Rufaa ya Lema kuanza kusikilizwa Disemba 4; Jaji Mkuu aamua kujitoa

Status
Not open for further replies.

Skillionare

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
1,190
523
Rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Godbless Lema, itasikilizwa December 4, na jopo la majaji wapya sio wa awali!

**********************
More:

Nov 29, 2012 - Gazeti la Mtanzania:

JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, amejitoa katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Habari za kuaminika zilizopatikana mjini Dar es Salaam jana, zinasema Jaji Chande amejitoa na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luhanda, ambaye atashirikiana na Natalia Kimaro na Salum Massati, kusikiliza rufani hiyo namba 47/2012 ya mwaka 2012.

Hii ni mara ya pili, kwa Jaji kujiondoa, baada ya Jaji Mbarouk Salim Mbarouk kuwahi kujitoa.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Lema alikiri kupata taarifa za kujitoa kwa Jaji Chande.

“Nimepokea taarifa ya kujitoa kwa Jaji Chande, sijui sababu ni nini… hii ni mara ya pili kwa jaji kujitoa, najiuliza maswali mengi nakosa majibu, …unajua kesi hii si yangu, ni wananchi ambao wanashauku kubwa ya kutaka kujua hatma yangu,” alisema Lema.

Alisema baada ya kusikia taarifa hiyo, aliwasiliana na wakili wake Method Kimomogolo, ambaye alimthibitishia kujiondoa kwa Jaji Chande.

Rufaa hiyo itasikilizwa saa tatu asubuhi na jopo la majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Jaji Benard Luanda wa Mahakama ya Rufaa.

Novemba 8, mwaka huu Mahakama ya Rufani ilimwamuru Lema kufanya marekebisho ya dosari za kisheria katika muhtasari wa hukumu ndani ya siku 14, kutokana na pingamizi lililowekwa na wajibu rufaa.

Mrufani huyo alishawasilisha rufaa hiyo upya, baada ya kufanya marekebisho na tayari imepangwa kusikilizwa wiki ijayo.

Awali rufaa hiyo ilikuwa ikisikilizwa na jopo la majaji watatu, Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, Jaji Salum Massati na Jaji Nathalia Kimaro, ambapo kwa wiki ijayo hatokuwepo Jaji Othman, nafasi yake itachukuliwa na Jaji Luanda.

Lema alivuliwa wadhifa huo na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, 2012 kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Baada ya kushindwa, Lema alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupitia kwa wakili wake Method Kimomogoro kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, huku akitoa hoja 18 za kupinga hukumu hiyo.
 
Kwanini rufaa ya Lema imekuwa na danadana nyingi?
Kwa mfano
1/Ilianza kusikilizwa Arusha baada ya kimya kirefu pasipo sababu ya msingi.

2/Ikahamishiwa Dar pasipo sababu ya msingi.

3/Ilikuwa inasikilizwa na jaji mkuu Chande pasipo sababu ya msingi.

4/Ikahairishwa kwa muda usijulikana pasipo sababu ya msingi.

5/Sasa jopo jipya la majaji pasipo sababu ya msingi.

*I smell something is fishing around.
 
Kila upinzani ukishinda lazima watengue.makongoro nyerere alishinda mwaka 1995 akiwa arusha wakatengua.lema nae........... Da?
 
Waache wahangaike mwisho wa siku kitaeleweka tu, Ni ukweli usiofichika JK hataki Lema awe mbunge wa Arusha,
majaji kwa kubanywa na Tundulisu wanataka kujenga heshima- fear play-.

Majaji wote wa jopo la kwanza ni wenye msimamo... bado tunafarijika kama Jaji Masati atakuwepo, Jk atagonga mwamba tena...
 
Mhhhhh walishaona Lema atashinda kwa hiyo JM anaona asije akamwangusha Boss wake!! Kama haki itatendeka Lema atashinda!! Ile kesi hata mwanafunzi wa sheria mwaka wa kwanza tena certificate angeweza kabisa kujua Lema ni mshindi!!
 
Status
Not open for further replies.
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom