Rufaa ya Lema Arusha: Kesi yaahirishwa hadi Oktoba 2, 2012

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,651
2,627
Hali ni tulivu hapa arusha na hapa nipo mtaa wa Goliondoi ulinzi ukiwa umeimarishwa jijini.NTAKUWA NAKULETEA KINACHOENDELEA POPOTE HAPA JIJINI JUU YA RUFAA HII YA UBUNGE WA KAMANDA LEMA..

Nitajitahidi kupenya mahakamani mitaa ya uzunguni japo makamanda wengi wanajitega wakiwa wameshawasili ili kupata fursa ya kupenya Uzio.TUTASAIDIANA na kamanda crushwise,mungi kushambulia kona zote.Rufaa hii ni gumzo hapa mjini kuanzia vijiweni,ktk daladala na majumbani.Jopo la majaji litaongozwa na Jaji mkuu Mh.Chande,Jaji Salum Masati na Mh.Jaji Natalia Kimaro..

===========
Up dates
===========

Leo hakuna lolote jipya watu wanasubiri kwa hamu siku ambayo Mahakama ya rufaa chini ya jopo la hawa majaji watatu watakapotowa maamuzi yao kuhusu rufaa hii. sasa hivi hizi ni mbwembwe tu na hakuna tija yoyote, kama hoja za msingi hata kesi iliposikilizwa mwanzoni upande wa walalamikaji hawakuwa na hoja yoyote, ndio maana nasema watu wanasubili kwa hamu uamuzi wa majaji hawa na sio tena mbwembwe za Wanasheria.

Mahakama ndo imeanza kusikiliza rufani ya mh Lema sasa hiv. Niko ndani ya mahakama na nitawaletea kila kitakachojiri hapa.

Update!
Kinachoendelea hapa ndani ya mahakama ni mvutano kati ya majaji na mawakili dhidi ya kumjumuisha AG au kutokumjumuisha katika rufani hii.

Mvutano ni kwamba AG aingie upande wa mkata rufaa au mkatiwa rufaa au rafiki wa mahakama na atetee pande zote. Lakini wakili wa AG anapingana nao na kusema hawezi kuwa upande wa wafungua shtaka maana kwenye mahakama kuu alikuwa anamtetea mshtakiwa.

Bado majaji wanashauriana hapa zaidi ya dakika 30 baada ya wakili wa AG kuambiwa achague upande wa kusimamia kati ya walalamikaji au mlalamikiwa na au kutokuwa na upande na yeye kuamua kuwa upande wa mlalamikiwa bwana Lema.

Ukumbi wa mahakama umefurika watu, nje ya mahakama watu nao wapo wengi, tunasubiri haki ya wana wa Arusha mbele ya majaji hawa

Mahakama imeagiza AG ahusishwe katika kesi hii bila kuingia katika kiini cha rufani kama necessary part.

Muda huu tunamsikiliza Natalia Kimaro anasoma rufaa, ukumbi umetulia, watu wa Arusha ni wastaarabu sana

Anaongea Alute Mughwai, naona limemkaa kooni

Anazungumza kuwa kesi hii iahirishwe kutokana na Tundu Lissu aliyetakiwa kuwepo mahakamani kutotokuwepo baada ya kufiwa na baba yake

Ameomba kesi iahirishwe hadi tarehe 2.10

Wakili mwenza wa wakili wa walalamikaji anomba kesi ihairishwe maana wakili mwenza amefiwa na baba yake ambaye ni mzee Lissu na kikao cha familia kitakaa tarehe 27 siku ya alhamisi baada ya kumaliza maazishi hivyo anaweza kuja siku ya ijumaa tar 28 hivyo anomba siku ya hukumu badala ya tar 1 oct bac iwe siku ya tar 2 oct.

Imeahirishwa hadi tar 2.10
 
Japo bado ni mapema sana lakini hebu katuhabarishe juu ya uwepo wa Chatanda, Gaudence Lyimo na Batilda Buriani hapo mahakamani.
 
Leo hakuna lolote jipya watu wanasubiri kwa hamu siku ambayo Mahakama ya rufaa chini ya jopo la hawa majaji watatu watakapotowa maamuzi yao kuhusu rufaa hii. sasa hivi hizi ni mbwembwe tu na hakuna tija yoyote, kama hoja za msingi hata kesi iliposikilizwa mwanzoni upande wa walalamikaji hawakuwa na hoja yoyote, ndio maana nasema watu wanasubili kwa hamu uamuzi wa majaji hawa na sio tena mbwembwe za Wanasheria.
 
Back
Top Bottom