Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,019
2,473
1609242319107.png
Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.

"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."

Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.

Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."


Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee

Mbunge huyo wa kike, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alisema kuwa sehemu ya barua ya tuhuma dhidi yao inazitaja tuhuma dhidi yao kama ifuatavyo:

"...ulikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama kwa kushiriki au kula njama ya kujiteua kuwa mbunge wa Viti Maalum ... [kinyume cha] ibara ya 7.7.17(q) ya Katiba... [na] kinyume cha kifungu cha Kanuni ya 10.2(iv), 10.3(iv) ya Kanuni za Chama, na pia kinyume cha Kanuni ya 3(a)(iii) na 3(e)(ii) ya Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."


1609288031151.png

Kivuli cha sehemu ya barua mojawapo iliyotumika kuwasilisha tuhuma kwa kina Mdee

Kutokana na aya hii kama ikisomwa pamoja na Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama, Mbunge huyo alizitambua na kuzitaja tuhuma sita zinazowakabili kama ifuatavyo:

Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”

Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa maana ya kuhujumu chama kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kula njama za kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kula njama za kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, jambo ambalo ni sawa na kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."

Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kuonyesha msimamo wa kuaminika kwa njia ya ama kula njama za kujiteua au kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."

Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kushindwa kujiepusha na upinzani dhidi ya maamuzi ya chama na makundi ya majungu yenye kugonganisha viongozi na wanachama wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”

"Kilichotushangaza zaidi ni kwamba, kwa tuhuma zote sita dhidi yetu walizozitaja kwenye barua ya tuhuma yenye ukurasa mmoja pekee, hakuna maelezo yoyote yenye kuonyesha nani alifanya nini, lini, kivipi, akiwa wapi, akiwa na nani, na kwa nini, jambo ambalo kisheria linamaanisha kwamba hakuna mashtaka yanayojibika tuliyopewa" anaongezea huyo Mheshimiwa Mbunge .

1609243038809.png

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema

Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “kwa hiyo, tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”

Majibu katika rufaa ya kina Mdee

Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.

Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.

Mosi, ni kuhusu tuhuma zenyewe. Tunasema kwamba, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.

Kuhusu jawabu hili Mbunge huyo alifafanua kuwa Katibu Mkuu, John Mnyika, anapaswa kujua zaidi majibu kwa kuwa kitabu chake cha dispatch kina muhuri wa Tume kuonyesha kuwa Tume imepokea nyaraka kutoka kwa Katibu Mkuu.

"Napenda watu wafahamu kuwa Bawacha waliwasilisha majina ya wanawake waliopatikana kupitia mchujo wa chama na Katibu Mkuu kuyafanyia kazi kwa kujaza na kusaini fomu zao yakiwa ni maandalizi ya kuyapeleka Tume. Kwa sasa kitabu cha dispatch cha Katibu, John Mnyika, kina Mhuri wa NEC kuonyesha kuwa nyaraka za chama zilizoandaliwa na Mnyika zilipokelewa NEC. Hivyo, ama alipeleka yeye Katibu na sasa anapindisha ukweli au ofisini kwake kuna mtu mmojawapo aliyepeleka nyaraka hizo baada ya kuwa zimeandaliwa na Mnyika. Kama mtu huyo ni miongoni mwa wabunge basi wabunge baki 18 hawahusiki. Na kama mtu huyo sio mbunge, basi wabunge wote 19 hatuhusiki na hakuna njama wanazosema," alihitimisha hoja yake Mbunge huyo.

Pili, ni kuhusu tuhuma zenyewe pia. Kusudi mtu atende kosa, lazima awe eneo la tukio. Lakini, ukweli ni kwamba, wengi wetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma ziliko ofisi za NEC na Chadema. Sisi kama viumbe wenye mwili hatuwezi kuwa sehemu zaidi ya moja kwa mpigo. Tunaongozwa na kanuni mbili, spatial locality and temporal locality (anwani ya mahali na anwani na muda). Mtu asiyekuwepo mahali fulani hawezi kutenda kosa mahali hapo,” anasisitiza Mbunge huyo.

Tatu, ni kuhusu utaratibu. Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, ibara za 6.5.1(a), 6.5.5 na 6.5.6, kila mtuhumiwa anapaswa kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kujibu ndani ya siku 14, na hatimaye kupata fursa ya kujitetea kwa mdomo baada ya kuwasilisha utetezi wa maandishi. Wao walitumia kifungu cha Katiba cha 6.5.1(d) kutuita kwa dharula ndani ya saa 48 wakitutaka kuhudhuria kikao cha uso kwa uso kwa sababu walidai kuwa kulikuwepo na sababu nzuri zinazohalalisha dharula hiyo. Lakini, hatukuona sababu ya kuhalalisha dharula hiyo. Lakini pia, kama waliona kuna dharula, Kamati Kuu ilikuwa na fursa ya kupata majibu yetu kidijitali, lakini hawakufanya hivyo. Haki yetu ya kupata tuhuma zilizoandikwa na muda wa kutosha kuandaa majibu dhidi ya tuhuma hizo haiwezi kufutwa kirahisi rahisi namna hiyo kana kwamba tuko vitani," anaeleza Mbunge huyo.

"Nne, ni kuhusu utaratibu vile vile. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.

Tano, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.

1609275551321.png

Devotha Minja (katikati) akiwa na begi lililo na kitu chenye ncha kali akiwaongoza wafuasi wa Chadema kwenye maandamano yaliyoziba njia ya kuelekea hotelini ambako kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika

"Na sita, ni kuhusu utaratibu katika suala jingine. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge

Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kwa ajili ya kuitisha Baraza Kuu ili likae, lipokee makabrasha ya mashtaka na utetezi, liyasome makabrasha hayo, liwasikilize watuhumiwa wakijieleza kwa mdomo, na hatimaye kuamua haki iko upande gani kati ya Kamati Kuu na kina Mdee.


Chimbuko la rufaa ya kina Mdee

Katika kikao cha 27 Novemba 2020, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kudai kujiridhisha kwamba kina Mdee walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kina Mdee wamefukuzwa kwa sababu ya kupatikana na makosa ya usaliti, kughushi nyaraka, kujipeleka bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum bila ridhaa ya chama, na kushirikiana na wanaokitakia mabaya chama cha Chadema.

Kwa mujibu wa tamko la Mbowe, msimamo wa Chadema ni kwamba hawakubaliani na mchakato wa uchaguzi Mkuu wa 2020 na matokeo yake, na kwamba, kwa sababu hiyo, hawako tayari kufanya uteuzi wa wabunge wa Viti Maalum, kwani hilo litakuwa sawa na kuhalalisha wanachokiita wizi wa kura za Chadema.

Mbowe alisema kuwa, wakati Chama chake kikiendelea kushikilia msimamo huo, ghafla kina Mdee walionekana Bungeni Dodoma wakila kiapo cha ubunge mbele ya Spika, Job Ndugai.

Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa mbele ya Baraza Kuu dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.

Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua kwenda kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama, ili kuiomba ifanye marejeo ya maamuzi yake na kuwarejeshea uanachama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.


Magazeti ya Saed Kubenea yawaandama kimakosa kina Mdee

Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema."

1609242755263.png

Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema

Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.

Taarifa zaidi zilizoufikia mtandao wa Mama Amon zinaonyesha kwamba, tangu siku za hivi karibuni, Saed Kubenea amenunua gazeti la Raia Mwema kutoka kwa wamiliki wake wa awali. Amekuwa analitumia kuwashambulia kina Mdee tangu walipofanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 01 Desemba 2020.

Kwa mfano, katika toleo la tarehe 02 Desemba 2020, Gazeti la Raia Mwema lilikuwa na habari kuu yenye kicha cha maneno “Sakata la Viti Maalum: Limekwisha Hilo,” iliyoendelezwa kwenye ukurasa wa 3.

Habari hii iliufahamisha umma habari isiyo na uthibitisho kwamba "mkakati wa kutengeneza uasi uliratibiwa na Mdee kwa kushirikiana na wenzake watatu, Bulaya, Tendega na Agnesta."

Ndani yake kulikuwa na makala iliyoandikwa na mtu aliyejitambulisha kama Issac Kimweri yenye kichwa cha maneno, “Halima James Mdee: Kutoka Ukamanda hadi Yuda Ikarioti (uk. 9).

Makala hii pia ilichapwa kwenye gazeti la la mtandaoni, linalomilikiwa na Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisioniline.com, chini ya kichwa cha maneno: Halima James Mdee: Kutoka U-kamanda hadi yuda Iskarioti.


1609280343913.png

Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukimtuhumu Mdee kuwa na tabia za Yuda Iskarioti

Aidha, katika gazeti la Raia Mwema kulikuwepo na makala ya Mwandishi Maalum yenye kichwa cha maneno “Mdee ameshindwa kujibu maswali? (uk. 11).

Makala hii ilidai kimakosa kwamba "kitu pekee alichoweza kueleza Mdee na wenzake 18 katika mkutano huo ni uamuzi wao wa kuwasilisha rufaa ya kupinga kufukuzwa kwao na Kamayi Kuu (CC), kwenye Baraza Kuu la Taifa (BKT), basi." Makala hii ilikiuka kanuni za uandishi kwa zaidi ya 75%.

Maandiko haya matatu hayakuzingatia kanuni za uandishi kwani yalijaa habari za kupotosha ukweli na ukweli nusu nusu. Badala yake yalilenga kuharibu taswira chanya waliyo nayo kina Mdee na wenzake.

Mhariri wa gazeti hili jipya ambaye hatajwi popote gazetini, kama ilivyokuwa inafanyika hapo zamani, alibariki makosa haya. Mmiliki mpya wa gazeti hili, Saed Kubenea, ndiye anajua mhariri ni nani na ndiye anamtuma kufanya yote haya.
 
View attachment 1662261
Mhe Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.

Sasa ni wazi kwamba, Mheshimiwa Halima Mdee na wabunge wenzake 19, ambao ni viti maalum kupitia Chadema, watarudishiwa uanachama wao asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la Chadema litakapokutana kusikiliza rufaa yao waliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chadema, juzi tarahe 27 Desemba 2020.

Akiongea na mtandao wa Mama Amon, Mbunge mmoja wa viti maalum, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na mashitaka. Anayataja hatua kwa hatua kama ifuatavyo:

“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushirikia katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum wakati, kitendo ambacho ni kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi.”

“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia cheo chake, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama.”

“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”

Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”

Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu. Anasema kuwa, barua za tuhuma zilikuwa na ukurasa mmoja usio na ufafanuzi wowote unaowawezesha kufanya utetezi wenye mashiko.

Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.

“Mosi, katika suala la maudhui ya tuhuma, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.

“Na unajua baadhi yetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma. Ni kwa vipi tumepewa tuhuma eti za kula njama na kujiteua?” anauliza Mbunge huyo.

“Pili, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.

“Na tatu, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.

Sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kuitisha Baraza Kuuu ili kusikiliza na kuamua rufaa hizi kumi na tisa.

Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi huo wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mujibu wa ibara ya 5.4.4 ya Katiba ya Chama baada ya kuridhika kwamba walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chama kwa kushiriki au kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum huku wakijua na kufahamu kwamba Kamati Kuu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo kwa mujibu wa ibara ya 7.716(q) ya Katiba ilikuwa bado haijafanya uteuzi.

Kamati Kuu baada ya kujadili tuhuma hizo iliridhika kwamba kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha Kanuni ya 10.2(iv), na kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama, na pia ni kinyume cha Kanuni ya 3(a)(i), 3(a)(iii) na 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.

Aidha, Kamati Kuu iliwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.

Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.

Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.

Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwasgutumu wabunge hawa kwa sababu ya madai kwamba, uamuzi wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama ni sawa na kuanzia mapambano ndani ya Chadema.

Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.
Hisia zangu zinaniambia mmojawapo wa wale 19 ni Mama Amon mwenyewe.

Ni hisia tu
 
Yote umeandika kipindi anaongea dah.

Hii ni habari mbaya kwa Hilda Newton ila kwa usawa huu wa Magufuli unategemea nani aache ubunge wa kula M12 monthly na allowance juu, aende kulima matikiti ambayo yanakauka kwa ukame na kupasuka, acha watete matumbo yao
 
Mama Amon, nyie hamjakisaliti CHADEMA, mmetusaliti sisi tusio wanachama wa chama chochote ila tuliweka imani yetu kwenu.
Dawa ya upumbavu wenu ni kichapo tu kwa miaka yote mtakayokaa bungeni, next time mtajifunza umuhimu wa kuweka maslahi ya umma mbele kuliko huo mtumbotumbo wako uliojaa mbalaga na makatapela na kisyesye na kifughe na kipome
Bujibuji, haki ya mtu hauliwi!
Tulia sindano ikuingie!
 
Kwa majibu hayo ni wazi kuwa hao Covid hawana hoja na wanapoteza muda wao kung'ang'ana kuwa sehemu ya Chadema!
Tunalitaka baraza kuu lipigie mstari maamuzi ya kamati kuu! Hili suala liishe na hao Covid wabaki wabunge wa mfukoni wa Ndugai!
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom