini hapa kupitia CHADEMA, David Mwangonela ameachiwa huru na Mahakama Kuu.

Kuachiwa kwa diwani huyo juzi jioni na Mahakama hiyo kulitokana na rufaa aliyokata kupinga adhabu hiyo aliyopewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya.

Mwangonela alihukumiwa kutumikiwa adhabu hiyo baada ya kukutwa na magunia 171 ya ngano yaliyodaiwa kuibwa kwenye Chuo cha Utafiti na Kilimo Uyole.

Kabla ya adhabu hiyo wakati kesi ikisikilizwa watu wanne walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi na kusomewa mashtaka manne.

Mashtaka hayo yalikuwa ni kuvunja ghala, wizi wa magunia 171 ya ngano, kupatikana na mali ya wizi na kuzembea kuzuia kosa.

Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Ibrahim Mwangu, Juma Mwatumeli, Andrea Nsoka na David Mwangonela, lakini Mahakama ilimkuta na hatia mshtakiwa wa wanne, Mwangonela hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela ambacho alianza kukitumikia Novemba 17, 2015 huku wengine wakiachiwa huru.

Hata hivyo, Mwangonela alikata rufaa kupinga hukumu hiyo katika Mahakama Kuu jijini hapa ambayo ilianza kusikilizwa Aprili mwaka huu chini ya Jaji Mfawidhi, Noel Chocha.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Chocha alisema Mahakama ya Hakimu Mkazi ilimshtaki Mwangonela kwa kutumia vifungu vya sheria ambavyo vilikosewa, hivyo viini vya shtaka pia vilikuwa na makosa.

Alisema kutokana na kukosewa kwa viini vya shtaka alilokutwa nalo mshtakiwa huyo, Mahakama hiyo inaona hana hatia na kumuachia huru.

Pia, Mahakama iliagiza arudishiwe magunia 171 ya ngano au kiasi cha fedha kinacholingana na thamani yake.

“Mahakama inaamuru David arudishiwe magunia yake 171 ya ngano ambayo yalikuwa yamezuiwa au apewe fedha zinazoendana na thamani ya magunia hayo na yupo huru kuanzia sasa,” alisema Jaji Chocha.

Akizungumza na gazeti hili nje ya Mahakama, Mwangonela alisema Mahakama Kuu imemtendea haki ambayo aliporwa na kuwashukuru wapiga kura wake kwa uvumilivu waliouonyesha tangu akumbwe na mkasa huo, hivyo kushindwa kuwatumikia tangu walipomchagua katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Rufaa yamtoa gerezani diwani wa Chadema
 
hakukua na kesi hapo zilikuwa mbinu za ccm kumchafua nahuu nimwendelezo wa ccm kuchafua viongozi wa vyama vingine. huku wakijiita wameletwa na mungu kukomboa taifa mama Tanzania ..... yanamwisho haya
 
Kila la heri diwani
[HASHTAG]#freemaxencemelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TunamtakaBenAkiwaHai[/HASHTAG]
[HASHTAG]#JusticeForLema[/HASHTAG]
[HASHTAG]#usirudiekosa2020[/HASHTAG]
 
Njia ni ndefu sana kwa mahakama zetu. Hapo wanaweza kufanya maamuzi lakini likishakuwa ni suala linalohusu raia dhidi ya mhimili "uliojichimbia zaidi" mahakama zetu kwa kweli zinakuwa hazitendi haki. Kwa mfano kwenye Kesi ya Mtikila kupinga uchaguzi mdogo wa Ludewa iliamuliwa Ijumaa wakati uchaguzi ukawa unafanyika Jumapili siku mbili toka Hukumu ilipotolewa!
 
Kuna diwani mwingine wa kata ya Mkoma wilayani Rorya nae alibadilushiwa kifungo chake cha nje ya miezi 12 akiwa anakaribia kuimaliza na kurudishwa gerezani kisa amri kutoka juu
 
Mungu ibariki chadema.
Angeshindwa hiyo rufaa yake mgesema haya maagizo kutoka juu, kashinda rufaa yake badala uipe pongezi mahakama imetenda haki unakimbilia kwa Mungu aibariki Chadema, hujui hiyo Mungu ndiyo kaamua Chadema kiwe chama cha upinzani
 
Angeshindwa hiyo rufaa yake mgesema haya maagizo kutoka juu, kashinda rufaa yake badala uipe pongezi mahakama imetenda haki unakimbilia kwa Mungu aibariki Chadema, hujui hiyo Mungu ndiyo kaamua Chadema kiwe chama cha upinzani
Lubuva hajawahi kuwa mungu .
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom