Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
RUFAA ya kupinga matokeo ya ubunge katika Jimbo la Ubungo iliyokatwa na aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hawa Nghumbi dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo John Mnyika itaanza kusikilizwa Desemba 7 mwaka huu katika Mahakama ya Rufaa.
Rufaa hiyo inatarajia kusikilizwa mbele ya jopo la Jaji Salum Massati, Jaji Nathalia Kimaro na Jaji Catherini Oriyo. Nghumbi alifungua kesi akipinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi yaliyompa ushindi Mnyika kwa madai kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu, kanuni na sheria za uchaguzi katika uchaguzi huo.
Hata hivyo Mei 24, mwaka huu, Jaji Upendo Msuya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam alitupilia mbali maombi ya Nghumbi na kuthibitisha Mnyika kuwa Mbunge halali wa Jimbo la Ubungo.
Katika kesi hiyo, Nghumbi aliiomba Mahakama ibatilishe matokeo hayo kwa kuwa uchaguzi haukuwa wa haki, alikuwa na hoja tano ambazo Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za Umoja wa Wanawake (UWT) na kutumia Laptop za Mnyika kuhesabu kura.
Aidha kuingia watu wengi wa Chadema katika chumba cha kuhesabia kura, kuwepo kwa kwa kura hewa 16,000, kukosewa kwa karatasi za kujumlisha kura (form). Katika hukumu hiyo Jaji Msuya alisema Nghumbi alishindwa kuthibitisha madai yake na kuonesha jinsi yalivyoathiri matokeo ya uchaguzi huo na kutangaza kuwa uchaguzi huo ulikuwa halali.
Alisema maombi kuwa Mahakama hiyo ibatilishe matokeo yaliyompa ushindi Mnyika yametupwa kwa kuwa hakuthibitisha madai yake na kutakiwa kulipa gharama za kesi hiyo pia mashahidi wa mdai hawakuonesha wala kuthibitisha madai yaliyowasilishwa yalitendeka vipi na ni namna gani yaliathiri matokeo ya uchaguzi.
Katika madai kuwa zaidi ya kura 14,000 alizodai hazieleweki zilitoka wapi Jaji alisema alihesabu kura hizo walizopata wagombea wa vyama 16 na kubaini ni kosa tu la kibinadamu na halina uhusiano wowote na Mnyika.
Aliongeza kuwa Fomu namba 24 b ilikuwa na dosari na ndiyo ilikuwa inabishaniwa na Nghumbi ilikosewa kuandikwa. Kura halali Mnyika aliyetangazwa kuwa ni mshindi alipata kura 66,742 wakati Nghumbi kura 50,544.
Wagombea wote kura ni 132496. Alisema kuwa katika ushahidi wa mdai hakuonesha ni vipi ongezeko hilo la kura liliathiri matokeo ya uchaguzi na pia mdaiwa Mnyika anahusika vipi na ongezeko hilo.
Chanzo: HabariLeo - Dec 01, 2012