Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Lugha ya Kiingereza ndiyo iliyotujengea Tanzania. Waliosoma kwa kiingereza ndio wamejenga barabara, hospital , shule, viwanda.vyuo, mahoteli, magorofa, Wanatibu Wagonjwa kwa Elimu ya Kiingereza waliyopata hadi wanafanya upasuaji wa moyo na vichwa, Walianzisha Mabank, Posta, Simu, Miundo mbinu ya Maji, Mpangilio wa Ofisi za Umma na Mashirika. Hawajakosea.Tumedharau kiingereza na tunapoteza mno, wapo na wengine kama akina jpm waliochukia lugha hii na kuanzisha kampeni dhidi ya kiingereza ila ukweli unabaki palepale, lugha ya kiingereza ni muhimu kwa ajira za ndani au nje ya nchi ambapo kiingereza fasaha kinahitajika.
Banda ya kuona tumeshindwa kuandaa Waalimu wa English ndio tunaona English Shuleni haifai.
Nilisoma kijijini enzi hiyo ya Mwalimu Primary nikabahatika kwenda Secondary Masomo yote kwa English. Nilijitahidi kusoma kwa bidii Novel na kujifunza English hakuna Somo nilikuwa sielewi na kujibu maswali yake sawasawa.