RUDI Tanganyika RUDI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RUDI Tanganyika RUDI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpevu, Apr 9, 2011.

 1. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Jamani mie nasema, tena nanena kwa uchungu...
  Naililia nchi yangu, tena nalia kwa uchungu...
  Nchi yangu Tanganyika, ulipotelea wapi...
  Nchi yangu Tanganyika, je nikuwekee MATANGA...?

  Hivi ulipoteaje, ilhali waliokupoteza - wameshatangulia mbele ya haki...

  Nimezaliwa sijakukuta mpendwa wangu Tanganyika...
  Nakusikia tu historiani, nikibaki naduwaa...
  Hukudumu Tanganyika yangu, kweli hukudumu katu...
  Ukapotea tu punde, pale ulipopewa uhuru ule wa kujitawala...
  Nakuhitaji Tanganyika, nijivune kujiita Mtanganyika...

  Tena nimepoteza utaifa wangu wa kujiita Mtanganyika... Leo hii mie naitwa - eti naitwa mtanzania...
  Babu zangu waliokupoteza wengi wameshatoweka... Tumesaliwa na waijukuu, tena tusiokujua vema... Rudi Tanganyika rudi-tujivunie utaifa wetu...

  RUDI TANGANYIKA RUDI, RUDI NASEMA TENA RUDI!

  Kwanini Tanganyika upotezwe, ilhali mwenzako Zanzibar yupo...
  Zanzibar leo yashamiri, Tanganyika twakusomea tu hitma...
  RUDI TANGANYIKA RUDI, RUDI NASI TUKUFURAHIE

  Muda sasa umefika, nasi kukuona Tanganyika...
  Ee Mola tusikie, kuturejeshea Tanganyika yetu tena uliyotutunuku...
  Mola wetu hukukosea kutupatia nchi yetu Tanganyika... lakini wanaadam tuna mambo kwa kuipoteza nchi yetu...
  Tanganyika yangu njoo, njoo nami nikuone...
  Njoo tena kwa uwazi, TUFURAHIE UHURU WETU...

  Kwani mkoloni hakuona, kutuwekea mipaka na Zanzibar (lakini leo twang'ang'anizwa, eti shauri ya usalama)...
  Rudi Tanganyika rudi, RUDI TUKUFURAHIE.

  Wengi watajitokeza, kuubeze utanganyika wangu...
  Waila imara nitasalia, kukulilia kwa simanzi...
  Nakupenda Tanganyika yangu, na daima nitakupenda...
  Na wakubwa wanisikie, juu yako Tanganyika...
  Majukwaani twakupindisha, mithili hatukujui...
  RUDI Tanganyika RUDI, tufarijike kiuzalendo wetu
   
 2. Wit

  Wit JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 417
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu haya maneno mazito yameugusa moyo wangu,ngoja nitafakari narudi.
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  hiyo tanganyika uliiona wapi?

  nini asili ya neno tanganyika?

  kwa nini ujivunie jina ulilopewa na wakoloni na kudhararu jina ulilopewa na baba zako?

  je huamini kuwa dunia ni moja? au kuwa afrika ni moja?

  ukitaka kuvunja muungano wa Tanzania na kurudi kwenye mipaka ya carl peters, na wewe tukuite mzalendo?

  jamani, dunia na vyote viitazavyo ni mali ya Bwana, hakuna wazanzibari wala wazanzibara, watanganyika wala watanga na nyika, sote tu mali ya Bwana na alitupaa dunia iwe makazi yetu kuanzia alaska mpaka siberia, cape town mpaka ireland. mipaka yote ni man-made tu.

  TUKISHINDWA KUIJENGA TANZANIA, HATA TANGANYIKA ITATUSHINDA
  . mark carefully my words

  ubarikiwe
   
 4. KABAVAKO

  KABAVAKO JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Apr 5, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ok. there is something wrong with Mr. Lowasa, but there is something behind his political situation. He is not the most corrupt person in this country. There are others, why Lowasa and not Samwel Sitta who sold Loliondo Game reserve to Arabs. I think there is a political trick in the issues behind mr. Lowasa. Please in need your comment.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280

  etiiii?
  Sita ndo aliuza loliondo?
   
 6. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  'Nilichukua TAN toka Tanganyika halafu ZAN toka Zanzibar na kuona kuwa nchi nyingi za Kiafrika zinaishia na IA hivo nikaunganisha na kupata TANZANIA'
  Huyo ni MDOSI anaejivunia jina lake hilo!!!!!!!!!!
   
 7. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2013
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Uzuzu mtupu, yaani hujui Tanzania imetokana ni nini? Labda sio kosa lako ni kosa la waalimu wako.
   
 8. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri shahiri kizazi kinacholitumikia taifa hili kwa kiasi kikubwa leo hii hawaijui Tanganyika, ujumbe uliopo kwenye sred hii ni mzito haswaaa tena wenye machungu kwa watu makini
   
 9. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2013
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sasa hna wewe kwa kauli yako hii, unaamini kabisa kuwa umefanikiwa kuficha uzuzu?

  hata nivyo nakuombea baraka tele

  ubarikiwe sana

  Glory to God!
   
 10. m

  mujore Member

  #10
  Jan 26, 2013
  Joined: Jan 9, 2013
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaeni tuu msidai tanganyika yenu.. tutawatuma kinoma.. zanzibar tuko kama 2 mills hivi lakini tunawaburuza watu milioni arubaini...dahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh. yaani sisi tumepoa soon tunajichimbia mimafuta kimpango wetu than ya kwenu tunakula kama kawaida.. tulieni tuu mtaendelea kutufanyia makazi sisi zanzibar tunakula.. katiba inayokuja inaweka wazi namna gani tunakula vya kwetu na vya kwenu kama kawaida sio.. daeni chnu nyinyi watanganyika haraka kabisa la si hivyo kunatafuta vyote.. zazibar kidogo lakini smart kabisa...huku kwetu hapewi mtu kitu but kwenu tunajibebea tuu ma ardhi hayo... dahhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh amka jirani yangu mtanganyika amkaaaaaaaaaaaaaaa...
   
 11. m

  mujore Member

  #11
  Jan 31, 2013
  Joined: Jan 9, 2013
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 12. F

  Fursa Pesa JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2013
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 2,314
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Tanganyika haiwezi kuja iwapo vyama vyote vikuu vya upinzani havitajiunga na kuwa chama kimoja kikubwa chenye nguvu.
   
 13. N

  Nurdin moh'd JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2013
  Joined: Nov 1, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika ipo imejificha,ttzo inaona noma kujitokeza ni aibu.
   
 14. C

  CosmasMU New Member

  #14
  Feb 2, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Amen,Kubarikiwa kwafaa kwa wote bila ubaguzi, maoni yangu kwenu nyote ni kwamba, kama muungano unatakiwa kuendelea, basi ni wakati muafaka wa kuutafakari, je i nchi zipi zinazounda muungano, zingatia upand mmoja tu ndo unaonekana kung'ara, Zanzibar, Serikali, bunge n.k kasoro kutambuliwa kimataifa. Upande huu tunauitaje? Hauna bunge wala serikali yake, tunapotaka kujadili mambo yasiyo ya muungano inawezekana kweli kujadili ndani ya bunge la muungano? Tafakari kwanza, vitu vidogo vidogo ndivyo huleta mikwaruzano isiyoisha, amin nakwambia, suluhu ya kweli ya muungano huu ni kutatua kero, hasa zile ndogondogo ambazo wengi kwa kufikiria makubwa makubwa pekee wana zi (overlook).

  Raia wa sasa wanauelewa mkubwa wa mambo, wanahitaji majibu ya maswali mengi sana ya muungano ambayo yakikosekana, uaminifu unapotea... Kuhusu Tanganyika kuwa jina la kikoloni hiyo itakusumbua sana, na Zanzibar ni jina gani, Ziwa Victoria, Dar es salaam, Kilimanjaro, olduvai gorge n.k. unatambua kwa majina gani yaliyopewa na babu zako? Haya, je uko makini? kwani Tanganyika ni jina ambalo bado linatumika, Lake Tanganyika ni ziwa pekee ambalo limebaki kuitabulisha Tanganyika. By the way majina siyo issue kwani ukisema Tanzania maanake ni muunganiko wa majina Tanganyika na Zanzibar, sasa kwa nini Zanzibar nalo lisife au Tanganyika lisiwe re-deemed? Wasiwasi wenu ni nini hapa?

  Ni LAZIMA (eminent) kwamba mjadala huu uwe chanya, siyo kuhusisha kufikirimioyo (emotions) bila akili kufikiri.... Muhimu ni kwamba mjadala uendelee na muafaka ufikiwe, siyo mwenzio anajadili unamkejeli, huko ni kushindwa kwa hoja, toa hoja yako kwa unyoofu wake iipinge hoja ya mwingine, na namna hiyo tunaenda, si hoja ya kukashfu. Hata ikitokea an independent third party kuangalia credebility ya hoja zenu atavutwa kuwasoma.

  I presented.
   
 15. H

  Honestdeos Member

  #15
  Feb 5, 2013
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuvunja muungano hauwezi kuwa suluhisho la matatizo yetu.

  Zaidi sana itachochea ubaguzi; tukisuluhisha matatizo yetu ya kichumi, kijamii, kimaendeleo mvutano kuhusu huu muungano utafutika kwa sababu hakuna mtu atakaye kuwa na lawama juu ya mwenzake.
   
 16. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Huyo mdosi anaitwa Mohamed Iqbal Dar
   
 17. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Enzi za Mwinyi, Sitta alishika nyadhifa ikiwamo kuiongoza Maliasili na Utalii.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2013
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Tanganyika sio tatizo letu.

  Ukiumwa kansa, panadol haisaidii.
   
 19. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2013
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,577
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Sawa sawa kabisa na naona huyo mdosi na familia yake wanajivuna kwa maana ya kutoa jina la nchi na hata mji wanao (bolded) wakati kwao Bombay wameishabadilisha jina hilo siku nyingi na kuuita mji wao jina la asili-Mumbai.
   
 20. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2013
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Unadhani Tanganyika ni taifa la nani? Linastahili kuwepo au la..!
   
Loading...