Rufaa ya kesi yamtesa kajala

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,142
13,216
[h=1][/h]


Msanii Kajala Masanja.
Stori: Imelda Mtema
MWIGIZAJI Kajala Masanja amesema amekuwa akikosa usingizi usiku kutokana na mawazo ya rufaa iliyokatwa na mumewe, Faraja Chambo hivi karibuni.
Kajala na mumewe walikuwa wakikabiliwa na msala wa kutakatisha fedha ambapo miezi kadhaa iliyopita mwigizaji huyo aliachiwa huru baada ya kuamriwa na mahakama alipe faini, mumewe akaendelea kusota gerezani kwa kushindwa kulipa faini.
Mumewe huyo amekata rufaa na kuomba kesi hiyo isikilizwe upya hivyo kusababisha Kajala aingiwe na hofu ya kutupwa tena Segerea kwa mara nyingine.
“Mara nyingi naweza kulala kidogo tu nikishtuka ndiyo siwezi kulala tena kwa sababu muda mwingi nawaza kwa nini matatizo yanikumbe mimi kila wakati? Inaniuma,” alisema Kajala.



 
Back
Top Bottom