Rufaa ya Amatus Liyumba yatupiliwa nje na Mahakama Kuu

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,469
2,000
Kuna habari kuwa Rufaa ya Amatus Liyumba imetupiliwa nje na Mahakama Kuu
 

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,215
2,000
Kuna habari kuwa Rufaa ya Amatus Liyumba imetupiliwa nje na Mahakama Kuu
Thats one of the the best things that LIFE BRINGS along in life..
Naombea iwe kweli ili wenye tabia yake wajifunze!
Fedha si jawabu la kila kitu bana...vilio vya wanyonge pia vinasikika.
 

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
6,979
2,000
Liyumba - Nadhani ungeachana na RUFAA ukaendelea kukaa hapo kwenye "private cell" Ukonga then in the next few month "voila"
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
207,583
2,000
Hebu tujikumbushe yaliyomsibu ni yepi hadi leo siku ya hukumu..........................Pole Liyumba mshahara wa dhuluma ni laana tu............

Hatima ya Liyumba kujulikana leo Monday, 20 December 2010 20:34

James Magai
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inategua kitendawili cha hatima ya kigogo wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba anayetumiakia kifungo cha miaka miwili jela kwa kutoa hukumu ya rufaa yake kupinga adhabu hiyo.


Liyumba alihukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Mei 24 mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka akiwa mtumishi wa BoT.

Hata hivyo, Mei 28 Mei mwaka huu, Liyumba kupitia jopo la mawakili wake wakiongozwa na Majura Magafu, alikata rufaa Mahakama Kuu huku akitoa sababu 12 za kupinga hukumu hiyo.

Habari zilizolifikia Mwananchi na kuthibitishwa na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Liyumba zinasema kuwa hukumu ya rufaa hiyo, itasomwa leo asubuhi na Jaji Emilian Mushi aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo.

"Ni kweli, ndio nimeletewa 'samasi' sasa hivi ya kunijulisha kutolewa kwa hukumu hiyo kesho (leo) asubuhi ," alisema wakili Magafu alipoulizwa na Mwananchi.

Magafu akisaidiana na mawakili wengine Jaji Hilary Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo, walidai kuwa mahakama hiyo ilimtia hatiani Liyumba kimakosa.

Walisema kifungu cha 96(1) kilichotumika kumshtaki Liyumba, hakitoi adhabu ya kifungo.

"Ifamahimike kuwa kifungu cha 96(2) hutoa adhabu ikiwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi ya umma yalifanywa kwa maslahi ya mtuhumiwa," walisema mawakili hao.

Liyumba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa BoT, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na mahakimu wawili kati ya watatu waliokuwa wakisikiliza kesi yake ambao ni Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa.

Hata hivyo, kiongozi wa jopo hilo Edson Mkasimongwa, alitoa hukumu yake ambayo ilimwona Liyumba kuwa hana hatia.

Mahakimu hao walimtia hatiani Liyumba katika shtaka la kutumia madaraka vibaya katika mradi wa ujenzi wa majengo ya ghorofa pacha yaliyo kwenye viwanja vya ofisi za makao makuu ya BoT.

Katika kesi ya msingi Liyumba alikuwa akituhumiwa kutumia madaraka yake vibaya kwa kufanya mabadiliko katika mradi huo na kusababisha ongezeko la gharama za mradi kutoka dola 73.6 milioni za Kimarekani hadi dola 357.6 milioni za Kimarekani.

Awali alikuwa akikabiliwa na mashtaka mawili, lingine likiwa ni kuisababishia serikali hasara ya Sh221 bilioni katika mradi huo, lakini akashinda shtaka hilo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom