AY na Mwana FA washinda rufaa yao dhidi ya Tigo, sasa kulipwa Billioni 2.1

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,213
2,326
Breaking News:
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali rufaa iliyofunguliwa na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa wasanii AY na MwanaFA Tshs 2,185,000,000 kwa kutumia nyimbo zao bila kulipa.

Wakili Albert Msando ambaye anawakilisha wasanii hao amesema huu ni ushindi muhimu kwa sanaa ya Tanzania. Amenukuliwa akisema "ni haki yao kulipwa kwa sababu ni kazi zao ambazo zinalindwa kisheria".

=======

Dar es Salaam. Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Hamisi Mwinjuma na Ambwene Yesayah ‘AY’ kwa mara nyingine wameibwaga mahakamani Kampuni ya Simu ya tigo baada ya kushinda pingamizi lao dhidi ya maombi ya kuzuia utekelezwaji wa hukumu ya awali.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya tigo kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyoiamuru kampuni hiyo iwalipe fidia ya Sh2 bilioni kwa makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki za wasanii hao.

Kampuni hiyo ilifungua maombi mahakamani hapo ikiomba mahakama hiyo iamuru utekelezaji wa hukumu hiyo ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala usimame kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa rufaa yao waliyoikata kupinga hukumu hiyo.

Hata hivyo wasanii hao kupitia wakili wao, Albert Msando waliweka pingamizi dhidi ya maombi hayo ya tigo ya kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo, wakiiomba mahakama hiyo iyatupilie mbali, pamoja na mambo mengine wakidai kuwa yana kasoro za kisheria.

Akitoa uamuzi wake leo, Jaji Isaya Arufani amekubaliana na hoja za pingamizi la wasanii hao na akatupilia mbali maombi hayo ya tigo na hivyo kusubiri usikilizwaji wa rufaa yao.

Katika pingamizi lao, pamoja na mambo mengine Wakili Msando amedai kuwa maombi hayo ni batili kwa kuwa hawakutaja kifungu maalumu cha sheria kinachoipa mahakama mamlaka ya kuyasikiliza na kuyatolea uamuzi.

Pia Wakili Msando amedai kuwa maombi hayo yanakiuka sheria kwa kuwa yamewasilishwa bila kuwekwa dhamana mahakamani kinyume cha sheria na kanuni za mahakama, huku katika hoja ya tatu wakidai kuwa hati ya kiapo kinachounga mkono maombi hayo ni batili.

Wakili Msando alifafanua kuwa ofisa mtoa maombi aliyetoa kiapo hicho, Tumaini Shija hakueleza kama mambo aliyoyaeleza kwenye kiapo hicho ni kutokana na ufahamu wake mwenyewe au ni ya kuambiwa.

Hata hivyo Wakili wa tigo, Mbwambo amepinga hoja hizo akidai kuwa kutaja vifungu vingi kwenye sheria hakuathiri uhalali wa maombi hayo na kwamba suala la dhamana linaangaliwa wakati wa usikilizwaji wa maombi na si kabla ya kuanza kuyasikiliza.

Kuhusu suala la ubatili wa kiapo, Wakili Mbwambo pamoja na mambo mengine alidai kuwa hata kama mahakama ikiridhika kuwa kuna aya ambazo zina kasoro basi tiba yake ni mahakama kuamuru ziondolewe au kuamuru kufanyika kwa marekebisho.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii Ni Mara Ya Pili?
Mkuu Hii Habari Nilisha Shuhudia
Sehemu Flani Ivi.
Kama Tigo Wamepinga Kulipa Fidia
Wana Mtafuta Msando Hapo
Kwa Habari Nilizo Nazo Wakili Huyu
Msomi Hajawahi Kushindwa Kesi Tangu
Aanze Uwakili.
Tigo Mnakazi Kushinda Hii Kesi.
Pongezi Kwa Msando, Mwana-FA & AY Katika Kutetea Haki Za Wasanii.
 
Mahakama Kuu yaitaka Kampuni ya TIGO kuwalipa Wasanii Ambene Yesaya Ay na Mwinjuma MwanaFA Sh. Bilioni 2.1 kwa makosa ya kutumia nyimbo zao bila kuwalipa.

Hapo awali Kampuni ya simu ya MIC Tanzania (Tigo) ilikata rufaa kupinga hukumu iliyoamuru iwalipe Sh2 bilioni wanamuziki wawili, Ambwene Yesaya na Hamisi Mwinjuma kutokana na kutumia bila ya ridhaa yao, nyimbo za wasanii hao nyota nchini.

Yesaya, ambaye ni maarufu kwa jina la kisanii la AY na Mwinjuma anayejulikana kwa jina la MwanaFA, walifungua kesi hiyo ya madai kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala kupinga kitendo cha kampuni hiyo ya huduma za simu kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ya ridhaa yao.

Nyimbo mbili zilizotumika kwenye miito hiyo ya simu ni “Dakika Moja” na “Usije Mjini” ambazo nyota hao wameshirikiana.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Juma Hassan alitoa hukumu ya kesi hiyo Aprili 11 2016, akiwapa ushindi wasanii hao maarufu katika muziki wa vijana uliopachikwa jina la Bongo Fleva.

Katika hukumu hiyo, Mahakama iliiamuru Tigo kulipa Sh5 milioni kama faini ya uharibifu na kulipa Sh2.16 bilioni kama faini ya jumla.

Wasanii hawa kushinda rufani hii, wameandika historia katika matumizi ya Sheria ya Haki Miliki na watakuwa wasanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kufungua kesi na kushinda.

Katika rufaa hiyo, Tigo kupitia kampuni ya Law Associates iliainisha sababu saba za rufani, ikidai hakimu wa Mahakama ya Ilala alikosea kisheria kuwapa ushindi wasanii hao kwa kuwa hawakuthibitisha madai yao wala hasara waliyopata.

Kampuni hiyo pia inadai kuwa mbali na kutoeleza hasara waliyoipata kutokana na kazi zao kutumika kwenye miito ya simu, walitakiwa kueleza faida ambayo wangepata kama kazi zao zisingetumika kwenye miito hiyo.

Sababu nyingine ya Tigo kukata rufaa hiyo ni wasanii hao hawakuwa wamesajili kazi zao Chama cha Hakimiliki Tanzania (Cosota).

Tigo ilidai kuwa wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi, wadai walisema wamesajili kazi hizo, lakini waliwasilisha barua ya Baraza la Sanaa (Basata) ya kutambua kupokea kazi zao na si cheti cha usajili cha Cosota.

Kwa mujibu wa Tigo, wanamuziki hao walipaswa kuwasilisha mahakamani cheti cha usajili wa Cosota ambako kuna utaratibu wa kujisajili ikiwa ni pamoja na kujaza fomu maalumu baada ya kulipia malipo ya usajili ya kila mwaka.

Kampuni hiyo ilisisitiza kuwa wasanii hao hawakuwa na haki ya kudai fidia hiyo wakati hawajasajili kazi hizo Cosota na hivyo kuiomba Mahakama Kuu itengue hukumu iliyowapa ushindi.

Sasa wameshinda. Hongereni Wasanii wetu.
 
Hii Ni Mara Ya Pili?
Mkuu Hii Habari Nilisha Shuhudia
Sehemu Flani Ivi.
Kama Tigo Wamepinga Kulipa Fidia
Wana Mtafuta Msando Hapo
Kwa Habari Nilizo Nazo Wakili Huyu
Msomi Hajawahi Kushindwa Kesi Tangu
Aanze Uwakili.
Tigo Mnakazi Kushinda Hii Kesi.
Pongezi Kwa Msando, Mwana-FA & AY Katika Kutetea Haki Za Wasanii.
Acha kumjaza ujinga kwamba hajawahi kushindwa kesi. Muulize kesi ya Zitto ya kupinga kusimamishwa uanachama wa CHADEMA alosimamia nani alishinda?
 
Acha kumjaza ujinga kwamba hajawahi kushindwa kesi. Muulize kesi ya Zitto ya kupinga kusimamishwa uanachama wa CHADEMA alosimamia nani alishinda?
Mkuu Tuweke Siasa Kando Kwani
Napendezwa Na Utendaji Kazi
Wa Chadema Na Vyama Vyote Bila
Kuwa Biased.
Kwenye Kesi Ya Zitto Z.Kabwe Vs Chadema Alishinda Albert Msando
Ukitaka Kuprove Google Itakupa
Majibu.
I Stand To Be Corrected.
 
Mahakama kuu hii leo imeitupilia mbali Rufaa ya kampuni ya Tigo Tanzania juu ya kesi iliotolewa maamuzi May 12, 2016 ambapo kampuni ya Tigo ya Tanzania iliamriwa kuwalipa wasanii
Ambwene Yessaya ‘AY’ na Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA; kitita cha shs Bilioni 2.1.

Leo pia maamuzi yametolewa tena kuwa ni lazima Tigo Tanzania iwalipe A.Y na F.A Bilioni 2.1 na hivyo kufanya wasanii hawa kushinda tena kesi hii ambayo imechukua zaidi ya miaka 5 mpaka kuja kuisha leo.

Wasanii hao waliishtaki kampuni ya Tigo kwa kutumia nyimbo zao kama miito (caller tunes) zikiwa na sauti zilizo katika mfumo wa miziki ambayo husikilizwa na mtu anapokuwa akimpigia simu mtu mwingine wakati akimsubiria mlengwa kupokea simu hiyo.

Nyimbo zilizotumika ni Usije mjini na Dakika moja.

a7ecf1d4077e25af2269772a84f381e7.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom